TANZIA Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia

Jifunze kwenye maisha usidharau jambo
Nimeumia Sana.
Nimekumbuka alishawahi nipm sikujua Kama ni mpauko..kumbe alikuwa akitumia jina la miguu ya kuku.
Nilimjibu baada ya mwezi kupita lakini hakunijibu Tena.
Na Mimi akili ya kufwatilia japo posts zake Sikuwa nayo..laiti ningejua Kama miguu ya kuku ndiye huyo mpauko basi ningefanya bidii zaidi kumtafuta japo kuongea naye.
Mungu nirehemu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pm zko ndo huwa sijibu..kun kipindi uliniuliza mishe fulan nikajipinda kuandika wee hukujibu....nikahesabia
2.unapendaga sana kuniattack jukwaa za siasa.. Uliwahi niumiza sana sana ww...nikasem nikianza gombana na mwanamke mwenzangu itakuwa sio poa...sijawah kujibu qoute yako ndo nimejibu leo!
Usichukulie siasa too personal, unaowapigania huko probably muda huu wamekaa wanapiga bia/mvinyo na mahasimu wao.

Siasa is just a game!
 
Better umueleze pia anaweza gain kitu.
Siasa si ugomvi japo watu wengine huhisi kutofautiana kisiasa ni tatizo.
Wanadamu tunatofautiana mengi lakini haituondolei utu wetu Wa ndani kwa yoyote.

Utakapomkuta Magufuli na Mbowe wanagonga mvinyo pamoja wakati wewe ulikutana na mwanaccm ukaacha mpa msaada kwakuwa wewe mwanachadema sijui utajisikiaje hapo!


Tuna safari bado kuelimishana juu ya itikadi hizi zisizo za kudumu.
Usichukulie siasa too personal, unaowapigania huko probably muda huu wamekaa wanapiga bia/mvinyo na mahasimu wao.

Siasa is just a game!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
r
Hizi nyuzi zake zilikuwa na viashiria vya kujinyonga kwanini Afande yule wa Tabora hajamkamata? unique vee,

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu afande aanze kuingia Mitandaoni Kutafta watu wanaoandika kujinyonga?

Ni km yule kamanda sijui wa mkoa gani aliyesema Ukiwaza tu kujinyonga watakukamata....


Cha msingi hapa ni kama unaweza kua chanzo cha kumfanya asijinyonge basi kua chanzo kweli....

Ukichelewa hapo ndio km haya ya ndugu yetu huyuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani kwa kuingilia ila mimi nimemsoma mane kuwa ulikuwa unamuattack yeye, suala la kutofautiana kwenye hoja lipo popote hata MMU tunatofautiana kwenye uzi huu tukienda uzi mwingine tunataniana kama kawaida. Shida ni pale mtu anapoanza kuattack mtu binafsi /I'd binafsi badala ya kuattack hoja. Nadhani ulimkwaza hapo, comment yako uliyomjibu mwanzo ilitosha na ni vyema ukamuomba radhi tu kama ni kweli ulifanya hivyo
Better umueleze pia anaweza gain kitu.
Siasa si ugomvi japo watu wengine huhisi kutofautiana kisiasa ni tatizo.
Wanadamu tunatofautiana mengi lakini haituondolei utu wetu Wa ndani kwa yoyote.

Utakapomkuta Magufuli na Mbowe wanagonga mvinyo pamoja wakati wewe ulikutana na mwanaccm ukaacha mpa msaada kwakuwa wewe mwanachadema sijui utajisikiaje hapo!


Tuna safari bado kuelimishana juu ya itikadi hizi zisizo za kudumu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fight for Depression,
Fight for Anxiety,
Love one another,
Help those in need.


 
Wana JamiiForums tupo kwaajili ya matani mengi na kebehi za hapa na pale, wachache ndo wanazingatia maumivu ya mtu na kutafuta namna ya kupata suluhisho.

