Uchaguzi 2020 Mwana JamiiForums Happiness Essau, achukua fomu ya Ubunge Jimbo la Bukoba

Acha propaganda mkuu.kwani mashart ya kutia nia ubunge au udiwani yanasemaje?....

Hii ndiyo democrasia.MTU kuwa msanii comedian sioni kama kikwazo cha kushindwa kuwatumikia wananchi.mifano IPO hai.

Waache wakatie nia.kanuni na taratibu zitafuatwa ili kupata mgombea mwenye dhamira ya kweli kwenda kuwatetea wananchi..hata ww.nafasi unayo tatizo hujiamini tu.
 
Nia ya wewe kusema uongo ni ipi hasa? Jamii Forums haina Afisa Habari wala Happiness si mfanyakazi wa JF
Mkuu, hebu msome Mhusika hapa halafu tupatie ufafanuzi:

Happiness Essau
Verified Member

Aug 9, 2016 166 225

Jul 26, 2017
NGOGO CHINAVACH said:
Leo tarehe 26.07.2017 mbunge alikuwa na mkutano maeneo ya soko kuu mbona hatupati mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu, mimi ni Afisa Mawasiliano wa Jamii Media sio wa Mbunge. Taarifa ya mkutano ataleta hapa Mbunge au Katibu wa Mbunge. Hili ni jukwaa la wanaBukoba wote na sehemu sahihi kwa ofisi ya Mbunge, Halmashauri na taasisi nyingine kuwasilisha taarifa zao kwa wananchi. Aidha, nimepata picha chache za mkutano huo;
 
 
 
Roving Journalist, Ok noted

Chama kinatiwa najisi cha mapinduzi

Chama kimegeuzwa sehemu ya kuonyeshea maigizo
Acha kudharau watu wewe, fikiria mtu mpaka apoteze muda aingie Jf awe member unaona ni mtu wa kawaida??
Kina Msukuma Kibajaji walikuwa wabunge mbona huwasemi wanao tetea bangi??
Walitumwa kutetea bangi bungeni na CCM??
Chunguza jirani zako wangapi ni member humu??
Huyo binti anastahili pongezi kujitokeza kugombea ubunge!!
Ingawa ni kwa lichama chakavu nampa kongole apambane wenzake kabla hawajakutana na CHIEF KAJUNA!!
 

Happiness alikuwa Afisa Habari wa Jimbo la Bukoba Mjini katika Mradi wa Tushirikishane uliokuwa ukiendeshwa na JamiiForums mwaka 2017.

Hakuwa mwajiriwa wa JamiiForums bali aliajiriwa na mradi na kazi yake iliisha mwisho wa mradi.

Zaidi, soma Ajira ya muda katika Jamii Media - Afisa Mawasiliano (9)
 
Soma Katiba ya nchi vizuri.
Ulichokiandika ni kinyuma cha katiba ya Jamhuri ya Tanzania (haki ya kuchagua na kuchaguliwa)

Halafu kutia nia haina maana ya kuchaguliwa kuwa Mbunge. Waache wajitokeze kwa wingi ili chama kipate fedha za kutosha kupitia ada ya fomu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…