TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

Maisha ya JF na ubaya wa fake id....
Any way apumzike kwa amani....dada yetu kipenzi....

Mkuu ni wewe tu hufahamiani na watu ndio maana unaona ubaya wa Fake ID Laiti ungelijua tunaofahamiana humu usingeona ubaya wake.

Dena alikuwa member mwenzetu wa hapa lakini ambacho hukijui alikuwa rafiki wa wengi nje ya JF na wana JF kwa wale ambao tunaaminiana.

Pumzika kwa amani mpendwa tutakukumbuka milele.
 
Mkuu ni wewe tu hufahamiani na watu ndio maana unaona ubaya wa Fake ID Laiti ungelijua tunaofahamiana humu usingeona ubaya wake.

Dena alikuwa member mwenzetu wa hapa lakini ambacho hukijui alikuwa rafiki wa wengi nje ya JF na wana JF kwa wale ambao tunaaminiana.

Pumzika kwa amani mpendwa tutakukumbuka milele.

Alaaa......kumbe.....
Basi ngoja.....
 
May his humble soul rest in godly eternal peace
 
Maisha ni hatua Dadaangu...
Namuomba Mungu wa Huruma amulike Makao yako upumzike Kwa Amani Dena Amsi... Pole kwa Wapendwa wote Tulioguswa na Msiba huu...
NA Mbarikiwe sana.
 
Huwa najiuliza,hivi ni nani anatoa taarifa za msiba wa mwana JF,huwa anajuaje kuwa huyu ni member,maana mimi nikimaliza kuchat tu nasign out.
Au huwa anaacha bila kusign out na ndiyo njia pekee mtu anaweza kuona ID japo bila password.
humu wapo watu wanajuana wengine wamekua marafiki haswaa
 
Ni habari za kusikitisha kwa familia ya JamiiForums kwa ujumla wake.

Inadaiwa marehemu Dena Amsi amefariki jana baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Taarifa za kina juu ya nini kilitokea na msiba upo wapi zitafuatia.

Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na kumjalia pumziko la milele.

R.I.P Dena Amsi
Faiza Foxy mbona hatumi RAMBIRAMBI?
 
R.I.P DENA (sory wapendwa hapo juu nimekosea kidogo)[emoji115] [emoji115] [emoji115]
 
Natamani sana angekuwa anazisoma hizi msg na condolences zenu kwakweli inauma sana lakini ndo hivyo Mungu keshatoa uamuzi wake tushukuru tu.

Kifupi huyu Dada ndio alini introduce kwenye Jamii Forums maana alikuwa akirudi home atakaa kwenye laptop akisoma na kuchangia huku akicheka saana! Ilinibidi nimsogelee kumuuliza mbona peke yake kucheka na laptop kila akirudi home na sisi kutupa muda mfupi wa maongezi naye?
Ndipo akanionesha jf na akaielekeza namna ya kujiunga.

Dena Amsi yaani jina la Bibi yake mzaa Babaake sio Id aliyoanza nayo humu, alianza na nyingine nimeisahu kwa mshtuko nilio nao juu ya msiba huu, ila ndugu mtabuzi anaweza kunisaidia kukumbusha id ya kwanza ilikuwa ipi.

Tumempumzisha leo yapata saa tisa alaasiri kwenye makaburi mapya Mbweni Dsm.
Sisi ni Wakristu tunaoamini katika uzima wa milele, hivyo tufarijike kwamba mwenzetu kapumzika katika utukufu wa Mungu Baba.
 
Back
Top Bottom