TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

Natamani Yericko aje kukanusha habari hizi. siamini macho yangu.
 
Mkuu Mohamedi Mtoi nakosa maneno ya haraka kukuelezea kwa muda huu kamanda...ila nitajipanga, na ninaahidi kulitendea haki jina lako lisisahaulike milele...utaishi katika fikra zetu na mioyo yetu wapenda mabadiliko! Ulikuwa mtu unaebadilika kufuatana na wakati,mwanamapinduzi wa fikra,mchokonozi wa fikra na mtu wa kusimamia unachokiamini...Umeondoka wakati ukombozi wa kweli ukichanua...Pumzika kwa amani mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Dah! Sina hata cha kusema, pumzika kwa amani kaka
 
RIP Kamanda,alikua anatumia jina gani humu JF maana Heading inasema ni mwanachama wa JF
 
Mkuu Mohamedi Mtoi nakosa maneno ya haraka kukuelezea kwa muda huu kamanda...ila nitajipanga, na ninaahidi kulitendea haki jina lako lisisahaulike milele...utaishi katika fikra zetu na mioyo yetu wapenda mabadiliko! Ulikuwa mtu unaebadilika kufuatana na wakati,mwanamapinduzi wa fikra,mchokonozi wa fikra na mtu wa kusimamia unachokiamini...Umeondoka wakati ukombozi wa kweli ukichanua...Pumzika kwa amani mkuu!

Mkuu yatakuwa MA-CCM HAYA dah R.I.P brother
 
Last edited by a moderator:
Pumzika kwa amani kamanda Mtoi mpenda mabadiliko umeondoka wakati wa ukombozi kamanda pumzika kwa amani kamanda pole kwa familia na watanzania wana ukawa kwa kuondokewa na kamanda wetu pumzika kwa amani kamanda mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi
 
Ajali za magari Tanzania imekuwa ni kama ngoma ya mdundiko, ikipita mtaani hakuna anaesumbuka kuchungulia. Hakuna anaetaka kujua ajali ilikuwaje kuwaje, na tuna dili nazo vipi kama tatizo la kitaifa.

Mtu kafa kwenye ajali kafa! That's it. Bwana asifiwe na Inna Lilah Waina kibaaao... Nobody cares how it happened. Third world maladies.
 
May God rest his soul in peace. Most of us we didn't know you in person, but this tragedy has shocked all of us. But we will never forget the love you had to this country.
 
..umesema kweli kabisa.

..yaani huyu dogo alikuwa kijana mtulivu ktk mijadala, na tena msikivu. nilimpenda kama mdogo wangu.

..kila nikimtumia ujumbe alikuwa mwepesi kujibu. ukimuuliza maswali mwepesi kuyajibu. tukimrushia maduku-duku yetu kuhusu chadema hakusita kutujibu tena kwa uungwana wa hali ya juu.

..lakini nisichokisahau ni kila ujumbe wake alionitumia, alimaliza na maneno, KILA JEMA NA LENYE KHERI LISIKUPONYOKE.

cc Nguruvi3, lusungo, Jasusi

Mkuu hiyo kauli yake imenifanya nilie nikiikumbuka....

Aisee jamaa ilikua ni vigumu kumkwaza au kukwaza wenzake... zaidi sana upole... uungwana... upendo!!

Sijui kwanini dunia ina huzuni na mateso hivi!!!

Mungu aipe wepesi na faraja familia yake ktk wakati huu mgumu.
 
Last edited by a moderator:
Pumzika kwa amani kamanda Mtoi mpenda mabadiliko umeondoka wakati wa ukombozi kamanda pumzika kwa amani kamanda pole kwa familia na watanzania wana ukawa kwa kuondokewa na kamanda wetu pumzika kwa amani kamanda mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi

Inauma sana Mkuu...wacha kamanda apumzike kwa amani sema kamanda unajua nini?? Tuwe na mashaka na MA-CCM kwa kifo cha kamanda wetu si unajua sisi hatuamini katika Mungu...kila kitu sisi tunakomaa tu kwamba ni Ma-CCM #RIP brother Mtoi
 
Huu ni mshumaa uliozima ghafla.....wala sitaki hata kuamini. Eee mungu tupe basi hata siri ya siku ya kuishi kwetu kwani twaweza japo kidogo kujua kipi tukifanye na kipi tukiache. R.I.P mtoi.......we won't see U anymore.
 
Taarifa za hivi punde nikuwa kamanda Mohamedi Mtoi amepata ajali na kufariki dunia

WAMETOKA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI TARAFA YA MLOLA.
KAMANDA MTOI AKAWAPELEKA WENZAKE MPAKA LUSHOTO MJINI KISHA AKAONDOKA KUELEKEA NYUMBANI KWAKE NDIO NJIANI GARI IKAPATA AJALI NA NDIPO KAMANDA MTOI AKAFARIKI DUNIA.

Maelezo haya yamethibitishwa na katibu wa chama wilaya Lushoto Kamanda Dulla.

========
UPDATES:

Pumzika kwa amani Bw. Mtoi, hakika tutakukumbuka
 
Ikiwa kuna aliyehusika kwa namna moja ama nyingine,atalipishwa mara 100 udhalimu huu....nina uchungu uliochanganyika na hasira...

Mkuu si unajua sisi UKAWA kila kitu tunaamini ni mipango ya Ma-CCM HATUAMINI KUWA MUNGU ANAMAAMUZI JUU YETU
 
Nakukumbuka toka enzi za Old Tanga, Mungu akupumzishe mahala pema, what a way and time to go
 
Back
Top Bottom