Mwanachama wa Yanga Mwigulu Nchema amrudisha Kocha Pluijm

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Uongozi wa Yanga umeandika barua ya kumuomba kocha Pluijm afute maamuzi ya kujiuzulu, hiyo ni baada ya kukaa na Pluijm, Baraka na Mwigulu.


=====
 

Mh.Mwigulu Nchemba amemrejesha kocha wa Yanga Hans Van De Pluijm ambaye alijiuzulu kuiongoza timu hiyog mapema wiki hii.

Katika mazungumzo yaliyodumu takribani siku tatu,Mchana huu Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.

Hii ni mara ya pili mwigulu nchemba anafanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya Club ya yanga,msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha Kiungo Haruna Niyonzima kuichezea Yanga.

Ikumbukwe,Mwigulu Nchemba ni mdau wa michezo nchi na mpenzi wa soka na mwanachama wa Jangwani "Yanga"

=========

Uongozi wa Klabu ya Yanga, umelezimika kumuangukia aliyekuwa kocha wake, Hans van der Pluijm na hii ni barua ambayo uongozi wa klabu hiyo umemuandikia kukataa ombi lake la kutaka kuachia ngazi.

Pluijm aliandika barua kujizulu Oktoba 22, 2016 baada ya Yanga kuamua kufanya mazungumzo na Kocha George Lwandamina raia wa Zambia. Ili kumrejesha Hans van Pluijm ndani ya klabu hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na kocha huyo kumsihi kutojiuzulu nafasi ya Kocha Mkuu wa Yanga.
 
Nilichojifunza kwenye hili sakata la babu hans ni kua yanga walikurupuku.Ni sawa na mtu kuacha kazi wakati huna uhakika na kazi mpya.
 
ninachokiona hapo nchemba yeye ni kama mwanachama wa kawaida tu,,ila kutokana na uheshimiwa wake ndio maana kapata nafasi ya kusikilizwa na huyo kocha,,na hapo me sioni kama kuna siasa ,,imekuwa kasumba kwa watanzania kwamba jambo likifanywa na mwanasiasa basi linasemwa ni la kisiasa,,tubadilike jaman,,
 
leo mwigulu nchemba amemrejesha kocha wa yanga aliyejihuzulu wiki iliyopita je? nape alishindwa kumshauri huyu kocha mahili hii inatuletea picha gani ?
 
Siasa hizi bhana, hivi huyo nchemba anauongozi pale bwawani?
Nawaza tu kama asingekuwa waziri/mbunge kama hii habari ingekuwa na hii title!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…