Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwamuzi mashuhuri wa soka kutoka Somalia, Omar Artan, amezuiwa kuingia Marekani licha ya kuwa miongoni mwa waamuzi 52 walioteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuchezesha mechi za Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika nchini Marekani, Canada na Mexico.
Artan, ambaye angekuwa Mwamuzi wa kwanza kutoka Somalia kuchezesha fainali za Kombe la Dunia, alizuiwa kuingia nchini humo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami mwishoni mwa wiki iliyopita licha ya kuwa na visa halali ya kusafiria. Baada ya kuzuiwa, alirejea Istanbul, Uturuki, ambako amekuwa akiishi kwa miezi ya hivi karibuni.
Soma: Orodha ya Waamuzi wa Afrika watakaochezesha mechi za FIFA World Cup 2026
Artan alitajwa kuwa Mwamuzi Bora wa Afrika wa Mwaka 2025 na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Rais Donald Trump aliweka marufuku ya kusafiri (travel ban) kwa raia wa Somalia na nchi nyingine kadhaa kuingia Marekani kuanzia Juni 9, 2025, akitaja sababu za usalama wa taifa, udhaifu wa mifumo ya uhakiki wa wasafiri, na changamoto za nyaraka za utambulisho katika baadhi ya nchi husika.
Kwa Somalia, vikwazo hivyo vinajumuisha:
Pia, Soma: Mataifa matano Afrika yanapaswa kuilipa Marekani dola 15,000 kwa shabiki mmoja Kombe la Dunia
The Athletic FC waliripoti kuwa Mashabiki kutoka nchi za Algeria, Ivory Coast, Cape Verde, Senegal na Tunisia wanapaswa kila mmoja kulipa kiasi cha dola 15,000 ambayo ni sawa na Tsh. Milioni 38 kama kianzio iwapo wanataka uhakika wa kwenda Kombe la dunia 2026.
Marekani walisema wamefanya hivyo ili kuondokana na wimbi la Raia kukaa nchini mwao kinyume na sheria.
Mijadala mingine kuhusu Kombe la Dunia;
Soma: Orodha ya Waamuzi wa Afrika watakaochezesha mechi za FIFA World Cup 2026
Rais Donald Trump aliweka marufuku ya kusafiri (travel ban) kwa raia wa Somalia na nchi nyingine kadhaa kuingia Marekani kuanzia Juni 9, 2025, akitaja sababu za usalama wa taifa, udhaifu wa mifumo ya uhakiki wa wasafiri, na changamoto za nyaraka za utambulisho katika baadhi ya nchi husika.
Kwa Somalia, vikwazo hivyo vinajumuisha:
- Kusitishwa kwa utoaji wa visa nyingi za kuingia Marekani kwa raia wa Somalia.
- Kuwekwa kwa Somalia kwenye orodha ya nchi zinazokabiliwa na marufuku kamili ya kuingia Marekani.
- Ukaguzi mkali zaidi wa wasafiri kutoka Somalia kwa misingi ya usalama na uhamiaji.
Pia, Soma: Mataifa matano Afrika yanapaswa kuilipa Marekani dola 15,000 kwa shabiki mmoja Kombe la Dunia
The Athletic FC waliripoti kuwa Mashabiki kutoka nchi za Algeria, Ivory Coast, Cape Verde, Senegal na Tunisia wanapaswa kila mmoja kulipa kiasi cha dola 15,000 ambayo ni sawa na Tsh. Milioni 38 kama kianzio iwapo wanataka uhakika wa kwenda Kombe la dunia 2026.
Marekani walisema wamefanya hivyo ili kuondokana na wimbi la Raia kukaa nchini mwao kinyume na sheria.
Mijadala mingine kuhusu Kombe la Dunia;
- Trump: Kwa kweli ‘sijali’ kama Iran itashiriki Kombe la Dunia 2026
- Orodha ya Waamuzi wa Afrika watakaochezesha mechi za FIFA World Cup 2026
- FIFA yakataa ombi la Iran la kucheza mechi za Kombe la Dunia nje ya Marekani
- DR Congo yaiomba FIFA kurejesha Fedha za Tiketi za Kombe la Dunia 2026 kutokana na Vikwazo vya Ebola vilivyowekwa na Marekani