Mwana Mfalme Reza Pahlavi alitaka Jeshi kuipindua Serikali ya Iran

Mwana Mfalme Reza Pahlavi alitaka Jeshi kuipindua Serikali ya Iran

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
9,662
Reaction score
8,023
Katika hotuba yake ya hivi karibuni, Reza Pahlavi ametoa ujumbe mzito akililenga Jeshi la Iran, akiwataka kusimama na kulinda taifa badala ya kubaki kimya.

Pahlavi aliwakumbusha wanajeshi hao kuwa wao ni warithi wa makamanda wazalendo wa kihistoria wa taifa hilo.

Alihoji ni jinsi gani wanaweza kubaki kimya na kutochukua hatua yoyote wakati mawakala wa kigeni na wahalifu wanaohusishwa na Jamhuri ya Kiislamu, wakiwemo Hashd al-Shaabi, Hezbollah ya Lebanon, na magaidi kutoka Afghanistan na Pakistani, wakitamba katika mitaa ya Iran.

Kiongozi huyo alikishutumu vikali kikosi cha Jamhuri ya Kiislamu (IRGC) kwa kile alichokiita kuwachinja makumi ya maelfu ya vijana jasiri wa nchi hiyo, na kuendelea kupeleka wengine kwenye vifo vyao kila siku. Aliongeza kuwa watawala hao ambao aliwaita "wavamizi," wameifikisha nchi ukingoni mwa maangamizi kutokana na kile alichokielezea kama wazimu wa uharibifu.

"Mbele ya macho yenu kabisa, Jamhuri ya Kiislamu na kikosi chake cha kigaidi na kandamizi cha IRGC wamechinja makumi ya maelfu ya vijana wa kiume na wa kike walio safi na jasiri wa nchi hii, na kila siku wanapeleka wengine kwenye vifo vyao."
 
Mnafiki mkubwa.
Marekani walioahidi kumrudishia Ufalme wake wameshindwa .
Aende mwenyewe akawongoze askari ili akomboe himaya yake.
 
Jeshi lipi sasa??
Iran kuna majeshi matatu yanayojitegemea.
Artesh, IGRC au Basij??
Kajifunze upya hakuna Jeshi linalojitegemea huko Iran.

Nimeamini huko Masjid Masheike-Ubwabwa yanawadanganya sana
 
Kajifunze upya hakuna Jeshi linalojitegemea huko Iran.

Nimeamini huko Masjid Masheike-Ubwabwa yanawadanganya sana
IRGC inasikiliza order ya Ayatollah tu ndio maana rais alisema hatutoshambulia majirani kamanda wa IRGC akaipinga hyo kauli hila hao wengine wanaweza kumsikiliza rais kwahyo miundo yao tofauti.
 
IRGC inasikiliza order ya Ayatollah tu ndio maana rais alisema hatutoshambulia majirani kamanda wa IRGC akaipinga hyo kauli hila hao wengine wanaweza kumsikiliza rais kwahyo miundo yao tofauti.
Kupinga huko kunatokana na kukosekana kwa chain-Command katika IRGC wala si vinginevyo!!
 
Back
Top Bottom