Mwana FA asema wimbo "Muziki" wa Darassa umerudisha heshima Kwa wasanii wa hip hop

Mwana FA asema wimbo "Muziki" wa Darassa umerudisha heshima Kwa wasanii wa hip hop

Msanii wa muziki wa hip hop, Mwana FA amesema hatua ya mafanikio ya wimbo ‘Muziki’ wa Darassa ni hatua ambayo wasanii wengi wa muziki wa hip hop walishindwa kuifikia kwa muda mrefu.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake ‘Dume Suruali’ amesema ni muda mrefu wasanii wa hip hop walikuwa wanashindwa kutoa ngoma ambazo zitaleta ushindani mkubwa na zawasanii wa kuimba.
“Kwanza I’m happy for rap music,” FA alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Imekuwa muda mrefu hatujawahi kutengeneza nyimbo halafu zikatoka na nyimbo za waimbaji, halafu usisikie nyimbo za waimbaji na rap music ikawa vile,”
Mwana FA amesema anapenda kuona Darassa akiendelea kufanikiwa zaidi katika muziki kwa kuwa ni msanii ambaye anaujua uwezo wake katika kile anachokifanya.
Wimbo ‘Muziki’ wa Darassa umeweza kufanya vizuri kwenye chart mbalimbali za muziki. Pia kupitia channel ya mtandao wa YouTbe video ya wimbo huo imeweza kuangaliwa mara 1,787,074 katika kipindi cha wiki tatu.
0f33acdd5ab39079470f3c7096144f1e.jpg

Chanzo: Bongo5.com

Kawimbo kake kamelala doro naona anaanza kujipendekeza kwa Darasa...MwanaFA bwana,angenyamaza tu...na yeye aonekane yupo,hahahaaa
 
Kawimbo kake kamelala doro naona anaanza kujipendekeza kwa Darasa...MwanaFA bwana,angenyamaza tu...na yeye aonekane yupo,hahahaaa
[emoji23] [emoji23] kafikisha views 1m YouTube huko. Ndio wasanii wetu hawa
 
Kokoro one of the best songs kutengenezwa mwaka huu BARANI AFRIKA.! Yes I said it, Africa..

Alafu mama unajua unawatia wasiwasi kariakoo wataanza kuhisi unahamia CMG [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Mhhhhhh unataka kuniambia ile collabo iliyokula 'mamia ya mamilioni' na P2 sio lolote mbele ya kokoro?[emoji134]

Aaaaah wapi,watu wangu wa k/koo wananijua vyema,hawana shaka nami.
 
Tusubiri ngoma nyingine tuone itakuwaje maana wabongo hatuchelewi kumbwaga mtu nakusema hajui
 
[emoji23] [emoji23] kafikisha views 1m YouTube huko. Ndio wasanii wetu hawa

Na hiyo 1m ya FA itakua katupia yale "manuva" yetu ya "views",hahhaaaa...ananifurahishaga anapojifanya kukopi mannerisms za JayZ...this nigga tries hard
 
Mwenzako anasifia wimbo wa darasa umeleta heshima ya hip hop ambayo HAIKUWEPO, halafu wewe unasema keshafanya mengi,mengi hayo yepi,si angejisifia yeye mwenyewe kama alishayafanya ........??

We mtoto wakubwa wakiongea uwe unatuliza vikalio vyako vyeusi kwanza...we FA unamjua kweli??..yaani FA wa ingekua vipi , amekufa kwa ngoma, mabinti et etc...we dogo kweli umekosa adabu
 
Mwenzako anasifia wimbo wa darasa umeleta heshima ya hip hop ambayo HAIKUWEPO, halafu wewe unasema keshafanya mengi,mengi hayo yepi,si angejisifia yeye mwenyewe kama alishayafanya ........??
Mkuu inaelekea humfaham Mwanafa, yaani unataka kufananisha mafanikio ya Darasa na Mwanafa kwenye huu mziki?
 
Wabongo kwa kugeuza maneno hawajambo, hicho kipindi nilikiona na Mwana fa aliulizwa iwapo wimbo wa Darasa umeusumbua wimbo wa Dume suruali....akasema ni kweli na hii ni mara ya kwanza kwa nyimbo za Hip hop (Muziki na Dume suruali) kuzizidi nguvu ngoma za kuimba zilizotoka wakati mmoja.
 
Mkuu inaelekea humfaham Mwanafa, yaani unataka kufananisha mafanikio ya Darasa na Mwanafa kwenye huu mziki?
Nyinyi watu wengine vipi,amsomi kilichoandikwa au ......Yeye ndio kamsifia Darasa,sio mimi kwahiyo kama unaona yeye ana muziki mzuri kuliko Darasa basi ni nyinyi kumuambia we jamaa ndio uko vizuri kuliko huyo unayemsifia.
 
Siyo yeye tu, hata afande sele kwenye page yake alikiri kua wimbo wa darasa umewapa "ahuweni" wasanii wa hip hop amefanya kitu kilichowashinda wengi mafanikio ya darasa ni mafanikio ya wana hip hop wote waliokua wanaupigania [HASHTAG]#muziki[/HASHTAG] huu
[emoji122] [emoji122]
 
Back
Top Bottom