lunatoc
JF-Expert Member
- Aug 16, 2017
- 2,911
- 5,479
Mkuu mbona umeficha hizo IDs ungeweka tuwajueHapa kweli kuna majuto. Hizi comments wakati akihitaji msaada zinasikitisha. RIP!!!
View attachment 1369645
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu mbona umeficha hizo IDs ungeweka tuwajueHapa kweli kuna majuto. Hizi comments wakati akihitaji msaada zinasikitisha. RIP!!!
View attachment 1369645
Kuna watu wapumbavu sana,yaani mnafanikiwa kuiba zaidi ya billion alafu mnaendelea kuranda randa hapo hapo kwenye mji ambao mmepiga tukio!!!yani ingekua ni mm ningekua huko kigoma ndani ndani au nshavuka boda mda.
Yaani dah...yaani mtu u comment hivyo halafu mtu afe...
Nimesikitika sana...sana...
Kuna watu hii Jf ni kimbilio la kupoza moyo kwa kutoa yaliyo moyoni....
Lakini kuna viumbe humu ni wanyama... ..humu ni.kama sehemu ya kutema nyongo zao..
Hata kama kuna mwelekeo wa ukweli..wao watasimama kidete kukejeli..matusi..na dhihaka za kumkatisha mtu tamaa..kabisa azidi kujiona dhalili !
Hata wale wachache wenye moyo ya kutoa basi pia watatumia nguvu nyingi.. kuwavunja moyo...kisa eti aliwahi saidia mtu akamtapeli!
Tuache unafiki ...
Akifikwa mtu ndio wanajitokeza kusikitika..hizo kauli zitawashitaki na nafsi zenu zitawahukumu ..mngali hai mdhalilike ... ... vile vile!
Kama huna au hutaki ni bora kunyamaza.. ... mnamsema mtu vibaya namna ile?
Looh!
Kwa hali inavyokwenda...tutegemee mengi kujitokeza!
Imefikia hadi humu pia mtu aogope kusema la moyoni..kisa wanaharamu fulani..watafufuka na kumshambulia!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye imani za dini kuna wanafki wengi. Wengine 24/7 wapo nyumba za ibada . Yaani wapo kimaslahiHakuna watu wenye roho mbaya kama hao wanaojiita wafia Dini , Ni Bora uende bar kwa wanywa pombe wako royal kuliko hiyo mi-minguruwe inayojifanya mitoto ya Mungu ... .
Ukisoma threads za marehemu huyu Yehodaya amechangia kiasi kikubwa kumuua.... Pitia Uzi wa marehemu akiomba Ada utaliona hili lishetani likijitanabaisha bila kificho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ubinadamu hakuna tena...Hapa kweli kuna majuto. Hizi comments wakati akihitaji msaada zinasikitisha. RIP!!!
View attachment 1369645
CC JamiiForums Maxence MeloNa kwa masikitiko makubwa hizo comment mara nyingi hua zinaachwa , sasa sijajua maana ya mtu ameajiriwa anajiita eti content nini sijui, hizo kazi ni za bure tu wanafanya, thread kama hizo hawazipi umuhimu, ambazo mtu yuko kwenye hatari ya kufanya suicide
Sent using Jamii Forums mobile app
KabisaSana waache kutoa lawama.
Kuna watu mpaka muda huu hawawezi kushika simu zao kwa presha ya hili jambo sababau walikuwa ni msaada kwa kijana sasa taarifa kama hizi zinashtua sana.
Alikuwa ndani ya mikono salama humu ndani, pengine kuna mengine ya ndani hatuyajuo yaliyokuwa yanamtatiza.
