TANZIA Mwanachama wa JamiiForums (kutoka JF Arusha Wing), Easymutant afariki dunia

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums (kutoka JF Arusha Wing), Easymutant afariki dunia

Poleni sana wafiwa,inasikitisha kwakweli,na sisi tuliokuwa hai tujiandaye kwakuwa karibu na Mungu kwani hatujui siku wala saa...
Apumzike mahali salama, ila hilo la kuwa karibu na Mungu ni hofu tuliyojengewa na wenzetu. Familia yake wapate faraja na kusonga mbele na maisha ya kila siku ingawa kuna changamoto.
 
Nitakujibu law msiba huu. Tunafahamiana na tumeanzisha group la WhatsApp na zaidi kufahaminiana kifamilia. Hata kama unatumia fake ID hutakosa hata mtu mmoja mnayefahamiana. Waliopo huku wapo sehemu tunazoishi
JAMANI HUU MSIBA UNANIKUMBUSHA MSIBA WA MWANAJF DOTO MNZAVA MWEEEE SIKU ZINAENDA SANA
 
Jamani Jamani....

Kuamini ni ngumu bado haswa kwa sisi tuliokuwa tunawasiliana naye karibia kila siku kwenye group letu.....

Umetuweza baba....Endelea kulala salama ....
 
R.I.P Easymutant......dah......siamini kama nakuandikia hivi we lofa......(tulikuwa tukiitana hivi)......Ila sina namna......weee nenda tu......till we meet again my friend.......

Pole best....

Tuyaenzi yale mema aliyokuwa akiyaishi....
 
R.i.p marehemu.
Ninachostaajabu ni kitendo cha mleta mada kuielewa id ya member mwingine!
Ina maana watu humu wanafahamiana pamoja na mafekelo ids?
Hili limekaaje mleta uzi?
Usikae tu kienyeji enyeji huku! We are family also
 
Pumzika kwa Amani mkuu.
WanaJF,
View attachment 1235230
Taarifa nilizozipata ni kwamba, mwenzetu, Easymutant amefariki dunia usiku wa kuamkia Jana kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Sabble Square karibu na uwanja wa ndege wa Kisongo. Msiba upo Olasiti Arusha na updates zaidi nitawaletea hapa.

Poleni sana JF Arusha Wing na Members wote wa JamiiForums kwa ujumla.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

View attachment 1235020

Updates:

Mazishi ni kesho, mwili utachukuliwa Mount Meru Hospitali asubuhi saa 4 na kupelekwa nyumbani kwake saa saba mchana na kupelekwa kanisani Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Olasiti.

Maziko yatafanyika kwenye nyumba yake Mateves chini ya kituo cha mafuta cha OilCom Kisongo baada ya ibada.

Michango ya rambirambi inapokelewa na Hortensia Tarimo kwa namba 0759422471. Yeyote atakayeguswa anaweza kutuma rambirambi yake kwa namba hiyo!

Updates
Jana tumefanikiwa kumpimzisha mwenzetu Easymutant katika nyumba take ya milele. Tunawashukuru wote walioshiriki kufanikisha na kuhudhuria hadi kukamilisha maziko ya mwenzetu. Tunatoa shukrani za kipekee kabisa kwa wana JF Arusha Wing na Jamii Forum HQ kwa ushirikiano was hali ya Juu kabisa na uwakilishi kuanzia nyumbani, kanisani na makaburini. Tunaomba ushirikiano huu udumu milele.

Asanteni nyote.
 
Back
Top Bottom