Mwana FA, Gerson Msigwa na viongozi husika watueleze zaidi ya Bilioni 30 za ukarabati uwanja wa Mkapa tangu 2023 ziko wapi?

Mwana FA, Gerson Msigwa na viongozi husika watueleze zaidi ya Bilioni 30 za ukarabati uwanja wa Mkapa tangu 2023 ziko wapi?

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Ni maajabu ya karne!

Tangu mwaka 2023 tulielezwa kwamba ukarabati mkubwa utafanyika katika uwanja wa Mkapa, Tukaelezwa kwamba zimeshatengwa zaidi ya bilioni 30 kwa ajili ya kazi hiyo na uwanja ukatangazwa kufungwa.

Ukijaribu kuhoji utaambiwa vyoo vimerekebishwa, Mashabiki na wachezaji wanakuja uwanjani kujisaidia haja ndogo? Hizi ni akili za wapi?

Lengo na madhumuni ya kwanza ya uwanja ni eneo la kuchezea, Inashangaza mpaka sasa pitch ni mbovu, hakuna TV, Hakuna mabango ya matangazo yanayodisplay kwa umeme, Kwa kifupi uwanja bado hauna mvuto hata kidogo!

Kumbuka hapo ni zaidi ya bilioni 30 zimewekezwa na ni zaidi ya miaka miwili imepita!

HAYA NI MAAJABU
 
Mkuu billion 30 ziliishia kwenye ukarabati wa vyoo,.

Na sasa tunasubiri bajeti ipitishwe na katibu mkuu, Hivi punde tutaanza ukarabati maana tayari mkandarasi tumempata na matarajio yetu hadi kufikia mwenzi october uwanja uanze kutumika.

My country. 😊
 
Tukiwaambia Nchi ina Majizi na Mapumbavu hamuelewi.

CCM imewafanya vijana wajikite kwenye ushabiki wa Simba na Yanga nako huko Inaabika.
  • Hakuna mchezo wa simba na yanga.
  • yanga kutolewa Mapema CAFCL.
  • Kufungiwa kwa Uwanja wa Taifa.
  • Taa kuzima mala kwa mala.
  • Kudanganywa ujenzi wa Uwanja Dodoma tangu 2017. (Mfalme wa Moroco.)
MUNGU WAPE MACHO WAONE.
 
MwanaFA jibu atakalo kwambia Bado nipo nipo bwana.
 
Ni maajabu ya karne!

Tangu mwaka 2023 tulielezwa kwamba ukarabati mkubwa utafanyika katika uwanja wa Mkapa, Tukaelezwa kwamba zimeshatengwa zaidi ya bilioni 30 kwa ajili ya kazi hiyo na uwanja ukatangazwa kufungwa.

Ukijaribu kuhoji utaambiwa vyoo vimerekebishwa, Mashabiki na wachezaji wanakuja uwanjani kujisaidia haja ndogo? Hizi ni akili za wapi?

Lengo na madhumuni ya kwanza ya uwanja ni eneo la kuchezea, Inashangaza mpaka sasa pitch ni mbovu, hakuna TV, Hakuna mabango ya matangazo yanayodisplay kwa umeme, Kwa kifupi uwanja bado hauna mvuto hata kidogo!

Kumbuka hapo ni zaidi ya bilioni 30 zimewekezwa na ni zaidi ya miaka miwili imepita!

HAYA NI MAAJABU
CCM ni tatizo
 
Maeneo yaliyopangwa yakarabatiwe ni pamoja na.
1. vyumba vya wachezaji,
2. chumba cha waandishi wa
Habari,
3.Eneo la watu mashuhuri (VVIP), 4. kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo,
5. ubao wa kuonesha matokeo,
6. kuweka mfumo mpya wa TEHAMA,
7. kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.

Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba,
8. mfumo wa umeme,
9. mfumo wa sauti,
10. Eneo la kukimbilia wanariadha,
11. chumba cha VAR,
12. lifti mbili mpya,
13. mfumo wa taa,
14. mfumo wa maji taka,
15. mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu

HADI SASA HAKUNA KILICHOFANYIKA
 
Waliambiwa wale kulinganq na urefu wa kamba 😂😂😂 kwahy tusishangae mambo kama hayo
 
Inawezekana ilikuwa ni ahadi ya Serikali lakini, fedha hazikutolewa.

Mara kadhaa Serikali huwa inatenga fedha lakini hazitolewi.

Tunaweza kuwalaumu akina Mwana FA na Katibu wake Mkuu, kumbe ilikuwa ni ahadi hewa
 
Mkuu billion 30 ziliishia kwenye ukarabati wa vyoo,.

Na sasa tunasubiri bajeti ipitishwe na katibu mkuu, Hivi punde tutaanza ukarabati maana tayari mkandarasi tumempata na matarajio yetu hadi kufikia mwenzi october uwanja uanze kutumika.

My country. 😊
Au wewe ndiye mwanakamati wa matengenezo!😄
 
Back
Top Bottom