Mwana FA amkana Baba yake mzazi

Swadaqta !!
Naomba usone kisa hiki

Kisa kama hiki kilitokea huko (jina na mji kapuni) " Jamaa baada ya kufariki dunia akaamua kwenda hadi mlangoni mwa jahanamu kuulizia maSwahiba zake...!! Akajibiwa kuwa msawahiba zako uliowaacha duniani walishatubu baada ya kifo chako, hivo hapa hawapo !! "

Jee msomaji umejifunza nini ktk issue hii !!
 
Mkuu bora umejibu maana hawajielewi na lawama kwa wanawake
watu wanajibu kirahisi bila kujali, wajaribu kuvaa viatu vya watoto yatima ndo watajua ugumu uliopo.

unakuzwa na watu baki kwa tabu kama mtoto yatima halafu baba yuko bize na mama mdogo aisee nisipokukana hadharani sijui tu!

kama amethubutu kunikana siwezi hata kufanya vibarua nipate pesa ya kula hata mimi sioni ajabu kukukana ukiwa na ndevu na mvi zako!
 
Kama Una Nia huyo Baba hasilalamike
 
Japo Sijaelewa vizuri wote hapo walikuwa wamefikwa na umauti, Ni kwamba tukitubu tunasamehewa na kwenda mahali salama
 
ni imani yangu hii mifano ya wasanii itatufundishia watu!
 
Mkuu nakuelewa vizuri
 
hujapitia magumu wewe!
Ni kiri tu mkuu, mimi ni miongoni mwa waliopitia hii dhahama
unalelewa kwa kuhamahama leo kwa aunt kesho kwa mjomba kesho kutwa kwa babu kisa baba ako kakukataa yuko bize na mambo yake?
Hadi sasa naishi kwa Anko tangu nikiwa na miaka 7, anko kanipeleka shule maana mzee alikataa na hata ndugu zangu wengine waliokuwa wanaishi na mzee walikataliwa kupelekwa shule. Maza alikomaa kivyake akawapeleka shule ndugu zangu wengine aliokuwa anaishi nao, Bro wangu alianzia MEMKWA hatimaye alifanikiwa kumaliza form 4 na Mungu akajalia akasonga mbele japo hajapitia Advance.

Mimi nilikomaa kwa Anko kibishi japo tunajua namna ya malezi kwa wasiokuwa wazazi wako yalivyo, nilisoma primary, secondary(O-level & A-level) hadi Chuo nishahitimu nipo mikononi mwa Anko huku Mzee yupo mzima wa Afya tu na hajawahi kuchangia hata kidogo kwenye malipo ya masomo yangu.

Nikifikiria mzee alivyokuwa mkatili ninaumia sana ila naishia kusema hakujua alitendalo na nishamsamehe, life linaendelea..

Wazee mara nyingi wanakuwa na viburi sana lakini pia wanawake nao wanachagia katika haya mambo ikiwemo kupandikiza chuki juu ya wazee kwa watoto.
kama ni mimi sitamsamehe niko radhi nigawane na walionisaidia kipindi ninahitaji msaada!
Mimi nishamsamehe, tunakula sahani moja kote kote na walionilea na yeye pia
huo ubaba wa uzeeni ni sawa na marafiki wanaokupenda ukiwa nacho( hawa napiga chini).
Mara nyingi hawa wazee huwa wanaviburi ila hawafikirii mbali yatakayotokea hasa wakifika umri wa uzee.

Laiti wangejua siku moja wataachwa na watoto wao kama walivyowaacha wao wasingethubutu kufanya hivyo
 
Mwana FA cannot do this.
 
Unajua watu wengine sijui wameumbwaje ? Hawana hata aibu , mi siwezi , ningekufa kigumu Tu , kama nilikata mtoto hiyo ni forever
Wanakuwa wamejisahau sijui..maana wewe mwenyewe ulimkana mtoto halafu akikukana unalia ....maajabu
 
Kuna mwaka flan wakati wa tuzo za Kili,the Kilimanjaro Band ilishinda tuzo akapanda huyu mzee akiwa kasindikizwa na Mwana FA na mbele ya umma mwana FA alisema ni baba yake mzazi,tangu siku hiyo hadi leo ndo najua huyu mzee pichani chini mwenye nguo nyeupe ndiye baba halisi wa FA
 
You are the greatest!!! Amani kwako!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya familia magumu sana,huwezi jua nini kilitokea hapo awali, so tuache kuhukumu sana na kulaumu bila kujua historia ya mtu.....nina rafiki yangu Baba yake alimkataa tangu mchanga na alikuwa na uwezo mzuri tu wa kumlea,jamaa alipomaliza form 4 akaenda kwake kuongea naye hasa baada ya kustrugle sana hadi hatua ile,kilichoshangaza jamaa akamtimua ila mkewe akawa mkali kuwa mbona anafanana sana na mwanao nawewe pia,dingi akasema sina mtoto zaidi ya hawa.

Mama wa kambo akamsaidia nauli akaondoka,akapambana hadi kamaliza chuo kikuu na kadigrii....familia yake watoto wakakataa shule na hakuna aliyefanikiwa hata kufika form4.....dogo alipomaliza chuo akapata kazi nzuri dingi aliposikia na alikuwa amestaafu hapo ndo usumbufu ukaanza,jamaa yangu aliapa yule dingi hata awe anakufa hapo no way atahangaika.

So huwezi jua Mwanafa kapitia maisha gani,na ukizingatia mzee nimwanamziki inawezekana starehe zilikuwa nyingi na kusahau familia
 
Labla baba mlezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…