Nadhani inategemea:-
Disclaimer, yeyote nitakayemtaja achukulie kwamba huo ni mtazamo wangu tu, na kama sijakutaja ujue nimekusahau tu bahati mbaya;
- Lara 1; Huyu ni replaceable kwenye kitengo cha story na connections (baharia wanaelewa hapa kwenye connections)
- Kiranga; Huyu jamaa kasoma vitu vingi sana, na akili sana, hivyo kwa sababu pia JF vilaza ni wengi na hawasomi, automatically anakuwa distinguished.
- Mshana Jr; Huyu jamaa ni moja ya watu ambao ni mfano wa kuigwa linapokuja swala la specialization, jamaa ni specialist kwenye kitengo chake. Ingawa anakuwa anajaribu kuwa all round, ila sifa zangu nampa, he is so so good at his post.
- Mwita25; Huyu ni mtu pekee kwa JF alikuwa anakimbizana na Kiranga kwenye Lugha ya Malkia, alikopotelea sijui.
- Eiyer; Hii ilikuwa ni asset linapokuja swala la Secret Societies, nimesoma series za Dan Brown, ila kila nikimsoma Eiyer, sielewi haya mambo ametumia muda gani kuyajua, na anawafunika waandishi kibao ambao ni best sellers.
- Chief-Mkwawa; He is undisputed when it comes to IT related issues.
- Mzee Mwanakijiji before October 2015; Hakuna bandiko lake ambalo utasema liko shallow kwa kipindi hicho, na nilikuwa na muda special wa kupitia maandishi ya jamaa.
- Mosdef; When it comes to football analysis, this kid is way far, I can't real tell who is the best between him and Gary Nevil.
Special shout outs to Malcom Lumumba, The Bold, Chinchilah Coat, Sky Eclat na Rebeca 83.