Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,403
- 12,775
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
R I PNi habari za kusikitisha kwa familia ya JamiiForums kwa ujumla wake.
Inadaiwa marehemu Dena Amsi amefariki jana baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Taarifa za kina juu ya nini kilitokea na msiba upo wapi zitafuatia.
Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na kumjalia pumziko la milele.
R.I.P Dena Amsi
Mlioko Dar mtufikishie salamu zetu za pole.... Utaratibu wa kutuma rambi rambi ukoje?Msiba upo Bunju na wanatarajia kuzika leo. RIP Dena Amsi
Tumejadili naye mambo mengi sana. Tumeshare jokes nyingi sana. Siwezi kuacha kutoa salam zangu za mwisho kwake
Jukwaa la Mahusiano na MapenziJMM ndio nani mkuu?
Mkuu kama yeye alipokuwa hai hakuweka picha yake halisi sidhani kama ni busara mtu yeyote aweke bila idhini yake.Ukitaka kujua ni ngumu ebu mkuu wewe weka picha yako halisi.
Mkuu nilitegemea utanielewa haraka lakini naona bado.Jiulize kwanini kuna "verified user" kwani wewe,mimi na yule siyo verified user?Ukifa huna tamanio.
Kama unabisha jaribu kufa uone kama jamaa hawatakufukia fasta (najua hupendi kufukiwa)
Iwekwe picha yake, hakuna atakayemshtaki kwa michango yake enzi za uhai wake.
Najiuliza siku nikifa nani atawapa taatifa maana hakuna mtu hata mmoja anayenijua.