Mwana FA asema wimbo "Muziki" wa Darassa umerudisha heshima Kwa wasanii wa hip hop

We mtoto wakubwa wakiongea uwe unatuliza vikalio vyako vyeusi kwanza...we FA unamjua kweli??..yaani FA wa ingekua vipi , amekufa kwa ngoma, mabinti et etc...we dogo kweli umekosa adabu
Huyo dogo hamjui FA kabisa yaani anataka kumfananisha Darasa mwenye hit songs tatu na Mwanafa? Kwa sababu hakuwepo miaka ile si vibaya kumshauri akasikilize hizi tracks halafu aje kusafisha utumbo wake;
1.Mabinti
2.Alikufa kwa ngoma ft.Jide
3.Hawajui ft. Jide
4.Msiache kuongea ft. Jide
5.Ingekuwa vipi ft. Jay MO
6.Unanitega ft. Noorah
7.Yalaiti ft. Lina
8.Habari ndio hiyo with AY
9.Asubuhi with AY ft. Q.Chillah
10.Mfalme ft. G.Nako
11.Tuliza boli
12.Bado nipo nipo
13.Jukumu letu with Prof.Jay
14.Wanapendana ft. Dully Sykes
15. Bila kukunja goti with AY ft. J.Martins
16. Kiboko yangu ft. Alikiba
Na nyinginezo
Hizo ngoma zote zilifanya vizuri, Darasa bado sana kumfananisha na Mwanafa
 
Mkuu, Darasa sio mwanamuziki mgeni kwenye industry hii, wala hii sio hit song yake ya kwanza unaikumbuka sikati tamaa? (aliomshirikisha mavoko kabla hajaenda WCB?) unaizungmziaje km utanipenda nayo ilisumbua sana kwenye majukwaa ya fiesta, too much je? Sasa unaweza ukaona hapa ni kazi juu ya kazi yaani bamba to bamba! Kinatoka kitu kinaingia kitu!


Acha maneno weka [HASHTAG]#muziki[/HASHTAG] [emoji443] [emoji445] [emoji441]
 
Mwanzo mzuri sana kwa mwanamuziki darasa, ameonyesha uwezo mkubwa sana sana!

Kama atapata mshauri mzuri wa masuala ya muziki basi atakuwa nyota wa tanzania. Kamwe asibweteke.
 
Na ngoma alikufa kwa ngoma na jukumu letu alifanya vizuri ni miongoni mwa ngoma zake conscious.
 
Kila kitu kina wakati wake, Binamu alishafanya mengi makubwa ambayo pengine Darasa anayaota
Makubwa yepi au ndio yale ya kutunishiana misuli na lady Jaydee. Tangu kipindi kile huyu dogo ajichomeke kwenye bifu la lady jaydee na clouds nilimdharau sana mpaka leo simkubali kabisa hana tofauti na mademu wa kitaa. Anyways sina maneno ya kwenye kanga acha muziki uendelee
 
Ile chorus ya Ben Paul angeirudia tena mwishoni ingekuwa poa sana.. anyway ile ni bonge ya club bang
 
Kwa tafsiri nyepes is iyo na ukakasi ni kwamba "mziki" umeifunika "dume suruali " isifanye vzr
 
Mkuu labda kama una chuki binafsi na FA lakini ukiacha mambo mengine Mwanafa amefanya makubwa kwenye bongofleva tofauti na Darasa. Kitendo cha kudumu kwenye huu mziki kwa muda mrefu si jambo dogo, track zake almost zote zilifanya vizuri, achana na local awards alizopata.
 
Mwenzako anasifia wimbo wa darasa umeleta heshima ya hip hop ambayo HAIKUWEPO, halafu wewe unasema keshafanya mengi,mengi hayo yepi,si angejisifia yeye mwenyewe kama alishayafanya ........??
Hey son,una mjua mwana FA vizuri? huyu jamaa fundi sana sema kitu kimoja tu kina muangusha hajui kutoa video kali,video zake zote mbovu hazivutii labda kidoogo hii ya dume suruali na asanteni kwa kuja...
 
Hyu darassa wa juzi tu mpita njia huwezi kumfananisha na "Mwanafalsafa"...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…