Mimba za utotoni ni Janga la Taifa. Idadi ya watoto wanaokatisha masomo kwasababu hii inazidi kuongezeka mara dufu. Athari ya janga hili ni zaidi ya hawa mabinti kukosa elimu. Mabinti wetu hawa hata wakipata nafasi ya kurudi tena shule zaidi ya 80% hawawezi kumudu kwasababu ya aina ya familia wanazotoka, jamii inayowazunguka na walimu wetu walivyoandaliwa.
Suluhisho la hili tatizo ni zaidi ya kurudi shule, suluhisho ni kushughulikia sababu za tatizo na kuangalia ni wapi tumekosea kama taifa na kujisahihisha. Tulipokosea sio kutokuruhusu hawa mabinti kuendelea na shule, tulipokosea ni pengine....tupasahihishe hapo. Tusishabikie tu kauli ya Rais kama ndiyo sababu au suluhisho la mimba za utotoni.
Mimi kama ningekua ni mwalimu wa rika la hawa watoto hakika nisingependa kufundisha darasa moja lenye mchanganyiko wa binti wa miaka 12 na mama wa miaka 12 kwasababu handling yao ni tofauti. Walimu wetu wameandaliwa kwaajili ya kufundisha watoto, hawa mabinti zetu wanaokuwa mama ktk umri mdogo wanahitaji waalim maalum. Lakini mimi pia kama mzazi nisingependa binti yangu wa miaka 12 kufundishwa darasa moja na binti mwingine wa miaka 12 ambaye ameshakuawa mama kwasababu sitaki aone kama hilo ni jambo la kawaida. Naamin hata mabinti wengine waliokwisha zaa na wanasoma/walasoma shule binafsi hawajulikani kinaga ubaga kama wana watoto.
Sababu kubwa ya mimba za utotoni sio kubakwa, takwimu zinaonyesha 80% wanafanya ngono kwa hiari. Ninaamini wengi walioepuka ngono na mimba za utotoni ni kwasababu ya woga/hofu ya Mungu na wazazi. Woga na hofu ndio sababu kubwa ya mabinti wengine kutokujiingiza ktk ngono na kutokupata mimba, elimu ya uzazi, mazingira bora na sababu nyingine vinafuatia kwa uzito mdogo. Kwahivyo mabinti zetu wanapaswa kuogopa, wanapaswa kuwa na hofu ya ngono na mimba kwa ujumla, kama hawana hofu na woga hata ifanyike nini haitasaidia. Hawa mabinti tunaowatetea hawana woga kabisa kabisa na ngono, hawaogopi wababa wala wababu!
Kama tunavyopaza sauti kuwatetea warudi shule, vivyo hivyo tupaze sauti kuwakemea dhidi ya ngono ktk umri mdogo, tuwatie woga, tuwatie hofu, waache tamaa. Wao wakikataa wanaume hawana nguvu dhidi yao! Tunavyoendelea kumkanya Rais dhidi yao, tunavyoendelea kuwakanya wanaume dhidi yao tunawafanya wajione vulnerable wakati nguvu ya kukataa na kutokupata mimba iko ndani yao na si kwa kundi lingine lolote!