Mwana FA Aahidi Kuboresha Miundombinu kwa Watoto Wenye Mahitaji Maalum Muheza

Mwana FA Aahidi Kuboresha Miundombinu kwa Watoto Wenye Mahitaji Maalum Muheza

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) ameahidi kutatua kero zinazowapata Watoto wenye mahitaji maalum Wilayani Muheza ikiwemo kuboresha miundombinu katika Shule wanazosoma, kuwapatia vifaa vya michezo na kuweka uzio katika Shule zao.

Amesema hayo katika hafla ya chakula cha pamoja na Watoto wenye mahitaji maalum, iliyofanyika Wilayani Muheza Mkoani Tanga “Hili jambo tunalolifanya ni Ibada, kuna ulezi na kuna ulezi wa Watoto wenye mahitaji maalum na lenyewe linaongezeka juu yake, huu ni ulezi unaotaka moyo wa huruma na dhamira ya dhati, hongereni sana Walimu na Wazazi wenye Watoto wenye mahitaji maalum”

Kwa upande wake DC wa Muheza, Zainab Abdallah amesema “Tumedhamiria Wana Muheza kuweka kipaumbele kwenye elimu, Wana Muheza mna bahati kupata Kiongozi kama Mwana FA, kama sio yeye kuweka mkono wake huenda tusingefanikiwa, namshukuru na kumpongeza Mh. Rais Dkt. Samia kwa mapenzi yake mema kwa Watoto wa Taifa hili, anahangaika usiku na mchana kuhakikisha Watoto wetu wanasoma kwakweli ni jambo la kumuombea dua”
 
.
 

Attachments

  • Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma (Mw...mp4
    26.4 MB
Siku hazigangi, wanaanza enda majimboni, na wananchi watashangilia!!!
 
Back
Top Bottom