Mwanadamu wa kale alioka mikate kabla ya kuanza kilimo

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Kikundi cha wanaakiolojia kimesema wamegundua kwamba binadamu walianza kuoka mikate mapema zaidi kabla ya kuanza shughuli za kilimo.

Utafiti uliotolewa kwenye Jarida la PNAS la Marekani unaonesha kuwa wanaakiolojia wamegundua mabaki ya mikate ya kuokwa yenye historia ya miaka 14,400 katika makazi ya kale ya binadamu kaskazini mashariki mwa Jordan

Watafiti kutoka wamegundua kuwa binadamu wa kale walisaga, kuchuja, kukanga na kupika nafaka pori, zikiwemo shayiri na ngano

Wamesema kuoka mikate kwa nafaka pori kuliwahimiza binadamu wa kale kuanza kulima nafaka, na kuleta mapinduzi ya kilimo katika enzi ya zama za mwisho za mawe.
 
Hili hata ukitumia ''ubongo'' bila utafiti wa kisayansi unaweza kuona logic yake. Mtu hawezi kuanza kilimo kabla hajajua manufaa ya kilimo. Hivyo hivyo kwenye ufugaji... Uwindaji ndiyo ulizaa ufugaji. Kwa mfano mtu anakwenda kuwinda kitoweo kinamnogea anafikiri... hivi nikipata ndege wengi kwa nini nisile wachache na wengine niwatengenezee tundu ili kila napotaka kula nisihangaike kwenda kuwinda?
 
..Africa huenda hayo yalikuwa yanafanyika miaka 400,000 iliyopita; maana mtu wa kale zaidi inasemekana aliishi East Africa miaka 2.4 milioni hadi 1.4 milioni iliyopita. Na ustaarabu, kilimo, sayansi, demokrasia, nk vilianzia Africa.

Sema hata wapate ushahidi mkubwa kiasi gani, ni vigumu wazungu kuuweka hadharani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikundi cha wanaakiolojia kimesema wamegundua kwamba binadamu walianza kuoka mikate mapema zaidi kabla ya kuanza shughuli za kilimo.

Utafiti uliotolewa kwenye Jarida la PNAS la Marekani unaonesha kuwa wanaakiolojia wamegundua mabaki ya mikate ya kuokwa yenye historia ya miaka 14,400 katika makazi ya kale ya binadamu kaskazini mashariki mwa Jordan

Watafiti kutoka wamegundua kuwa binadamu wa kale walisaga, kuchuja, kukanga na kupika nafaka pori, zikiwemo shayiri na ngano

Wamesema kuoka mikate kwa nafaka pori kuliwahimiza binadamu wa kale kuanza kulima nafaka, na kuleta mapinduzi ya kilimo katika enzi ya zama za mwisho za mawe.
Usiseme binadamu wa kale sema warabu wa kale.Afrika hakukuwa na ngano, imeletwa juzi tuu.Waafrika wa kale walikula wanyama, matunda na asali za porini
 
Waafrika was kale walikuwa wawindaji na waokotaji wa matunda! Mambo ya ngano sijui Kama afrika yalikuwepo ...maana hata mahindi yaliletwa toka nje ya afrika
 
Watu wanapenda mikate mikateee
watu wanapenda mikate mikateeee
Ukienda Zama za mawe za kale mikateee
Zinjathropus Mixer Homo eractus wailipenda nini mikateee 🍞
 
Hili hata ukitumia ''ubongo'' bila utafiti wa kisayansi unaweza kuona logic yake. Mtu hawezi kuanza kilimo kabla hajajua manufaa ya kilimo. Hivyo hivyo kwenye ufugaji... Uwindaji ndiyo ulizaa ufugaji. Kwa mfano mtu anakwenda kuwinda kitoweo kinamnogea anafikiri... hivi nikipata ndege wengi kwa nini nisile wachache na wengine niwatengenezee tundu ili kila napotaka kula nisihangaike kwenda kuwinda?

Unaposema "..hawezi kuanza kilimo kabla hajajua manufaa ya killimo" sio sahihi sana kwa sabab kuna sabab zilizolamisha binadam kulima ila sio kwa sabab labda alikuta anaoka mikate.... Mfano mwa kufuga umeuzungmzia katka mtazamo sawa ila kilimo kilianza kwanza ujue kilianza km ndondokela(by chance) ila mabadiliko ya kimazingira na taabu za utegemezi kutoka kwene mazingira kuzid ndipo binadam akawaza namna gan angeweza jikwamua na taabu hio.... Baada ya kuona kwamba kuna mimea inaweza pandwa na kuzaa ndipo akaanza kazi ya upanzi wa mazao-pori ilikua na chakula cha kujikimu.

Issue kubwa wana akiolojia hao wametufumbua macho kwamba kuoka mikate kulianza miaka karibu 4000+ kabla kuanza kwa kilimo. Nasubir tafit nyingne zaidi juu ya hili.
 
Kama walikua hawalimi walioka nini sasa ,maana umesema kabla ya kilimo 😂😅😅😂😅😅😅😅🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶,chai imejaa majani
 
Jifunze kuwa unasoma mpaka mwisho mkuu kabla ya kukomenti..

Waliokota grains ambazo hawakupanda wao (zinazojiotesha mapolini) baadae ndio wakaanza kulima wenyewe
 
Sio kweli.
Binadamu wa kale chakula chake ni matunda, mboga za majani na asali.
 
Back
Top Bottom