Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Uongozi wa Yanga umeandika barua ya kumuomba kocha Pluijm afute maamuzi ya kujiuzulu, hiyo ni baada ya kukaa na Pluijm, Baraka na Mwigulu.
=====
=====
![]()
Mh.Mwigulu Nchemba amemrejesha kocha wa Yanga Hans Van De Pluijm ambaye alijiuzulu kuiongoza timu hiyog mapema wiki hii.
Katika mazungumzo yaliyodumu takribani siku tatu,Mchana huu Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.
Hii ni mara ya pili mwigulu nchemba anafanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya Club ya yanga,msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha Kiungo Haruna Niyonzima kuichezea Yanga.
Ikumbukwe,Mwigulu Nchemba ni mdau wa michezo nchi na mpenzi wa soka na mwanachama wa Jangwani "Yanga"![]()
=========
Uongozi wa Klabu ya Yanga, umelezimika kumuangukia aliyekuwa kocha wake, Hans van der Pluijm na hii ni barua ambayo uongozi wa klabu hiyo umemuandikia kukataa ombi lake la kutaka kuachia ngazi.
Pluijm aliandika barua kujizulu Oktoba 22, 2016 baada ya Yanga kuamua kufanya mazungumzo na Kocha George Lwandamina raia wa Zambia. Ili kumrejesha Hans van Pluijm ndani ya klabu hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na kocha huyo kumsihi kutojiuzulu nafasi ya Kocha Mkuu wa Yanga.