Mwanadamu anatawaliwa na falme mbili

Mwanadamu anatawaliwa na falme mbili

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Binadamu pamoja na utashi na maarifa yote aliyonayo lakini kamwe hawezi kujiongoza yeye kama yeye... Lazima kuna mahali aegame... Anapopaamini kwa namna yoyote ile moja kwa moja ama kinyume nyume! Hana utashi wa kujisimamia mwenyewe na akijaribu huishia kubaki na mkanganyiko mkubwa

UFALME WA KWANZA
Ni ufalme mama... Ufalme wa mbingu... Mamlaka ya juu kabisa kiimani katika uumbaji na utamatishaji wa chochote kilichoumbwa.... Mamlaka ya kimungu...huu ni ufalme kamili
Dunia imeumbwa na uwili.. Kila kilichopo kina mbadala wake... Kiwe chenye uhai ama kisicho na uhai.. Ni uwili asilia... Uwili mbadala... Hivyo basi ufalme wa mbingu una mbadala wake ama kinyume chake

UFALME WA PILI
Huu ni mbadala na kinyume cha ufalme wa mbingu... Unajulikana kama ufalme wa anga
Asili ya ufalme wa anga kiasili ni ufunguo wenye kukamilisha dhana ya uwili... Haupo hapa ulipo... Upo kwa ajili ya kutimilisha unabii
Ufalme wa anga ni kamilisho la hitaji la kiumbaji katika ufunuo wa roho, upo kwa ajili ya kupingana na ufalme wa mbingu... Baadhi husema ni UFALME WA NURU DHIDI YA UFALME WA GIZA

Falme hizi mbili ndio engine zinazoendesha dunia toka kuumbwa mpaka kukoma kuwa.... Toka ulimwengu wa macho mpaka ulimwengu wa roho.. Sote ni waamini na waabudu falme hizi mbili.... Kama kuna mtu anaweza kujitokeza na kwa hakika kabisa akasema yeye si mfuasi wa mojawapo kati ya hizi falme mbili, msikilize mpaka mwisho tuu... Hitimisho lake litaangukia kwenye mojawapo ya falme hizi mbili
Habari za wapinga Kristo, Freemason, atheists nk, zote zinaangukia kwenye kundi la ufalme wa anga kwa kutumia misingi na falsafa za maandiko ya ufalme wa Mbingu.... Wanaweza kuchagiza na kutoa hoja zenye kushawishi sana lakini mwisho huangukia kundi lile lile la kuwaabudu wanafizia wanafilosofia na wanazuoni kwa kutumia mabandiko yao kama mifano na vyanzo vya kuthibitisha hoja zao.,...

Kama ilivyo kwa uhai na kifo.. Hata hizi falme mbili, zinaangukia kwenye falme hai na falme mfu
Maandiko ya falme za mbingu katika ujumla wake... Kwa kesi hii Bible takatifu... Yana mwanzo lakini hayana mwisho bali mwisho wake ni kitabu cha ufunuo wa utabiri ya yajayo... Lakini falme za anga mabandiko yake yana mwanzo na yana mwisho... Yakihitimisha yamehitimisha....

Huna haja ya kubabaika na kuanza kuchagua ufalme, asili hukuchunga na kukuchagulia njia... Ni unabii na ufunuo wa aina yake... Kila mtu kila kitu kinaishi kwa kufuata miongozo ya falme hizi mbili mpaka kikomo cha tamati
Na daima tunaziishi hizi falme mbili kwa mfuatano wa ajabu, ukishika huu kidogo unachabanga nao wee inafika mahali unakuchosha na kubadili uelekeo.... Sometimes tunaswitch hizi falme mara nyingi ndani ya muda mfupi tuu.... Falme hizi ni unabii na ufunuo vilivyo juu ya utashi na maamuzi ya kibinadamu ndio maana daima tunaishi tukikigwaya kifo ila muda unapofika tunakufa na hatuna jinsi ya kukikataa kifo
 
Mshana, umesema suna haja ya kuchagua asili hunichunga. Hii asili ni nini ambayo inanifanya nisiwe na free will ktk machaguzi.
Vipi mbona kuna mtu anaamua kuwa atheist ktk kipindi fulani cha maisha je asili ndo imemchagulia iwe destiny yake au inaweza kumfanya across tena ktk kuamini?
Mwisho wa anayeamini ktk ufalme wa anga unaamuliwa na ufalme wa Mbingu Asili ndo itaamua mwisho wake?
 
Mimi ni mfuasi wa "Niko ambaye Niko" milele iliyopita na milele ijayo..

