afahamika sana hapa lakini siyo wengi wanajua historia yake. Kufuatia hayo, yaliyomsibu kwa sababu ya CHADEMA, ni jambo la kuangalia kwa makini sana mintarafu usalama wa chama na viongozi wake.
Nashauri haraka na lazima,idara yetu ya ulinzi na usalama,na inteligensia, ihakikishe Mtoi hakutani na dokta Slaa na Mbowe akiwa peke yake.
Kwasababu ya uharaka na unyeti wa jambo hili,nategemea ujumbe huu utafsiriwe katika proper context, ndiyo maana nimeandika kwa jina langu.
Nimeshauri
By Mohamedi Mtoi:
Wakuu.
Sikutaka kumjibu Ludovick kwa kuwa majibu ya Afisa habari wetu wa chama kamanda Tumaini Makene yalijitosheleza sana! Nimeamua kumjibu binafsi kwa kuwa anaweza kuibua hofu isiyokuwa na msingi kutokana na matumizi ya lugha aliyotumia.
Kwenye sehemu ya bandiko lake kwa wale wanaojua kukusanya na kuunganisha nukta ameandika hivi "... Kufuatia hayo yaliyo msibu kwa sababu ya CHADEMA...".
Japo kwenye bandiko lake hukueleza yaliyonisibu ni yapi, lakini wakati huohuo amejivika kuwa msemaji wangu ambaye kwa haiba na matendo yake ya usaliti kwenye chama siwezi kumruhusu kufanya hivyo, bali anaweza kuwa msemaji anaye tumiwa na waliowahi kumtumia kuiangamiza CHADEMA kwa ugaidi fake na mwishowe wakashindwa wote.
Mpaka amekuja kuandika ujumbe wake hapo juu, Sina lolote lililo nikumba ndani ya CHADEMA na natimiza majukumu yangu na wajibu wangu kwa chama chetu ambacho naamini kwa matendo na mwenendo wake (Ludovick Joseph) hawezi kuwa na udhu wa kukisemea achilia mbali kujinasibu kuwa ni mwanachama.
Kama kuna lolote baya linaloweza kunikumbuka na kunidhuru kama ilivyotokea kwa Kibanda ambaye kwenye moja ya mchango wake kule mabadiliko alisema "...miongoni mwa watu walio nivamia ana fanana na Joseph Ludovick...",wakati huo Ludovick akiwa wa kwanza kuripoti kwenye mitandao kuwa Kibanda amevamiwa, litafanya nikumbuke hiyo kauli yake ya "...Yaliyo msibu kwa sababu ya CHADEMA.."
Ninachoweza kumuambia, NIKO TAYARI KWA LOLOTE maana najua hawashindwi kufanya lolote kama jinsi ambayo wamekuwa mafundi wa kupanga yote waliyopanga na wakashindwa kwenye yote.
"Foward ever, backward never"
CLEOPA sikuona damu ya usaliti Kwa afisa habari huyu ambaye alizaliwa lushoto akakulia lushoto akasoma lushoto-Lafudhi Yake, unyenyekevu wake Na kutosaliti Na kushinda mawimbi vitaishi milele