October man
JF-Expert Member
- Nov 23, 2017
- 3,635
- 5,012
Baada ya majumuisho yote hayo bado nabaki palepale umasikini ndio adui wangu mkubwa kuliko wote.
Huko huko ndumbwi ndipo alipokuwa anaishiSorry ni maeneo ya jogoo ndumbwi?? Maana kuna mkaka alijinyonga juz juz. Hayo maelezo ni kama yale ambayo nliyaskia pale
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu marehemu hata mimi alishawahi kunijia pm nikampa mchango wa mawazo ambao alijaribu kufanya alichofanya ingawa response kwa baadhi ya watu wenye nyadhifa zao ilikuwa ni ndogo sana.Hapo ninachokiona ni stress ndio zitakuwa zimemfikisha kwenye hatima ya uhai wake,ukiangalia nyuzi alizokuwa akiziandika ni za kukata tamaa ya kuishi karibu zote.Kwa tuliobaki duniani,tusitumie nguvu sana kuzitumainia akili zetu wenyewe hasa tunapokutana na mambo magumu kuliko tunavyoweza,Mungu yupo na tukimtumainia yeye atatuonyesha njia ya kutokea...Ndugu huna cha kujilaumu! Tena Ahsante kwa kuwa na Utu wa kumsaidia mtu kwa kuwa ana shida, bila ya kujuana naye kwa undani. Binafsi huyu marehemu alinishirikisha baadhi ya masuala na nilisaidia nilivyoona itamsaidia. Kati ya ujumbe wa mwisho nafikiri ni Desemba, aliniarifu wamempatia vyeti vyake na ameahidiwa uwezekano wa kupata kazi kama si Januari ni Februari.
Kinachoniacha hoi ni leo hii kujua kuwa sikuwa peke yangu niliyemsaidia, na ambacho sielewi zaidi ni kwa vipi mtu anayepewa aina mbalimbali ya misaada iwe ni mawazo, fedha, connections, n.k. ,tena na watu baki bado anakuwa na hali ya kukata tamaa mpaka kujitoa uhai wake?
Hatuwezi kupata majibu, ila bado inanishangaza.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi mkuu, kwa Hali ya kawaida kabisa, ya kawaida kabisa , Kuna mtu anaweza akawa yuko vyema alafu akaingia kwenye utapeli ?? Shida..shida hizo mkuu ,Changamoto ni namna gani ya kuthibitisha yupi tapeli yupi mwenye shida ya kweli. Kumbuka Kuna watu wametapeliwa humu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaha usichekeshe watu, tuko kwenye majonziHii imenisaidia sana mimi, kuna watu walikuwa wananizodoa eti unasema una hali ngumu ila kutwa kiguu na njia ila imenisaidia sana, ningebakia palepale huenda hata mimi ningekuwa marehemu....hata kama si kwa kujinyonga yangeniua hata magonjwa maana hata yenyewe hayakuwa nyuma kunishambulia, yaani kama nina ukimwi vile likitoka hili linaingia hili
Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha kweli ni kitu cha kupita; huyu ndugu niliwahi kuwasiliana naye siku za nyuma kupitia Inbox. Nikamtumia mzigo fulani kwa Moneygram lakini akasumbuliwa sana kuupokea mwishowe baada ya zaidi ya mwezi hivi ukanirudia mwenyewe.Mshana Jr, Natetemeka siamini ninachokisoma..
Mungu pekee anajua ninavojisikia juu ya Robin.
Karibia mwezi mzima namtafuta nijue progress yake then kuna kitu nimeandaa incase alipo( maana lastly alinambia yuko Dar kwa mama mmoja ) hajaanza kuona mwanga nimchukue tuendelee na michakato tuliyoanza anione live nikiendelea nayo apate tumaini.
Baada ya kuwasiliana na kaka mwingine tukagusia issue ya Robin Friday akanambia amefungiwa simu, nikapotezea issue nikijiambia nitamtafuta tena kwa pm Jf au nipige simu mtwara wakanitafutie mawasiliano kwao.
Sijui niandike nini Mimi.
Nina deni kubwa kwa Robin.
Process ya kushughulikia suala lake kuanzia tamisemi mpaka wizarani imekuwa too slow..
Aaahhhh Mungu wangu na Baba yangu!!!
Wacha nishukuru tu sina naweza sema kwa usahihi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ulijitahidi sana mkuu japo msaada wako haukuweza kumfikia mlengwa. Dhamira yako ni safi na thawabu hakika utapata. Apumzike kwa amani Marehemu...Maisha kweli ni kitu cha kupita; huyu ndugu niliwahi kuwasiliana naye siku za nyuma kupitia Inbox. Nikamtumia mzigo fulani kwa Moneygram lakini akasumbuliwa sana kuupokea mwishowe baada ya zaidi ya mwezi hivi ukanirudia mwenyewe.
Nasikitika kuwa niliplani kutumia tena kwa njia nyingine lakini baadaye tukakosa mawasiliano hadi leo ninaposoma post hii.
View attachment 1369240
Kwa bahati mbaya sikuwahi kusoma threads zake hata siku moja zaidi ya PM tu.
Uko sahihi. JF is full of bullies. Yaani hakuna ubinadamu kabisa. Tabia hizi za kutukanana, kukejeliana na kudogoshana zingekuwa zinaishia huko kwenye jukwaa la siasa ingekuwa poa sana. Hawa wanaojitoa mhanga mpaka kuja hapa kuomba msaada mods itabidi waanze kuwa macho na kufuta comments zote zenye ukakasi na kuvunja moyo. Huduma za mambo yanayohusu ubongo bado sana hapa kwetu na mpaka mtu uokote makopo ndiyo watu wanajua kuwa kweli kichwani hauko sawa. Magonjwa kama depression na sijui bipolar utaambiwa kuwa hayo ni magonjwa ya wazungu na matajiri. Na kutukanwa juu...Sad !!!JF usipokua na Roho ngumu unaweza ukajiua
Mimi nawalaumu mods. Maxence na wengine. Sawa JF ni platform ilitotengenezwa kwa nia nzuri. Ni sehemu ambayo watu wamepewa uhuru wa kujieleza huku ID zao zikibaki anonymous. Dhamira ilikua ni kuendeleza na kukomaza demokrasia.
Shida inakuja hapa mods wanashindwa ku control contents or hawataki na kuamua kupuuzia ilimradi ku maintain "traffik" Kwenye hii site. JF imetoka kwenye motto yao ya "home of great thinkers" imekua "home of bullies".
Humu ndani kuna makundi ya watu wanakua bullied. Celebrities, politicians,Single mothers, wanawake ambao sio bikra, depressed people wanaokuja kuomba ushauri kwa ku take advantage ya anonymity ya JF kwamba hamna anaewajua humu personally hivyo anaweza kueleza shida zake bila fedheha ya aina yoyote. Cha kushangaza ni kua nyuzi na replies za kebehi na bullying mods hawazitilii maanani wao wanakomaa na "matusi tu". Acheni hizo.
I blame his death on moderators. Sijui ku tag ila ningewatag wote. Acheni double standards, hypocrisy na misogynistic behaviour. Jifunzeni kwa Zuckerberg yeye anajitahidi sites zake ziwe bully free.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mmh hebu mwacheni mdogo wangu, marehemu amesaidiwa sana na wadau wa hapa na walionyesha kumjali lakini bado amejiua, huyu angetoa msaada gani wa ajabu ambao ungefuta hizo fikra za kujiua
Nilirespond ile pm baada ya muda kidogo kupita..lakini hakunijibu Tena.
Ooh maskini bas ndo yeye,alikua anasaidiwa na huyo mama alipewa hifadhi na alikua anasoma... May his soul rest in eternal peace[emoji120]
Mkuu ushauri na kumtia moyo mtu sio Kitu Cha maana?Honestly Hakuna chochote cha maana ulichokua ukimpa, acha unafki
sana
Sijui nimeongea kisukuma. Kuna sehemu nimeonesha kushangaa?
Mi nimemwambia inavowezekana na nikampa mfano ilivokuwa kwangu afu wewe unanambia nashangaa. Kutoa ushuhuda ni kushangaa?
Usichukulie siasa too personal, unaowapigania huko probably muda huu wamekaa wanapiga bia/mvinyo na mahasimu wao.
Siasa is just a game!
Pole sana, Usiwe unapenda chukulia siasa too personal aisee!
Zile mishe nilishapata ufumbuzi wake na nikaendelea nazo. Sorry sikukupa feedback
Uwage flexible sisi wengine issue za political attacks hazitumaliziagi utu yaani tunaziachaga kwenye Uzi husika na ukija Uzi mwingine inakuwa issue nyingine, ivo tu.
Sent using Jamii Forums mobile app