hapana. ila ni pale tunapoifanya migumu mioyo yetu.
Dini ya kweli ni ipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hapana. ila ni pale tunapoifanya migumu mioyo yetu.
Dini ya kweli ni ipi?
Nilisema hivyo kwakuwa uumbaji wa kwenye bible si sawa na wa kwenye quran, pia sijui budha, hindus na dini nyingine zinasemaje.
Pamoja na hilo kwann tuamini kuwa uumbaji wa kwenye bible ndio standard?
What if evolution theory inzungumzia uumbaji in a different way?
SOma James 1:27 pale anaposema Religion that God our Father accepts as pure and faultless is this: to look after orphans and widows in their distress and to keep oneself from being polluted by the world. Pia soma Deuteronomy 14:29 "so that the Levites (who have no allotment or inheritance of their own) and the aliens, the fatherless and the widows who live in your towns may come and eat and be satisfied, and so that the LORD your God may bless you in all the work of your hands." Mahala pengine unaweza kupitia maeneo haya Deuteronomy 14:29 ,Job 31:16, Job 31:17, Psalm 146:9, Isaiah 1:17, Isaiah 1:23, Matthew 12:32, Matthew 25:36.' Romans 2:13Galatians 3:11Ephesians 2:2, Titus 2:12, James 3:9, James 4:4, 2 Peter 1:4, 2 Peter 2:20, 2 Peter 3:14, 1 John 2:15, 1 John 5:18. Natumaini utaelewa Dini ya kweli ni ipi.
Kwa Biblia na Quran ni rahisi kuangalia, kwa yale mambo ya kufanana jinsi yanavyoongelewa.Biblia ndio ya kwanza kuyasema.Quran ikafuatia na Uandisi wa Quran umekuwa influenced na Biblia sana, na hii ipo wazi sana katik vitabu vya Kiislam.Kama issue ya wakristu kuficha vitabu, kama Mtume kupewa hifadhi na wakritu wa Ethiopia, kam mtume kuhitaji Padri wa Kikristu ku approve kuwa yeye ni Nabii wa Mungu.So its obvious that Biblia is more original than the latter. N ayenyewe ndio ilikuwa msingi wa Quran, kwani hata manabii wengi wa Biblia wamekuja Tajwa katika Quran na wengine kwa njia tofauti zaidi.Imani nyingine hazikujiwekeza sana katika uumbaji na hivyo kuachia mwanya wa explaination nyingi nyingi.
So game inabaki kati ya Biblia na Sayansi.Sayansi nayo ina maelezo mengi na youte yamebaki kuwa theory, na hivyo kuacha mwanya wa kuthibitishwa tofauti.
Nashukuru sana kwakuelewa point yangu na kuwa open minded.
I like this kind of discussion.
Nakubaliana na wewe kuwa bible ilitangulia na kuna similarities kati ya vitabu hivyo viwili.
Ila wakati bible inazungumzia uumbaji wa mwanadamu kwa udongo, quran inazungumzia tone la manii(kama sijakosea).
Hapo tayari kunatofauti na kila moja kati ya dini hizo mbili zinaamini ziko sahihi.
Na haiwezi kueleweka kwa sababu wameshaambiwa waamini...ili uwe muumini mzuri ni lazima uwe hauelewi,kama waumuni wote wakielewa Dini itakua ndo mwisho wake kwa hiyo sifa kubwa ya kua muumini ni lazima uwe hauelewi,Histiria inaonyesha walioelewa wote walionekana si waumini wazuri na wengine hata kuuawa kama akina Galileo Galilei.
kila kitu kina mapungufu mkuu
kila kitu kina mapungufu mkuu
Hilo ndilo ambalo wengi hawataki kulikubali mkuu.
Dini ipi ni imara na inafaa?
yeah..ila katika quote yangu nimeweka mchuano unabaki katika Bible na Sayansi.Na sababu ni rahisi tuu.kama yenyewe ndio ilianza leta claims za uumbaji,Quran ikafautia ikiwa na diffrence katik jinsi ya uumbaji, na siku zilizotumika.Na pia Quran ndio imebeba influence za Biblia na si kinyume. huna haja ya kupoteza muda kuangalia tofati zao "wakati issue ni origin of man" kwa hio una kambi inayoongelea kuwa ni "Uumbaji" na Nyingine ya sayansi ambayo ni "by chance then evolution".
Katika utafiti huwa sometimes kunahitajika ku eliminate other parameters.so hapa ni either Biblia na Quran ziwe kambi moja gainst science .kama creation ikiwa ndio inayokaribia usahihi zaidi then ndio waje kuangalia uumbaji huo ulifanyika namna gani hapo ndipo watapishana wao kwa wao ,baada ya kueliminate science.
Ila science nayo inastruggle haswa katika uumbaji tofauti na kelele unazozisikia ktik media na mafuvu wanayochimba.Kwani hayo mafuvu Biblia inayo majibu yake na yana support ya kisayansi.
mi naamin kila kitu baada ya creation ni man made ambayo huwa haijatimia always japo sitaki kuongelea creation sababu sina evidence against or for it ila maswali yakujiuliza ni kwanini watu huamin vitabu vya miongozo ya dini? Na creation ilifanyika wap exactly? Na why does God let us fall to sin? Nawasilisha wakuu
Hili swali ni tricky...kwani kama Ukristu si Dini kama dini nyingine.Yesu hakuhubiri dini, ila Injili.Na ndio panapowachanganya waislam na wakristu.
Baadaya kuamua jinsi ya ku approach hizo dini then ndio unaingia katika theology za hayo makundi bila kuwa biased ndipo utajua kundi gani utafuata mafundisho yao.Halafu katik hilo kundi ndipo utaangalia ni jinsi gani utafuata hayo mafundisho kufikia malengo yako.Kama ni ukombozi na kuiona mbingu au kama ni kuweza yaishi haya maisha ya dunia kwa kuwa na identity fulani.
Ni vizuri kujua kwanza na lengo la wewe kuamini.Halafu tafuta univeral values ambazo mwanadamu anahitaji kuzishika ili mahusiano yake na dunia, na wengine na yake binafsi yawe mazuri.Jaribu ziangalia zitatumikaje kufanikisha wokovu wako.Then angalia dini gani ina zitekeleza vyema.then zitumie kama vipimo vya kupima mafundisho yao,utekelezaji wake, kwani katika dini nyingine mambo hayatekelezeki kiasi cha kuchanganya waumini wao katika mambo ya msingi.Pia angalia staha, wasifu binafsi wa nabii husika.Kama nabii anakupa shida sana kumwelezea kukupata karaha, kama sifa zake zinatosha mpatia nafasi katika maisha yako na ungependa ufanyake kama yeye bila kuvunja universal principles ulizoziandika.Pia huyo nabii awe na sifa za kiroho asiwe tuu just kiongozi.Nadhani utakuwa katika sehmu nzuri ya kuifuata hiyo dini.
evolution kama ilivyo katika Darwin theory ni kama dini zaidi kuliko science ndio maana ni theory na kila kitu wanasema"its believed" yaani" inaaminika". halafu wanakimbilia kutumia science kuwajibia.Na hata kabla ya kuanza evolution pana theory inayolezea mkusanyiko wa gas unaozaa "amino acids" ambazo ndizo zinakuwa msingi wa cell za maisha ndogo sana na baadaye "evolution " ikachukua nafasi.hapa kuna shida nyingi sana. ahap kwenye amino acid mambo yote ni kwa bahati "chances" na ktika evolution mamabo ni "chances+randomness".
Science imepata picture sana kuweza kuona jinsi gani chances inaweza fanya chochote kufanya vitu vinavyohitaji "exactness".yaani ili kupata cell hai , panahitajika kila kitu kiwe sahihi (temperature,humidity, PH,ammonium gas, oxygen(kumbuka miti nayo haipo)),gravitation field weather, na radi zipige kwa kiasi cha sahihi ili zitengeneze hizo chemical reactions etc, halafu baad ay kupata hiyo cell ipate mazingira sahihi ili isife kwa miaka million kadhaa ili ibadilike na huku ikiwa zinazaana. Then evolution ipate nafasi n aiafany kazi katika hizo bahati nasibu zake na kuweza kupata makundi tofauti ya viumbe hai, na hao hao viumbe tena kibahati nasibu waanze jifunza kukabilian ana mazingira, tutangoja sana kuona jinsi gani samaki aweze kupata mapafu ili aje nchi kavu kama mazingira yanabadilika sana na maji kuwa hayafai.
Uumbaji unasema kuwa viumbe waliumbwa kama walivyo na kwa mazingira husika.na hii inafanya mazingira yakibadilika basi wanaweza adapt mazingira katik viwango vyenye mipaka.Yaani binadamu bila vifaa anaweza jifunza ishi katik kiwango fulani cha baridi na joto na kikivuka basi kam asi kuhama ni kudhurika na hata kuangamia.kuna viumbe wa baharini kwa miaka yote wameweza tuu kukaa katik maji kwa muda fulani, na si kwa maisha yao bila kupanda juu na kupata hewa.
Kuna horinzotal evolution an vertical evolution.Horizontal ndio kama hii tunayoiona kuwa jinsi watu wanavyokula vizuri na kufanya mazoezi wanakuwa na mabadiliko ya urefu,unene, uelewa na mengine ila hawaami na kuwa specie nyingine.Vertical ni kuhama katika species na hii haifanyiki yenyewe ,na katik lab wanabadili wanasayansi ila ktk nature hakuna.Otherwise utaambiwa kiumbe fulani kazaliwa kilema.
Hapa ndipo alipo boogie darwin katika observation yake.na wote kati yetu hapa tutazaa binadamu siku sote tofauti itakuwa urefu, ila kwa sehemu kubwa tunarithishana kila kitu.
Ukweli ni kwamba science inafuata vitabu vya dini na Haswa Biblia,kwa vile Watafiti wengi ktik kipindi cha madabiliko ya sayansi wametoka magharibi, na huko magharibi kuna vunguvungu la kuhoji kila kitu na kuna makundi yasiyopenda uwepo wa Mungu.
Kuna makundi yaliyokuwa yakisoma Biblia na kupata mawazo ya ugunduzi na hawa ni akina Eistein, Newtons etc, na kuna makundi yaliyokuwa yakiisoma na kutafuta namna ya kuthibitisha tofauti sana hawa kuan walioishia kuikubali na wengine kuikaaa na ndio walipotez amaisha yao yote kukimbizana na kutafuta ushahidi wapingamizi zao.
Vitabu vingine havijawekwa katika uchambuzi mkali kama wa Biblia kwa vile vingine haviongelei uumbaji au mengine yanayowanyima uhuru wasipenda uwepo wa Mungu, ama wafuasi wake ni wakali kabisa na hawataki vitabu vyao viulizwe maswali makali kwani wanaona kama ni kufuru.
Mpaka sasa wana sayansi wamethibitisha uwepo wa characters wengi katika Biblia, na masalia ya kihistoria kutokana na matukio.Pia sayansi inathibitisha kuwa maji yaliyopo duniani yanatosha zamisha dunia.Pia matukio ya kijiologia yamefanya ardhi kuvimba na hivyo kuifanya iwe na nchi kavu kama vichuu ktik dunia.Watu wame reverse uchafuzi wa genes na kuona kuwa uwepo wa binadamu duniani hauzidi miaka 8000.Yaani kadiri siku zinakwenda genes za viumbe hai vinachafuka kiasi cha kuwafanya watafunwe na magonjwa ya kuridhi, na hivyo kuwafanya wazaane kupitia wenza wa jamii nyingine ili kupunguza uwekano wa kukuza udhaifu wao.Na hii nafikisha mahali pa kukbaliana na Biblia pale mwanzo watu walizaana watu wa karibu na bado uzao wao ukawa imara.Leo fanya hivyo katik boma kama ifugo haikujatoweka ghafla.Au binadamu kuwa na uzao mkubwa ila wabakio kuwa wachache.Kwa bongo watu wamezoea kuona nyumba nyingi za waasia zina vilema au watoto wenye mangilio mbaya sana wa meno na udhaifu mwingine, na kuhusisha na ushirikina ila malezo mazuri zaidi ni uzao wa ndugu wa karibu.
kuna mangi sana yanayoendelea kwa nia njema na mbaya katik vita ya kutaka muondoa Mungu katika jamii zetu.Ila wengi wa wanasayansi wanongozwa kwa hela za wabudu mashetani kupitia mgongo wa Kutoamini uwepo wa Roho/Mungu.Ila pia mashindano ya dini ili kuthibitisha nyingine si sahihi katik izazi cha dot.com.Ndio maana makanisa ya kimarekani maprofessor wao wameafanya kazi kubwa kukimbizana na sayansi, pamoja na kanisa katoliki wana observatory yao kubwa sana,inayowafanya wawe sawa na sayansi au mbele.Ndio maana wana majibu kwa maswali kama ikiwa patagundulik viumbe wengine km binadamu ,je nao watahitaji ukombozi wa Yesu , na kwani ni?Ambalo ni kuwa Yesu hatohitajika kule kama mkombozi, ila kwa nafasi ingine iwahusuyo wao.Sababu ni kwmaba wao si uzao wa Adamu ambaye aliwarithisha dhambi ya asili.Ni rahisi ona dhambi ya asili kwa matukio ya karibu tuu kwani mara nyingi watoto hurudia makosa ya wazazi(baba) wao ambayo huwaangusha hata kama hawakulelewa wala kujuana nao.haya makosa si alazima yawe na effect sawa ila za kushabihiana.
Kwa hiyo unashauli nini kwa wanadamu?