Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

kisingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2014
Posts
516
Reaction score
377
Walimu 6 wa Jangwani Sekondari jijini Dar es salaam wamemhukumu kwa kumchapa makalioni fimbo 20 mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu na kumjeruhi vibaya kwa tuhuma za kuwa alionekana ameshika simu.

Mwalimu aliyesema hivyo alimvua nguo na kumpekua kila mahala na hakukuta simu. Alimchukua hadi ofisi ya walimu na kumlazimisha akiri lakini alikataa ndipo walimu 6 wakamshushia kipigo cha fimbo 20.

Mmoja alimchapa 5 wawili 4 kila mmoja, mmoja 3 na wawili 2 kila mmoja. Wapo walimu wa kiume na wa kike waliofanya kipigo hiki. Alipoona kipigo kina zidi aliropoka kuwa yeye hana simu bali aliye na simu ni mwenzake.

Huyo aliyetajwa kachukuliwa hatua japo mzazi alikuja kukiri binti yake kuwahi kuwa na simu.

Huyu binti aliyechapwa alihamishiwa shuleni hapo na kuishi bweni akitokea mkoani kutokana na tatizo la kiafya. Hali hiyo bado ilikuwa inamsumbua na zipo kumbukumbu katika hospitali za Dar na huko alikotoka lakini baadhi ya walimu wanasema anajifanyisha hivyo kushindikiza atolewe bweni azma ambayo wameipitisha pamoja na hicho kipigo.

Tatizo jingine ni imani kwa kuwa jitihadi za kumbadili kupitia ugonjwa zilipo shindikana wanasema haumwi.

Wapo wanafunzi walibadilishwa na kwenda upande wa hao walimu.

Tunaomba TAMISEMI, Polisi na Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto wafuatilie suala hili. Huyu binti ni mgonjwa sasa akiwa mwanafunzi wa kutwa akipata tatizo njiani nani wa kuwajibika.

Mtoto wa kike anadhalilishwa fimbo 20 shule tena kwenye makalio.

Tupaze sauti.
 
Huna akili wewe.
Nyie ndio mnalea ujinga kwa watoto
Tupoteze muda kwa swala la malezi mabovu kwa mtoto wako. Kwanza hao walimu wangeongeza idadi zifike fimbo 100 kwa tako moja.
Ameenda kusoma au kuchati na kupiga picha walimu..
Ficha ujinga wako mkuu
 
Kuna adhabu za kuwapa watoto na sio mabakora. Ndio maana tunaonekana manyani meusi yasiyo na akili.
Mpe jembe akalime/afyeke/asafishe vyoo vya shule/apige magoti aite mvua mpaka wenzake wakitoka darasani/apewe suspension/alazimishwe asome vitabu kadhaa na aviandikie muhtasar la sivyo anafukuzwa shule n.k nk. mpe adhabu za kumjenga na sio kudhalilisha utu wake.
 
Back
Top Bottom