Yeye aliye Alfa tena Omega.
Aaamen... Japo kuna kuanguka hapa na pale, muhimu ni kusimama na kusonga mbele ama kujikwaa na kuteleza
 
Mshana, umesema suna haja ya kuchagua asili hunichunga. Hii asili ni nini ambayo inanifanya nisiwe na free will ktk machaguzi.
Vipi mbona kuna mtu anaamua kuwa atheist ktk kipindi fulani cha maisha je asili ndo imemchagulia iwe destiny yake au inaweza kumfanya across tena ktk kuamini?
Mwisho wa anayeamini ktk ufalme wa anga unaamuliwa na ufalme wa Mbingu Asili ndo itaamua mwisho wake?
Asili ninayozungumzia inahusika na mambo yafuatayo
. Kizalia
. Makuzi
. Harakati za shule
. Harakati za maisha nknk
Haya yote huathiri mitazamo maamuzi na maono yote... Ni mpaka ufunuliwe ndio huweza kusimama kutafakari kuhoji na kuamua.. Lakini bado asili haitakuacha.. Nimetumia asili kwenye Kizalia kwakuwa hapo ndio shinani
 
mshana huwa nazikubali sana post zako.lkn Mimi nina shida moja .nawezaje kupata ufunuo juu ya haya uliyosema
Rahisi sana
Fikiria walioko gerezani
Fikiria walioko madarakani
Fikiria walioko mitaani
Fikiria kila kitu kwa uzuri na ubaya wake
Angalia maamuzi ya watu hasi na chanya
Jiangalie mwenyewe jichunguze.... Jitafakari
 
Dah ok katika dunia hii kila kitu kina pande mbili... Kila upande ni kiwakilishi cha ufalme mmojawapo
sawa. usione nakusumbua ukafikiri bure.nafanya hivyo Kwa sbb kuna mambo yalishanitokea kwenye maisha yangu na mkp sasa yameniaribia maisha yangu Kwa kiasi kikubwa sana .na watu ninaowahisi au kujulishwa walikuwa watu wangu Wa karibu sana na niliwaamini sana.lkn tokea siku nilipopata habari zao kwa upande Wa Pili wamekuwa maadui zangu wa wazi na wamejitenga na Mimi kabisa.lkn ukikutana nao njiani ni waumini wazuri sana hawakosi kanisani na wanasali sana tena zile sala ndefu.sasa nilitaka kujua je? hawa nao wanaomba Mungu huyu huyu tunaemwomba sisi au
 
sawa. usione nakusumbua ukafikiri bure.nafanya hivyo Kwa sbb kuna mambo yalishanitokea kwenye maisha yangu na mkp sasa yameniaribia maisha yangu Kwa kiasi kikubwa sana .na watu ninaowahisi au kujulishwa walikuwa watu wangu Wa karibu sana na niliwaamini sana.lkn tokea siku nilipopata habari zao kwa upande Wa Pili wamekuwa maadui zangu wa wazi na wamejitenga na Mimi kabisa.lkn ukikutana nao njiani ni waumini wazuri sana hawakosi kanisani na wanasali sana tena zile sala ndefu.sasa nilitaka kujua je? hawa nao wanaomba Mungu huyu huyu tunaemwomba sisi au
Pole sana hata ndani ya hizo nyumba za ibada kuna waumini pande mbili wanaotumikia falme mbili lakini wakivaa ngozi ya kondoo kuficha uhalisia... Wengine wanahinikizwa na vishawishi tu
 
Complete perspective is complete understanding and truth. Every piece of the puzzle is important.You are never too far away from error. It’s only a few degrees away from the truth.

You are never too far away from the truth either. It is only a few degrees back.Inspiration has a holistic nature. Inspiration and creativity are one.

Creativity is the ability to make connections, relate truths, combine ideas and integrate concepts into a single whole. Creativity combines existing forms to create new ones that are differentiated yet complete, or complete yet differentiated.

The greater truth should be able to hold other truths within it. If not, it is not the greater truth.Always advance to the next level in your understanding of things. Be willing to refine your thinking and shift paradigms. Be formless, be changeable structure
😕 😕

Put yourself in the speed state of mind with consciousness moving from one thing to the next without
stopping and sometimes even skipping. A state of non attachment, formlessness, free flowing,
changeability, without a care, acting at will without hesitation according


The truth is everything and available for free. No one actually owns anything because it is all part of the universe. Ownership is an idea where people agree what belongs to who and what rights do they have regarding it.

Ownership of anything is all based on agreement between consciousness. When there is conflict of consciousness, people fight and take from each other by force against the will. When there is harmony of consciousness, people willingly agree in sharing or exchanging ownership of things.

By the way nimefurahia somo lako hapo juu.. 🙂 🙂
 
Back
Top Bottom