Ndugu waTanzania salaaam, Siku ya Jumamosi jioni Balozi wetu wa nchi za BENELUX (Belgium, Netherlands and Luxemburg) Ndugu Simon Mlay alikutana na waTanzania katika Hoteli ya Crowne Plaza, The Hague. Kwa wale tulioudhulia mjumuiko huo, tutakubaliana kabisa kuwa Balozi wetu alitupokea kwa furaha na uchangamfu usio kifani. Kila mtu alifarijikana charisma yake pamoja na uhuru aliotupa kujichanganya naye mara tulipopata wasaa. Hata sisi tulikuokuwa 'tunamuogopa' kama tulivyomuogopa yule mtumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusadikika 😉 tulishangaa kwa jinsi Mheshimiwa alivyojichanganya nasi na kutufanyatujisikie si tu kuwa tuna Balozi, bali pia mlezi wetu wa huku ughaibuni. Kwa kweli ilikuwa mgeni njoo mwenyeji apone 😀 Kwa sababu hili suala ninalotaka kuliongelea ni suala siriasi, basi naomba niache mbwembwe na kuaddress serious issues seriously. Balozi Mlay alikuja na agenda kadhaa. Baada ya kujitambulisha yeye na ofisa mwingine wa ubalozi aliyeandamana naye - Mama Hyera -, Mh Mlayalitoa muktasari wa yale yaliyomleta Netherland. Balozi pia alituruhusu tumuulize maswali mbalimbali. Mwishoni, Balozi aliangusha agenda muhimu kabisa ya kikao. Kwa miaka mingi waTanzania wanaoishi Netherlands wamekosa umoja ambao unawaunganisha bila kujali kabila, dini, rangi, elimu , status nk. Ingawakumekuwa na jitihada za baadhi ya waTanzania ku-take-initiatives za kutuunganisha kwa kupitia groups mbalimbali, jitihada hizi zimekuwa zikigongamwamba kwa sababu mbali mbali. However hivi karibuni ubalozi wetu wa nchi za BENELUX ulianzisha viguvugu la kuunda Umoja wa waTanzania wa nchi hizi tatu ukiwa na malengo ya kutukutanisha na kushughulikia maslai ya waTanzania wa kanda hii. Jitihada hizi pia zilishindwa kutoa matunda yaliyotarajiwa. Badala yake, ubalozi ukaonelea ni vizuri kwanza kuundwe Associations za waTanzania katika kila nchi na baadae iwe ni raisi kuwaunganisha waTanzania kwa kupitia associations zao. Hizi associations zina nia moja tu - kuwaunganisha na kutetea maslai ya waTanzania palewanapoishi bila kujali rangi zao, dini zao, kabila zao, na hata umri wao. Associations hizi si govermental bali zitapata mibaraka yote ya serikali kupitiaubalozini na Balozi kama mlezi wake (unless voted otherwise). Kwa maana hii, Balozi Mlay alitoa wazo la kuundwa kwa Tanzanians Association hapa Uholanzi na kuhaidi kusaidia katika kutoa mawazo, muundo na ushauri ili hatimaye Netherlands iweze kupata Asssociation yake kama zilivyo nchi nyingine duniani. Kwa kuanzia, Balozi Mlay alitoa nafasi kwa waTanzania walioudhuria kupendekeza majina ya Tanzania Association interim committee ambayo mandate yake ni kukusanya mawazo na kujadili katiba itakayounda Tanzania Association hapa Netherlands. Majina yaliyopendekezwa na kupitishwa ni kama ifuatavyo, Damian George Mwenyekiti Utrech dcgeorge@gmail. comKweba, Bulemo Katibu The Hague Bulemo@gmail. comHarold Sungusia Mjumbe Groningen Haroldsung@yahoo. comJoyce Challe Mjumbe Wageningen Joycechalle@ yahoo.comNasobile Mwakila Mjumbe The Hague ma07080@iss. nl Donald Mmari Mjumbe The Hague odara98@yahoo. comLadslaus Modest Mjumbe Delft ladslaus@yahoo. comConjesta Kabete Mjumbe The Hague Miza Mwinyimbegu Mjumbe The Hague Way forward: - In few days kamati itaanza majadiliano online na baadae kupanga muda muafaka wa kukutana na ku-finalise collected reccomendations kuhusu katiba ya Tanzanians Association.- Mtu yeyote mwenye maoni kuhusu muundo wa katiba ya TA, tutaomba atutumie kwenye anuani zetu kama zilivyo hapo juu (au ajibu email hii as addressed in the relevant forum/s)- Naomba umfikishie mTanzania yeyote (hapa Uholanzi) ambaye labda kwa namna moja au nyingine atashindwa kupata hii email. Mara maongezi ya katiba yatakapokamilika tutawajulisha ili tukutane tena kwa ajili ya kupitisha katiba na pia kuchagua viongozi wakwanza wa Tanzania Association hapa Uholanzi. (wagombea binafsi mkae tayari 😉 Siku njema,
Ndugu Kweba, BulemoInterim Secretary Tanzanians Association in The Netherlands.