Uchaguzi 2020 Mwana-CHADEMA aliyeshiriki vurugu zilizosababisha mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti atubu mbele ya Mama Samia!

Uchaguzi 2020 Mwana-CHADEMA aliyeshiriki vurugu zilizosababisha mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti atubu mbele ya Mama Samia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Akiongea mjini Rungwe leo mmoja wa vijana aliyekuwa CHADEMA na sasa amehamia CCM amekiri na kutubu dhambi zake kwamba alishiriki maandamano ya Nyololo, Morogoro na Kinondoni yaliyopelekea mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti.

Kijana huyo ambaye alikuwa anaongea mbele ya makamu wa Rais mama Samia na wananchi wa Rungwe amesema maandamano hayo yalikuwa ni utekelezaji wa Azimio la Mwanza lililokuwa linatekelezwa na CHADEMA.

Amesisitiza kuwa akiwa CHADEMA ameshiriki uharamia mwingi na kufungwa jela mara kadhaa kwa maslahi ya chama lakini sasa imetosha anaomba toba kwa Mungu na anaamini CCM ni mahali salama tofauti na CHADEMA walikosheheni wahuni.

Nitajaribu kuweka clip ili mumsikie ninyi wenyewe, inatisha.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mmebakiza maigizo tu, hayatawasaidia.
Baada ya miaka mitano ya giza kwa waTz, 28/10 lazima mtavuna mlichopanda.
1600699048861.png
 
Umemsikiliza lakini bwashee?!
Bwashee,
Kuna Mtu alimwagiwa tindikali, alikua anatembezwa na Madilu, kuna mwingine alilia bungeni, shughuli za bunge zikasimama, speaker akambembeleza! Kuna Masai wa Siha, kuna mlevi wa Tarime huko! Upo Wewe na na paschal, lakini CHADEMA ni mbele kwa mbele, samaki hana rivasi!
 
Mwanachadema aliyeshiriki vurugu zilizosababisha mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti atubu mbele ya mama Samia!
Anatakiwa apelekwe mahakamani akahukumiwe kifo, kutubu kwa mama Samia haiondoi kosa la mauaji. Yaani waendesha mashtaka wanatafuta mtu aliyefyatua risasi, kumbe yupo bhana?
 
Pigeni propaganda zenu zote mzijuazo ila boss wenu achomoki mwaka huu, yaani hesabuni genge lenu la hapo lumbumba mwaka huu ndio mwisho na kwa hasira lazima tulipige kiberiti, tuone sura zenu vizuri, msije mkawa chawa maanake roho zenu shetani ana nafuu.
 
Akiongea mjini Rungwe leo mmoja wa vijana aliyekuwa Chadema na sasa amehamia CCM amekiri na kutubu dhambi zake kwamba alishiriki maandamano ya Nyololo, Morogoro na Kinondoni yaliyopelekea mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti.

...
Yale yale ya Tesha wa Igunga kumwagiwa tindikali na Chadema na kugeuka mtaji wa kisiasa CCM. Kwamba huyu alishiriki mauwaji ya Mwangosi halafu miaka mingine mingi baadaye akashiriki ya Aquilina; huyu kweli alikuwa kwenye "kazi maalumu" no wonder amerudi kwa waliomtuma. By the way, Nyololo iko Iringa sio Morogoro muwage na kumbukumbu!
 
Hata waliokuwa wanaumwa mahospitalini zilikuwa ni movie, aliyempa kuku ilikuwa Kiki, aliyemuuzia Hindi ilikuwa ni Kiki. Tunasubili mtuletee na mwanachadema aliyempa MANGULA sumu naye aseme alikuwa Cdm. Poor politicians with cheap politics.

Kumpa kumchagua salima kikwete ni sawa na kupoteza nafasi ya uwakilishi kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom