Mwana FA & AY - Usije Mjini

Mwana FA & AY - Usije Mjini

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Mwana FA na AY baada ya kujitoa ECT walikua wanaachia pini juu ya pini kali tupu.

Mfano hii Pini ya Usije Mjini, dah ilikua inanikosha sana kuanzia biti hadi AY anavoimba na FA kuchana.

Kuna mstari verse ya kwanza FA alisema: "... huku huku kwenye ufisadi, waliopo hawataki kurudi, ata mbunge wa kwenu yupo, uko atakuja uchaguzi.."

Hii kauli sahivi yeye ndio anaomba huo Ubunge.

Yote tisa, aisee hawa jamaa walikua wanaimba sana sema nadhani enzi izo game ilikua hailipi saana kama sahivi.
 
Hii nyimbo ndiyo nyimbo iliyoingiza hela nyingi kuliko zote za wasanii wa Tanzania..

Nyimbo ya usije mjini imewafanya mwana fa na ay wawe matajiri.

Hii nyimbo imewagharimu tigo bilioni 2 na milioni 155

Bila hii nyimbo mwana fa asingekuwa na hela za kugombea ubunge
 
Hii pesa yote waligawana wawili tu au mgao ilienda kwa wengi na vipi kuhusu kesi mwanasheria wao alikuwa nani na kwanini tigo hawakukata rufaa
 
Hii pesa yote waligawana wawili tu au mgao ilienda kwa wengi na vipi kuhusu kesi mwanasheria wao alikuwa nani na kwanini tigo hawakukata rufaa

Tigo walikata rufaa.. ila kina mwana fa wakashinda tena..

Mwanasheria wao alikuwa albert msando

Ndio pesa waligawana wote na mwanasheria wao .. ila mgao wa bilioni mbili watu watatu.. sio pesa ndogo kila mmoja anapata..

Inasemekana Mwana fa alipata milioni 600 kwenye mgao
 
Back
Top Bottom