TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

What exactly happened?

Sawa ni ajali, lakini ilitokeaje....tufahamishwe basis.

Gari imegonga mti? Imepinduka? Zimegongana uso kwa uso?

How? How?......kwa sababu huyu kamanda ni miongoni mwa wana JF ambao possibility yao kuingia bungeni ilikuwa ni over 90%!

Kwa kweli it pains, lakini hatuna jinsi. Kamanda katangulia mbele ya haki.

R.I.P kamanda....lakini tunakuhakikishia huko huko uliko, hamasa yetu ya mabadiliko nje ya CCM ndiyo imeongezeka zaidi!!

Aluta continua!

ni swali zuri mkuu.......
 
Lets all believes on natural death and no body is behind his death as he was such a big threat kwa CCM Lushoto, Stay in Peace in God we Trust
 
Japokuwa mimi si mwanachama wa CHADEMA lakini nilikuwa navutiwa sana na hoja zake ambazo zilikuwa ni za kweli makini, zenye uchambuzi wa kisayansi na madhubuti. Nilitaka sana ashinde ubunge ili mchango wake uweze kunufaisha Taifa kupitia bungeni. Hakuwa mdini alikuwa mzalendo wa kweli.

Kifo chake kimenihuzunisha sana.

Raha ya milele umpe ee bwana, na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani Amen X 3

Amina, RIP Mtoi!
 
Hakuna nafsi ambayo haitauonja umauti!!
R.I.P Kamanda Mtoi
 
Nimeshtuka sana sina la kusema ni kumuachia mungu. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
 
japo jamaa nlikuwa napinagana nae sana mambo mengi,lakini jamaa kaniuma sana ,innalillah wainna ilayh raajiun mohammmed Mtoi daima tutakukumbuka
 
Last edited by a moderator:
Daah siamini.. Rip brother! Nimetoka lushoto juzi na kukubali harakati zako na jinsi unavyokubalika. Poleni wafiwa..
 
Heshima kwake Kamanda Mtoi. Mwenyezi Mungu ampumzishe pema. Huyu ni miongoni mwa waislam wenye akili walionisaidia kuikataa propaganda ya CCM kuwa CDM ni chama cha kanisa 2010.
 
hii habari ni ngumu sana kwangu, huyu jamaa .... dahhaaa, kweli tujiandae kila sekunde maana hatujui saa wala dakika... Mtoi??,,......... duuuhh, sometime nikiwazaga haya maisha yetu binadaamu hata sionagi maana yake....


Ndio maana tunahitaji kuwaelimisha hawa CCM waache udhalimu kwani unawadhulumu watu kumbe unajiongezea madhambi tu na hujui wakati gani unaondoka duniani.

Mali yote uliyoichuma kwa ufisadi unaiwacha hapahapa
 
Jamani kamanda Mtoi nakulilia, ulikuwa mzalendo, mpambanaji wa kweli wa taifa lako. Utakumbukwa katika mioyo ya wengi. RIP Mohamed.
 
Yaani nimeumia sana nimeumia kupita maelezo.

Pole nyingi kwa Familia, Chama, Wananchi wa jimbo la Lushoto na Tanzania kwa ujumla. Tumempoteza mtetezi wa haki za Watanzania wa ukweli. Nenda Kamanda Mtoi, Mbele yako nyuma yetu. Wananchi wa Loshoto wana kila sababu ya kuenzi Spirit yako ktk kusaka Mabadiriko.

Watanzania, WanaJf na Wanacdm tutakukumbuka daima na tutayaenzi mazuri yote toka kwako....grrrrrrrrrrriiiiiiiiii... Tangulia Comrade.

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom