Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wa Feek,Baarakallahu Fiika/Baarakallafu Fiiki.
RIP dena Amsi,Rest in Peace
Mkuu Mulama, pole kwa msiba huu. Kwa sisi waumini wa life after life, Dena yupo na anasoma kila tunachoandika, kilichokufa na kuzikwa ni mwili, a physical body, lakini roho, a spiritual body haifi, roho ndio inayokwenda mbinguni au peponi kwenye raha ya milele au jehanum kwenye zawa la moto na mateso ya milele, na kwa majibu wa michango ya Dena Amsi humu jf, japo mimi sio Mungu, ila saa hii tunapoendelea kuchangia uzi huu, roho yake iliishapokelewa mbinguni kwa Baba saa nyingi.Natamani sana angekuwa anazisoma hizi msg na condolences zenu kwakweli inauma sana lakini ndo hivyo Mungu keshatoa uamuzi wake tushukuru tu.
Kifupi huyu Dada ndio alini introduce kwenye Jamii Forums maana alikuwa akirudi home atakaa kwenye laptop akisoma na kuchangia huku akicheka saana! Ilinibidi nimsogelee kumuuliza mbona peke yake kucheka na laptop kila akirudi home na sisi kutupa muda mfupi wa maongezi naye?
Ndipo akanionesha jf na akaielekeza namna ya kujiunga.
Dena Amsi yaani jina la Bibi yake mzaa Babaake sio Id aliyoanza nayo humu, alianza na nyingine nimeisahu kwa mshtuko nilio nao juu ya msiba huu, ila ndugu mtabuzi anaweza kunisaidia kukumbusha id ya kwanza ilikuwa ipi.
Tumempumzisha leo yapata saa tisa alaasiri kwenye makaburi mapya Mbweni Dsm.
Sisi ni Wakristu tunaoamini katika uzima wa milele, hivyo tufarijike kwamba mwenzetu kapumzika katika utukufu wa Mungu Baba.
Pole sana Mulama ,RIP dada Dena.Kwa mnaotaka kujua chanzo ni kwamba alikuwa na matatizo ya kisukari tangia akiwa Nairobi, tarehe 24/12 kisukari kilipanda kwa kasi kikachanganya na presha, akakimbizwa zahanati ya karibu lakina hali ikazidi kuwa mbaya, ikabidi apelekwe Hospital ya Rabninsia lakini baada ya muda mchache akakata roho.
Kuhusu picha,je ni ya kwake au ya bibi yake mzaa baba akiwa kijana?Natamani sana angekuwa anazisoma hizi msg na condolences zenu kwakweli inauma sana lakini ndo hivyo Mungu keshatoa uamuzi wake tushukuru tu.
Kifupi huyu Dada ndio alini introduce kwenye Jamii Forums maana alikuwa akirudi home atakaa kwenye laptop akisoma na kuchangia huku akicheka saana! Ilinibidi nimsogelee kumuuliza mbona peke yake kucheka na laptop kila akirudi home na sisi kutupa muda mfupi wa maongezi naye?
Ndipo akanionesha jf na akaielekeza namna ya kujiunga.
Dena Amsi yaani jina la Bibi yake mzaa Babaake sio Id aliyoanza nayo humu, alianza na nyingine nimeisahu kwa mshtuko nilio nao juu ya msiba huu, ila ndugu mtabuzi anaweza kunisaidia kukumbusha id ya kwanza ilikuwa ipi.
Tumempumzisha leo yapata saa tisa alaasiri kwenye makaburi mapya Mbweni Dsm.
Sisi ni Wakristu tunaoamini katika uzima wa milele, hivyo tufarijike kwamba mwenzetu kapumzika katika utukufu wa Mungu Baba.
Wote lips zenu zinafanana.hongera kumsindikiza inahuzunisha sana
Tunajuana wengi tu. Kama wewe hujuani Na yeyote basi ni tatizo lako.!IRP
ila nauliza kwamba mlimjuaje wakati wana jf hatujuani kwa majina yetu halisi?
Ungekua inafatilia sana Jf ungemjuatuu kuwa Jf si kusoma na kutoa mada tuu Bali hata memba unatakiwa kuwafahamu hasa wakongweWafiwa, ndugu, jamaa na marafiki zake poleni sana.
Dena Amsi ana legacy gani hapa jamvini? Anakumbukwa kwa lipi?