Utakuta mtu Kama Miguu ya kuku anashida kubwa na anaandika kwa hisia Kali lakini watu wapo kwenye matani na kejeli za maneno mabaya na ya mikato, Yani hawajali chochote kile,Tena ukute ndo wanazidi kumtania kwa kumwambie aende kwa mganga wa kienyeji.

Hii si sahihi kabisa tunauana sisi wenyewe Kisha tunakuja kuandika R. I. P ishara ya kuguswa kumbe ni wauaji wakubwa, Jamani tufikie hatua tuthaminiane Kama ni matani Basi yabakie mahala pake na Mambo ya kuzingatia pia tuyape uzito mkubwa.

Huyu Miguu ya kuku alihitaji ushauri na maneno ya faraja Sana na pengine alihitaji kuwekwa sehemu ya jamii ili dhana mbaya imtoke na ajihisi mtu katika watu.

Post zake karibia zote zilikuwa za mashaka mno, alikuwa amekata tamaa na hata alipokuwa anaposti watu hatukuzingatia namna ya kutoa majibu mazuri, Sana Sana majibu yetu yalikuwa ya mkato tu, 'NENDA HOSPITALI ZA BINAFSI HUKO' Sasa haya ndo majibu ambayo yanastahili kutolewa kwa mtu mwenye uhitaji kweli?

Haya majibu na majibu mengine kwakweli hayakuwa ya kuridhisha.

Tupendane, tushauriane tupeane faraja na Kisha tusherekee maisha pamoja.

Apumzike panapostahili Miguu ya kuku.
Amina.

Ahsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wote mlioweza kujitoa Kwa chochote Kwa huyu ndugu mungu awazidishie popote mlipotoa au kupunguza,ILA NAXIDI KUJIFUNZA HAKUNA SEHEMU IMEJAA WANAFIKI KAMA JF...
NB:MAREHEMU KACHUKUA MAAMUZI MAGUMU SANA SANA NA NAMUOMBEA APUMZIKE ANAPOSTAHILI,TULIOBAKI MWENYEZI MUNGU ATUPE MWISHO MWEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kale katabia mfano unaenda kwenye msiba unakuta mtu analia huku anahadithia "marehemu alikuja kwangu kunianzima nguo nikamwambia njoo kesho leo amefariki Siamini"
Unabaki kujiuliza huyu ameguswa kweli na msiba au ndio nionekane nilikuwa kwenye harakati za kutoa msaada.
Umeongea ukweli mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mahali nimekualika kaka
Ndugu huna cha kujilaumu! Tena Ahsante kwa kuwa na Utu wa kumsaidia mtu kwa kuwa ana shida, bila ya kujuana naye kwa undani. Binafsi huyu marehemu alinishirikisha baadhi ya masuala na nilisaidia nilivyoona itamsaidia. Kati ya ujumbe wa mwisho nafikiri ni Desemba, aliniarifu wamempatia vyeti vyake na ameahidiwa uwezekano wa kupata kazi kama si Januari ni Februari.
Kinachoniacha hoi ni leo hii kujua kuwa sikuwa peke yangu niliyemsaidia, na ambacho sielewi zaidi ni kwa vipi mtu anayepewa aina mbalimbali ya misaada iwe ni mawazo, fedha, connections, n.k. ,tena na watu baki bado anakuwa na hali ya kukata tamaa mpaka kujitoa uhai wake?
Hatuwezi kupata majibu, ila bado inanishangaza.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama 1.6m ilikuwa ni tatizo, kwani alishazipata.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wakati naandika hiyo post jamaa alikua bado hajatoa maelezo ya nini kiliendelea.

Pamoja na yote, ukifuatilia kwa ukaribu sana hili sakata lote limeghubikwa na umasikini mkuu. Hiyo 1.6 yenyewe imepatikana kwa vuta nkuvute, kumbuka jamaa kawatembelea waheshimiwa na watu kadhaa aliotegemea wangemsaidia akaishia kuambulia kibali cha kuchangisha michango. Hiyo peke yake ni zaidi ya stress.

Baada ya majumuisho yote hayo bado nabaki palepale umasikini ndio adui wangu mkubwa kuliko wote.
 
Back
Top Bottom