Uchaguzi 2020 Mwana-CHADEMA aliyeshiriki vurugu zilizosababisha mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti atubu mbele ya Mama Samia!

Uchaguzi 2020 Mwana-CHADEMA aliyeshiriki vurugu zilizosababisha mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti atubu mbele ya Mama Samia!

Shida ya kudandia mambo,kwahiyo CHADEMA inamiliki bunduki na police..policeccm walimuua ushahidi upo utadumu karne n karne
 
Ina maana yeye ndiye alivaa sare za polisi na kumfyatulia bomu Mwangosi Kisha akahukumiwa na kufungwa kule Iringa? Kwa maana nyingine polisi wameanza kutubia siyo?

Huu ni ujinga na upumbavu wa kuichagua polisi ambao walikuwepo eneo la tukio Tena yote kuwa walihisika kwa kumlea huyo anayetubu! Na polisi walivyo wa ajabu watamuacha aende zake badala ya kumkamata na kumshtaki kwa mauaji!

CCM mmeishiwa hoja, jificheni mvunguni kukwepa aibu!
 
Kwani hao uliowataja waliuawa na maandamano au Russia?
 
Familia za hawa wahanga hawajapata haki badala yake wanasikia maisha ya ndugu zao yakitumika cheaply kwenye kampeni.
 
Ina maana yeye ndiye alivaa sare za polisi na kumfyatulia bomu Mwangosi Kisha akahukumiwa na kufungwa kule Iringa? Kwa maana nyingine polisi wameanza kutubia siyo?...
Kuna tofauti kati ya kusababisha kifo na kuua.....uwe unaelewa bwashee!
 
Siasa za kipuuzi na zisizo na mashiko mbele ya jamii ya wenye utimamu kichwani ndio hizi! CCM imeishiwa hoja hadi kuanza kutengeneza sinema za kipuuzi hivi!
 
Kwani ishu ya Mwangosi ilikuwa na maandamano? Si walikuwa wanafungua tu tawi tena hata wafuasi wa Chadema hawakuwepo?
Mwambieni hizo kick akalale nazo.
walikuwa wanafungua tawi bila wafuasi?
 
Akiongea mjini Rungwe leo mmoja wa vijana aliyekuwa CHADEMA na sasa amehamia CCM amekiri na kutubu dhambi zake kwamba alishiriki maandamano ya Nyololo, Morogoro na Kinondoni yaliyopelekea mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti...
Hapakuwa na vurugu,msidanganye watu.Wilbroad Slaa yupo na Kamhanda naamini hajafa.Ilikuwa utumiaji wa nguvu wa Polisi bila sababu za msingi.

Huyo ni kama yule babu mbeba jogoo.
 
Sasa sisi tufanyeje .

Badilika Mbatizaji haya mambo mengine yanazidi kukushusha.
 
Mzee Mgaya
Akiongea mjini Rungwe leo mmoja wa vijana aliyekuwa CHADEMA na sasa amehamia CCM amekiri na kutubu dhambi zake kwamba alishiriki maandamano ya Nyololo, Morogoro na Kinondoni yaliyopelekea mauaji ya Mwangosi, Aquilina na muuza magazeti.

Kijana huyo ambaye alikuwa anaongea mbele ya makamu wa Rais mama Samia na wananchi wa Rungwe amesema maandamano hayo yalikuwa ni utekelezaji wa Azimio la Mwanza lililokuwa linatekelezwa na CHADEMA.

Amesisitiza kuwa akiwa CHADEMA ameshiriki uharamia mwingi na kufungwa jela mara kadhaa kwa maslahi ya chama lakini sasa imetosha anaomba toba kwa Mungu na anaamini CCM ni mahali salama tofauti na CHADEMA walikosheheni wahuni.

Nitajaribu kuweka clip ili mumsikie ninyi wenyewe, Inatisha.

Maendeleo hayana vyama!
JamiiForums-1335650171.jpg
 
Kwani ishu ya Mwangosi ilikuwa na maandamano? Si walikuwa wanafungua tu tawi tena hata wafuasi wa Chadema hawakuwepo?
Mwambieni hizo kick akalale nazo.
mtajisema wenyewe, ipo siku na wewe utatubu huku ukibubujjikwa machozi..
 
Back
Top Bottom