Mwana mfalme wa Iran aliye uhamishoni, Reza Pahlavi, amwagiwa majimaji mekundu mjini Berlin

Mwana mfalme wa Iran aliye uhamishoni, Reza Pahlavi, amwagiwa majimaji mekundu mjini Berlin

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwana mfalme wa Iran aliye uhamishoni, Reza Pahlavi, amemwagiwa majimaji mekundu Alhamisi wakati akitoka kwenye jengo moja mjini Berlin.

Pahlavi alikuwa ndiyo kwanza ametoka kwenye mkutano na waandishi wa habari, ambapo alikosoa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran, wakati tukio hilo lilipotokea nje ya jengo la mikutano ya habari la shirikisho la Ujerumani.

Alionekana kutoumia kutokana na majimaji hayo yaliyotanda nyuma ya koti lake na shingoni, na aliwapungia mkono wafuasi wake kabla ya kuingia kwenye gari lililoondoka. Polisi walisema kuwa majimaji hayo yalionekana kuwa juisi ya nyanya.

Soma Pia: Mwana Mfalme Reza Pahlavi alitaka Jeshi kuipindua Serikali ya Iran

Mtuhumiwa wa tukio hilo, ambaye jina lake halikutajwa kwa mujibu wa sheria za faragha za Ujerumani, alikamatwa mara moja na polisi.
 
Huyo lazima atakua ni wale Wairan waliokimbia utawala wa mahayatollah na cha ajabu eti na wenyewe hawataki kukaa Iran ila wanapenda kuishi kwenye nchi za wazungu. Bure kabisa.
 
Huyo lazima atakua ni wale Wairan waliokimbia utawala wa mahayatollah na cha ajabu eti na wenyewe hawataki kukaa Iran ila wanapenda kuishi kwenye nchi za wazungu. Bure kabisa.
Huyo ni mtoto wa mfalme wa Iran aliyepinduliwa na kina Ayatollah kupitia mapinduzi mwaka 1979 hivyo hawezi kuishi Iran chini ya kina Ayatollah!

Sema anajidanganya kufanya harakati zake akiamini utawala wa Iran ukiangushwa atapewa yey. Marekani wenyewe huwa hawana adui wa kudumu bali wanajali maslahi yao. Kile Venezuela, mpinzani wa maduro ambaye aliteswa mpaka kukimbilia Marekani aliamini baada ya Maduro atapewa nchi lakini mambo yakawa tofauti na kupewa makamu wa rais wa Maduro!
 
Back
Top Bottom