manchoso,acha usanii wa dr Zakir Naik bana.Achana na mawazo ya watu angalia maandiko.Mjadala uliouanzisha japokua unatutoa kwenye mada nitakusaidia kidogo:Uungu wa Yesu umeanzia agano la kale,lakini nitakupa mistari michache kutoka agano jipya.Pia namna Yesu alivyoitwa Mungu ni tofauti na Musa na baadhi ya mifano uliyotoa,hilo tuliache.Kwenye ufu 1:8 kuna kauli ina sema,"Mimi ni alfa na omega asema Bwana Mungu,aliyeko na aliyekuwako na atakaekuja,Mwenyezi".Kama unataka kumjua huyo aliyesemwa hapo ni nani,jiulize ni nani alisema atakuja?Pia ufu 21:7,Yesu anasema,"Yeye ashindae atayarithi haya,nami nitakua Mungu kwake nae atakua mwanangu".Unadhani Musa au kuna mtume yoyote unaemjua wewe aliyewahi kutoa kauli hii?Thubutu!!!Pia ufu 22:16 anasema,"Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia mambo hayo katika makanisa.Mimi niliye shina na mzao wa Daudi,ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi".Hivi unadhani ni mwanadamu gani anaweza kusema "nimemtuma malaika WANGU"?Sote tunajua malaika ni wa Mungu kwa sababu amewaumba,tangu Adam mpaka leo hakuna mwanadamu alidai ana malaika,Yesu hakuwa mwanadamu bali Mungu,na yeye ndie aliyewaumba malaika na vyote Yoh 1:3.Asingesema hayo kama angekuwa mwanadamu!