Mwanafunzi alivyosababisha Vita Kuu ya kwanza ya Dunia

Mwanafunzi alivyosababisha Vita Kuu ya kwanza ya Dunia

VITA Kuu ya Kwanza ya Dunia (WWI), ilianzia na kuhusisha mataifa ya Ulaya lakini ikasambaa ulimwenguni kote.

Vita hii ilianza Julai 28, 1914 na kufikia tamati Novemba 11, 1918. Tangu kuanza kwa vita hiyo hadi kuibuka tena kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1939, ilikuwa inafahamika tu kama Vita Kuu. Zaidi ya wanajeshi milioni 9 waliuawa. Huo ulikuwa mgogoro wa tano mkubwa zaidi katika historia ya dunia, na kufungua mlango wa mabadiliko makubwa ya kisiasa, yakiwemo mapinduzi katika mataifa mengi yaliyohusika.

Vita hivi vilihusisha mataifa yote yaliyokuwa na nguvu za kiuchumi duniani, ambayo yalikuwa katika pande mbili zinazopingana kulingana na uchumi wao: Majeshi ya Washirika (yaliyotokana na Mkutano wa Utatu wa Uingereza, Ufaransa na Dola ya Russia) na Majeshi ya Kati (Central Powers) yaliyoundwa na Ujerumani na Austria-Hungaria. Ingawa Italia ilikuwa mjumbe wa Muungano wa Majeshi ya Kati pamoja na Ujerumani na Austria-Hungaria, haikuweza kuungana nayo kwani Austria-Hungaria ilikuwa imekiuka masharti ya umoja huo.

Majeshi hayo ya pande mbili yalikuwa yameundwa na kutanuka kadiri mataifa mengi yalivyoingia kwenye vita hivyo: Italia, Japan na Marekani wakajiunga na Majeshi ya Washirika (Allies), na Dola ya Ottoman na Bulgaria wakajiunga na Majeshi ya Kati. Maofisa milioni 70 wa kijeshi, wakiwemo milioni 60 kutoka Ulaya, wakajipanga katika mojawapo ya vita vikubwa kabisa katika historia ya dunia.

KUUAWA KWA MFALME FRANZ FERDINAND

Daraja mjini Sarajevo ambapo Mfalme Ferdinand na mkewe Sophie waliuawa Juni 28, 1914.

Japokuwa kuibuka kwa ubepari kulikuwa sababu ya msingi ya vita hivyo, lakini chanzo kikubwa kilikuwa ni tukio la Juni 28, 1914 la kuuawa kwa Archiduke Franz Ferdinand wa Austria, mrithi wa taji la ufalme la Austira-Hungaria. Ferdinand aliuawa mjini Sarajevo, Yugoslavia na manafunzi mwanaharakati Gavrilo Princip.

Hii ilileta mgogoro wa kidiplomasia wakati Austria-Hungaria ilipopeleka sharti (ultimatum) kwa Ufalme wa Serbia, na umoja wa kimataifa uliokuwa umeundwa miongo kadhaa nyuma ukavunjika. Ndani ya wiki chache tu, mataifa makubwa yalikuwa vitani na mgogoro ukasambaa haraka dunia nzima.

Mnamo Juni 28, 1914, Mfalme Mkuu Franz Ferdinand wa Austria, ambaye alikuwa ndiye mrithi wa taji la ufalme la Austro-Hungaria, na mkewe Sophie, Duchess wa Hohenberg, waliuawa mjini Sarajevo na Gavrilo Princip, mmoja wa kundi la wauaji sita (watano Waserbia na mmoja Mwislamu wa Bosnia), mauaji yaliyoratibiwa na Danilo Ilic.

Madhumuni ya kisiasa ya mauaji hayo yalikuwa kuyavunja majimbo ya Slavia ya kusini katika himaya ya Austro-Hungaria ili yaungane na Serbia Kuu au Yugoslavia. Maofisa wa kijeshi wa Serbia walikuwa nyuma ya mauaji hayo yaliyoendeshwa katika harakati za Young Bosnia.

Mauaji hayo yalisababisha Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia wakati Austira-Hungaria ilipotoa sharti la mwisho dhidi ya Serbia, ambalo lilikataliwa. Austria-Hungaria ikatangaza vita, na ndipo vita hasa ilipoibuka.

Kati ya maofisa wa jeshi la Serbia waliokuwa nyuma ya mpango huo walikuwemo Mkuu wa Ujasusi wa Kijeshi wa Serbia Dragutin Dimitrivajec, msaidizi wake wa karibu Meja Vojislav Tankosic, na Jasusi mkuu Rade Malobabić. Meja Tankosić aliwapatia wauaji mabomu na bastola na kuwapa mafunzo. Wauaji hao walipewa fursa kuingia katika mtandao maalum na kutumia nyumba za siri na mawakala wa usalama ambao Rade Malobabić aliwatumia wakati akipenyeza silaha na shughuli zake ndani ya Austria-Hungaria.

Wauaji hao, wafuasi wa mtandao ya kijasusi, na maofisa wa jeshi la Serbia waliohusika ambao walikuwa hai bado, walikamatwa, wakashtakiwa, wakakutwa na makosa na kudhibiwa. Waliokamatwa Bosnia walishtakiwa Sarajevu Oktoba 1914. Wengine walishtakiwa kwenye mahakama ya kangaroo ya Kiserbia katika eneo la Salonika Front lililokuwa linamilikiwa na Ufaransa kati ya mwaka 1916-1917 kwa mashtaka ya uongo yalisiyohusiana na mauaji hayo; Serbia iliwanyonga maofisa watatu wa jeshi.

Movie mpya wema Uko wapi?
 
Planet.

Acha roho ya kwanini kwanini? Mbona ikiandikwa gari limepata ajali na waliokufa ni watu sita na mmasai mmoja hulalamikagi... Au mmasai c ntuuu? Acha hizo. Guud history. me mwenyewe nilikua sijui kama chanzo cha vita ni mwanafunzi.
 
Planet.

Acha roho ya kwanini kwanini? Mbona ikiandikwa gari limepata ajali na waliokufa ni watu sita na mmasai mmoja hulalamikagi... Au mmasai c ntuuu? Acha hizo. Guud history. me mwenyewe nilikua sijui kama chanzo cha vita ni mwanafunzi.

Mkuu, watu wa ainahiyo tuponao wengi hapa jf. Kubwa huwa tunawapotezea tu, then maisha yanaendelea
 
ushiboy; Asante sana kwa kipande hiki ingawa sijui umekitoa wapi. Mimi siyo mwanahistoria ila ninapenda sana historia nikiwa mtu wa kwanza kupigania jukwaa hili kuundwa hapa JF. Nimeifurahia sana article yako hii
 
Last edited by a moderator:
ushiboy; Asante sana kwa kipande hiki ingawa sijui umekitoa wapi. Mimi siyo mwanahistoria ila ninapenda sana historia nikiwa mtu wa kwanza kupigania jukwaa hili kuundwa hapa JF. Nimeifurahia sana article yako hii

Na wavunja mioyo pia wapo Kichuguu, sababu watu wa kuvunja moyo kutafuta makosa tu. Na chakushangaza watu wa aina hiyo badala ya kufanya marekebisho ili tusonge, basi wao kufanya kejeli na dhihaka.
Anyway, kubwa hapa jf ni kuvumiliana ili tusonge.
Asante sana Kichuguu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom