Mwana FA: Tulilipwa Bilioni mbili na milioni mia moja hamsini na tano baada ya kushinda kesi

Mwana FA: Tulilipwa Bilioni mbili na milioni mia moja hamsini na tano baada ya kushinda kesi

wachache wanajitambua, P-Funk alilamba ile 100m peke yake na kumchinjia mbali Prof-J kuhusu beat ya Nikusaidieje kutumika kwenye Katwe
Proffesa Jay kipindi kile alipokuwa anatumia biti za Majani kupiga show alikuwa anamlipa kiasi gani Majani?

Tena Majani yupo fair sana kama tungekuwa na sheria kama za mbele Majani leo hii angekuwa ni bilionea.
 
Ku “attach” au “kufreez “ account
Kwa lugha ya kisheria ni attachment of Judgment debtor account au kwa neno lingine inaitwa garnishee order, mahakama inamuamuru third party (bank) kumzuia mdaiwa (judgment debtor) kutoa pesa kwenye account yake badala yake benki inaamuriwa kumlipa mdai (decree holder) deni lake kutoka kwenye akaunti husika.
 
Bila shaka ni "Mwana-FA" na siyo ''Mwanafa" .

Anyway, huyu Mwana-FA ana falsafa nzuri sana kimaisha. Bila shaka ugumu wa maisha ulimpa akili nyingi sana.

Muheza wamepata mbunge sahihi. Kura nyingi kwa Mwana-FA.
Nakumbuka 2015 kwenye kampeni za CCM, Rais Magufuli alikuwa anamwita "Bwana FA" [emoji16][emoji16][emoji23]
 
Haya majamaa yana akili nyingi sana,wamekausha kwa kipindi chote hicho sasa hv ndio wanafunguka mpunga waliouingiza baada ya kuutumia wote,nadhani walijua fika kuwa wangeropoka kipindi kile mizinga ingekuwa mingi sana kutoka kwa ndugu na jamaa
Waliogopa kutekwa au kuvamiwa.
 
Kama walifanya hivyo basi ni jambo zuri.

Maproducer wana hali mbaya,Zest yule katengeneza karibia 80% ya hit songs za Aslay office yake ipo Tabata karibu na Remnant school,ila ukimtizama kachoka yaani sasa hivi ukimnunulia mzinga wa konyagi ana kunyongea biti.

C9 nimetizama intvw yake na wasafi,sasa hivi ameamua afungue duka lake la mitumba,uproducer haumlipi kafikia hatua ya kuzuia nyimbo za Isha Mashauzi na wasanii wengine.
Khalfan Majani Alilalamikia Sana Mambo Hayo.....
 
Msanii Hamis Mwinjuma aka mwanafa ameweka wazi kiasi cha pesa walicholipwa na kampuni ya simu iliyokuwa ikitumia nyimbo zao bila ridhaa.

Msanii Mwanafa na AY waliishitaki kampeni hiyo ya simu mahakamani mwaka 2011 na baada ya miaka 7 ya purukushani za mahakamani hatimaye mwaka 2018 walifanikiwa kupata amri ya mahakama ya kuattach akaunti ya benki ya kampuni hiyo na kufanikiwa kupata kiasi cha pesa 2.185 bilioni.

Mwanafa akihojiwa na mtangazaji Salama Jabir amesema pesa hizo zilitolewa kwenye akaunti ya benki ya kampuni hiyo ya simu na kuingizwa kwenye akaunti ya mwanasheria wao kabla ya wao kugawana fedha hizo.

Mwanafa amesema alitumia sehemu ya fedha hizo kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo perfume yake ya falsafa.

Mwanafa hakusita kuelezea historia ya maisha yake jinsi alivyolelewa kwa tabu kwa maisha ya kutanga tanga. Mwanafa amesimulia kuwa mara baada ya mama yake kupata ujauzito wake kulitokea sintofahamu kati mama yake na baba yake. Hali hiyo ilipelekea babu yake mzaa baba kuingilia kati na kumchukua mama yake na mwanafa na kuishi naye mpaka alipojifungua. Baada ya kujifungua babu yake alimrudisha shule mama yake na hivyo yeye (babu mzaa baba) kuendelea kulea kichanga hicho akishirikiana na bibi yake mwanafa wa kufikia (maana bibi yake mzaa baba alikuwa ameshatengana na babu yake hivyo babu yake akaoa mke mwingine).

Mwanafa akiwa na miaka 3 babu yake mzaa baba alifariki hivyo mwanafa akalazimika kwenda kuishi na mama yake aliyekuwa ameolewa jijini Dar es salaam. Akiwa na umri wa miaka 5 mama yake aliachika na kuamua kuolewa tena huku safari hii akiwa na watoto wawili mwanafa na mtoto mwingine mdogo. Kwa kuogopa kwenda kwenye ndoa na mzigo mkubwa ilibidi mwanafa arudishwa Muheza Tanga safari hii kwa Bibi yake mzaa baba na si bibi wa kufikia tena. Ameishi na kusoma muheza na sasa ni mgombea ubunge wa Jimbo la Muheza kupitia CCM.

Sikiliza zaidi

😍😍
 
Sidhani Kama harmy B alitoka mtupu kwa jinsi alivyoshibana na hao jamaa .

Unaweza kuwa aliwauzia biti Ila jamaa watakuwa walitoa Muungwana tu maana Ni mchizi wao sana .

Kwenye huo mpungu hata msando kaonja hela
Hiyo pesa hakuambuliwa kitu iligawana kati yake, Ay, na mr. albert almaarufu kama (ksado)
 
Fedha hatari mkuu inakatika kama upepo!! Bil 1.2 imeishia kutengeneza FynByFalsafa kwa wakala?
Kuna siri nyingi sana kwenye pesa hawezi kuziweka wazi. Zile hela ziligawanywa kwa watu wengi. Hata hivyo hawezi kufirisika kirahisi kama Idrissa. Mwana-FA ana akili kubwa sana. Nyota yake inazidi kung'ara tu na sasa anaingia mjengoni
 
Haya majamaa yana akili nyingi sana,wamekausha kwa kipindi chote hicho sasa hv ndio wanafunguka mpunga waliouingiza baada ya kuutumia wote,nadhani walijua fika kuwa wangeropoka kipindi kile mizinga ingekuwa mingi sana kutoka kwa ndugu na jamaa
Mbona issue inajulikana muda tu mkuu..tena kesi ilikua mahakaman..haikua Siri hela waliyolipwa

Sent from my SM-G920P using JamiiForums mobile app
 
Kwa lugha ya kisheria ni attachment of Judgment debtor account au kwa neno lingine inaitwa garnishee order, mahakama inamuamuru third party (bank) kumzuia mdaiwa (judgment debtor) kutoa pesa kwenye account yake badala yake benki inaamuriwa kumlipa mdai (decree holder) deni lake kutoka kwenye akaunti husika.
Thanks naona jargon za kisheria hizo
 
Kwa mimi ngoma pekee ya FA niliyoielewa ni ile ya "Mimi na Mabinti damu damu" baada ya hapo naona kama alijiwekea rekodi ambayo baadae ameshindwa tena kuifikia.
 
Kuna siri nyingi sana kwenye pesa hawezi kuziweka wazi. Zile hela ziligawanywa kwa watu wengi. Hata hivyo hawezi kufirisika kirahisi kama Idrissa. Mwana-FA ana akili kubwa sana. Nyota yake inazidi kung'ara tu na sasa anaingia mjengoni
Nakubaliana na wewe kwenye akili kubwa,kwenda bungeni ni probability maana anayepambana naye ni mbunge aliyemaliza muda 2020(Chadema).
 
Back
Top Bottom