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanaojiua wanakuwa hawako kweli hali ya kawaida kimawazo. Wewe unasema hivyo kwa sababu uko kwenye hali ya kawaida. Ni kama mtu asiye na homa anayemcheka mtu mwenye homa aliyejifunika blanketi wakati kuna joto kwa sababu ya baridi. La muhimu ni kujichunga na kuomba Mungu tusiwe kwenye hali hiyo. Nikupe mfano. Miaka ya nyuma kuna dada mmoja alijiua kwa kunywa sumu. Siku ya mazishi wakati wanachimba kaburi, jamaa mmoja akawa anajeli na kusema tuchimbe shimo refu kabisa ili asipate nafasi ya kurudi kwani amekufa kwa ujinga wake. Baada ya mwaka yule jamaa naye akafa kwa kunywa sumu.Kujiua ni kufa kizembe sana,mm siwezi kujiua,bila changamoto hakuna maisha,
Kuna wakati mtu anakuwa kwenye wakati mgumu sana mpaka anakosa majibu anaangukia kujiua,
Sent using Jamii Forums mobile app
Robin apumnzike mahali salama inasikitisha mno. Mi pia ni nimewasiliana sana PM na hilo la ulalamishi ni kweli tupu. Na aliwahi niambia kuwa mnawasiliana, wale wote waliomsaidia kwa hali na mali Mungu awabariki.Marehemu mm nilikua nachat naye sana kwanza ni mlalamishi kwa kila kitu..then alikua na hasira! Apumzike tu sasa
Kisaikolojia Kuna Kinaitwa Resilience Capability yaani uwezo wa kuhimili changamoto ... Kuna mtu akituanwa anapigana wakati mwingine akitukanwa ndio kwanza anainuka zake anaenda zake bila ugomvi ... Mwingine akaipitia misuko suko kiuchumi anaona sawa kuwa maisha ni kupanda na kushuka ipo siku itakuwa poa ila mwingine wa kesi hiyo hiyo anaweza kuwa mlevi...
Hivyo Basi binadamu hatuko sawa kwenye kuhimili changamoto , Ni kujua namna ya kuwapa "misaada Jamii" wenzetu walio katika changamoto waweze kuhimili changamoto huku tatizo husika likiwa linashughulikiwa .... Hizi Bullies hazipo tu mitandaoni hata watoto wetu Shuleni huko wanakumbana nazo saaaaaaaaaaana Kama wazazi tusisahau pia huko ... Tunapofanya kuwakagua watoto tusioshie tu kwenye performance fanya uchunguzi wa Kama Yuko Bullied Shuleni ... Shulen Kuna watoto wa kila dizaini Kama wati wa kila dizaini walioko mitandaoni....
Sent using Jamii Forums mobile app
Robin apumnzike mahali salama inasikitisha mno. Mi pia ni nimewasiliana sana PM na hilo la ulalamishi ni kweli tupu. Na aliwahi niambia kuwa mnawasiliana, wale wote waliomsaidia kwa hali na mali Mungu awabariki.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huo msaada wa kimawazo na zaidi ya huo alipewa basi tu ni vile alishaji-tune kwenye wazo la kujitoa uhai. Kama ulikua mfuatiliaji wa nyuzi zake utakumbuka attempt za kutaka kutoa uhai na zote ilishindikana.Hizo ni forms za depression na bipolar iliyokomaa , alijitaji pia msaada wa kimawazo
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo kubwa ni kwamba kuna watu wengi wanaanzisha thread za kuomba msaada au kutishia kujiua wakati ni matapeli au wanatania. Kwa mfano huyu marehemu alipoanzisha thread moja alikuwa anaulizia kama utani anataka kujiua na aambiwe njia nzuri. Kwa mtu amabye hakuwa anafuatilia ile thread kwa kusoma yote, au hajasoma thread zake nyingine alizoanzisha moja kwa moja angechukulia kama ni utani.Kupitia huu mkasa wa ndugu yetu aliyetangulia mbele ya haki kuna haja ya moderators kufanya namna ya ku deal na bullies
Bullies zinaharibu saikolojia ya mtu, mtu anakuwa wa tofauti kabisa, mods please lifanyieni kazi hili
Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha kweli ni kitu cha kupita; huyu ndugu niliwahi kuwasiliana naye siku za nyuma kupitia Inbox. Nikamtumia mzigo fulani kwa Moneygram lakini akasumbuliwa sana kuupokea mwishowe baada ya zaidi ya mwezi hivi ukanirudia mwenyewe.
Nasikitika kuwa niliplani kutumia tena kwa njia nyingine lakini baadaye tukakosa mawasiliano hadi leo ninaposoma post hii.
View attachment 1369240
Kwa bahati mbaya sikuwahi kusoma threads zake hata siku moja zaidi ya PM tu.
Nadhani Roho ya mauti ilimvaa.
Roho ya mauti ikishakuja hayo mawazo yote huwa hayapo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Marehemu mm nilikua nachat naye sana kwanza ni mlalamishi kwa kila kitu..then alikua na hasira! Apumzike tu sasa