TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

upumzike kwa amani kamanda. Naomba kwa anayefahamu utaratibu wa kanuni za uchaguzi zinasemaje pale mgombea anapofariki anifhamishe na mimi nijue
 
Nimeshtuka sana, Mohamed Mtoi was a good guy, My friend.
Pumzika kwa Amani. Poleni sana wafiwa.
 
Amefariki kwa ajali inasemekana alikuwa na mwanamziki Roma Mkatoliki

chanzo cm toka muheza ila sina uhakika

kama ni kweli basi familia ya mzee Mtoi inabahati mbaya sana kwani mdogo wa Mohamedi mtoi alifariki pia kwenye tukio la mabomu kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha.

Muhamedi Mtoi ni mwanaharakati wa muda mrefu wa CHADEMA. Amekuwa akishiriki harakati nyinga za kujenga chadema mkoani Arusha na Tanga pia ni Moja kati ya wanajamii Forum anayepost habari nyingi kuhusu harakati za chadema na hana chembe ya uoga kwani hutumia jina lake halisi Mohamed Mtoi

Kwani Kuna Mwenye Guarantee Ya Kuishi Milele Hapa Duniani?
 
Tunaomba serikali ifanye uchunguzi maana CDM kuna katabia ka kulegeza bolti za matairi.
 
إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ

Poleni wafiwa
RIP Mohamedi Mtoi
 
Poleni.wanafamilia, cdm .wanajamii na watanzania msiba hauna itikadi
 
Taarifa za hivi punde ni kuwa kamanda Mohamedi Mtoi amepata ajali na kufariki dunia

WAMETOKA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI TARAFA YA MLOLA.
KAMANDA MTOI AKAWAPELEKA WENZAKE MPAKA LUSHOTO MJINI KISHA AKAONDOKA KUELEKEA NYUMBANI KWAKE NDIO NJIANI GARI IKAPATA AJALI NA NDIPO KAMANDA MTOI AKAFARIKI DUNIA.

Maelezo haya yamethibitishwa na katibu wa chama wilaya Lushoto Kamanda Dulla.

========
UPDATES:

maskini kamanda hujashuhudia tanzania mpya apo october? Mwenyezi mungu mrehemu na wape nguvu ndugu zake tupo pamoja kwenye uzuni. Apumzike kwa amani ni kazi yako baba
 
Umeeondoka ukiwa bado Taifa linakuitaji. Nakumbuka tulivokuwa woote Mwenye University, fikra na mawazo yako yalikuwa chachuvya maendeleo yetu.

R.I.P Mtoi
 
RIP Mtoi,

Umeondoka wakati ambao unahitajika sana kwenye jamii na taifa kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom