Mwana FA: Baada ya kukaa Karantini kwa siku 28 nimepona kabisa Corona na nitagombea ubunge kupitia CCM mwaka huu

Mwana FA: Baada ya kukaa Karantini kwa siku 28 nimepona kabisa Corona na nitagombea ubunge kupitia CCM mwaka huu

Kwasasa CCM ukitaka ubunge we ulilie kupita kwenye kura za maoni baada ya hapo unakula bata
 
Hata kama hali ya korona itaendelea hivi, uchaguzi utakuwepo tu?

Labda hali izidi kuwa mbaya zaidi, lakini kama ikiwa hivihivi au kupungua basi uchaguzi upo.

Burundi wao washatoa na ratiba ya uchaguzi.

NB; Kama Corona haitaisha, Dunia itatafuta namna ya ''kuishi nayo''. Hatuwezi tukazuia shughuli mbalimbali kwa muda mrefu.... Corona ikiisha baada ya miaka 20 je ?
 
Tokea nione ile clip ya mbunge wa CCM anashindwa kuongea bungeni na kuhitimisha kuwaambia wabunge wanaomcheka "MSINIZENGUE" nimeamini kila kiumbe mwenye uhai anaweza kuwa mbunge wa CCM
Na bora agombee tu ili wazee kama hao na wengine wapishe damu changa, kazi yao ni kwa kwaa kwaaa hata pasipo sitahiri!...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwambieni aje ubungo au kawe na kama anajiweza, Mbeya mjini aonje joto ya jiwe kidogo
 
Kupitia chama letu atashinda tu..
Next election ni uchaguzi wa kura za hasira ya covid19, simwoni mwana ccm atakayepita kihalali au kwa kuiba. Na hasira ikizidi sioni mtu atakayetoka kwake kwenda kuchomwa na jua.
Jiandaeni kiakili mapemaaaa kukabidhi nchi yetu, m'meichezea sana.
 
Hivi watu wanapachukuliaje bungeni pale, kuwa ni sehemu unajiamulia tu kwenda sababu una mihemko ya kutaka kuingia kwenye siasa......?!

Hivi unakuwaje msanii leo, kesho kiongozi wa kutumikia watu full time, au ndio kama vile wanavyosema kuwa siasa ni maneno matupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliku namkubali huyu kijana ila tangia suala la covid 19 kuingia nchi amekua hana hekima, au kuna kitu nyuma
 
Hivi watu wanapachukuliaje bungeni pale, kuwa ni sehemu unajiamulia tu kwenda sababu una mihemko ya kutaka kuingia kwenye siasa......?!

Hivi unakuwaje msanii leo, kesho kiongozi wa kutumikia watu full time, au ndio kama vile wanavyosema kuwa siasa ni maneno matupu

Sent using Jamii Forums mobile app
Anafuata njia ya msanii Sugu.
 
Back
Top Bottom