Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Nikiwa kidato cha pili, niliwahi tembezewa stick 47 (Arobaini na saba) hadi nikazima maksudi staff. Reasons ni hizi.

1. Wizi wa attendance register uliokithiri.
2. Kutongoza Waalimu wa kike. (Wote walikua wanachomoa 😂
3. Wizi wa viazi, mahindi ya kuchoma, karanga mashambani kwa walimu.
4. Kwenda shule nimelewa na kuvuta sigara.
5. Utoro sugu.

Ila Mungu alivyo, nina Bachelor's Degree ya Education. Hatari.
 
Mbona uko upande wa mwanafunzi zaidi?
Kila kinachosemwa na walimu wake wewe unasema ni uongo kwani wewe ni nani yake??
Hadi wanafunzi waliotoa ushahidi unasema wamelazimishwa na walimu, we umejuaje? hao wanafunzi si ndio wanakaa muda mrefu na huyo mwanafunzi!?

Mboko 20 chache sana, hizo simu zinaharibu sana mabinti, tena zinawapa viburi zaidi. Huko kwenye simu wanavimbishwa mabichwa na viboyfriend uchwara wamlambe bakora zaidi mpaka aseme ni nani huwa anawasiliana nae humo simuni.
 
Kosa lake ni kuleta Mada ambayo haikupaswa kuletwa humu,Alitakiwa akusanye zawadi na kuwapelekea hao walimu.This Is the home of Great thinkers not otherwise
Mimi sikubaliani na adhabu ya fimbo kama ndio njia ya kutatua tatizo,mbona international school hawana huo ukiritimba na wanafanya poa zaidi ya wanaochapwa viboko 20+
 
Mkuu Wewe ni nani, tuone taarifa uliyotoa ipo sahihi kiasi gani, kwamba huyo mtoto kipindi anaadhibiwa ulikuwepo?

Umejuaje kwamba walimu walisema mtoto haumwi bali anajifanyisha tu?

Habari imekaa kiukandamizaji zaidi kwa walimu labda ungekua mwandishi ambae amehoji pande zote mbili ungebalance stori yako.

Yote kwa yote wote wafate sheria wanafunzi kwa walimu.
 
Mbona uko upande wa mwanafunzi zaidi?
Kila kinachosemwa na walimu wake wewe unasema ni uongo kwani wewe ni nani yake??
Hadi wanafunzi waliotoa ushahidi unasema wamelazimishwa na walimu, we umejuaje? hao wanafunzi si ndio wanakaa muda mrefu na huyo mwanafunzi!?

Mboko 20 chache sana, hizo simu zinaharibu sana mabinti, tena zinawapa viburi zaidi. Huko kwenye simu wanavimbishwa mabichwa na viboyfriend uchwara wamlambe bakora zaidi mpaka aseme ni nani huwa anawasiliana nae humo simuni.
Mkuu umenena vyema sana. Alafu ubaya zaidi kwa wanafunzi simu moja inaweza kutumika kuharibu mabinti zaidi ya mmja sababu huwa wanashare. Simu sio nzuri hasa kwa watoto wetu hawa wakiafrika wengi malimbukeni.
 
Ona sasa baada ya kuchapwa ndio anawataja wenzake wenye simu. Maana yake na yeye alikuwa anatumia simu. Kama wewe ni mzazi utakuwa na malezi mabaya na kama ni mwalimu una roho ya chuki kwa walimu wenzako na huenda unataka madaraka. Kesi hiyo umeshindwa kuwasiliana na mwalimu wa nidhamu, mkuu msaidizi, mkuu je? Acha chuki zako uza hata barafu kama maisha ni magumu unategemea mwenzako aanguke upewe madaraka.
 
Unadhani walimu wanafaidika nini kumuadhibu mwanafunzi mwenye makosa? Kuna shule ambazo walimu wameuamua kuendelea na shughuli zao na kuwaacha wanafunzi wafanye wanavyotaka sababu ya watu kama mleta mada. Wanafunzi wa kizazi hiki ukisema uwape azabu ya kufanya shughuli za nje ndio furaha kwao maana ndio wanachopenda, watafanya hata wiki nzima bila shida yoyote.
 
Nikiwa primary darasa la nne niliwahi chezea stick zaidi ya 40 kutoka kwa mwalimu mmoja hivi bonge anaitwa Sylvia. Kisa nilikuwa napiga safa sana (natoka home ila shule sifiki).

Siku hiyo nikaja kimbizwa na wanafunzi wenzangu ambao walikuwa ndio wenye mbio shuleni wakanidaka. Tulikuwa karibu na home kwa chaliangu tunaepiga nae safa yeye aliwahi kushika panga wakaogopa kumdaka mimi nikabebwa juu juu nikaenda kuchezea stick shazi.
 
Mkuu umenena vyema sana. Alafu ubaya zaidi kwa wanafunzi simu moja inaweza kutumika kuharibu mabinti zaidi ya mmja sababu huwa wanashare. Simu sio nzuri hasa kwa watoto wetu hawa wakiafrika wengi malimbukeni.
Kabisa mkuu, kama unalea mtoto wa kike alie sekondari ndio unaweza elewa ubaya wa simu kwa hawa mabinti.
 
Kuna adhabu za kuwapa watoto na sio mabakora. Ndio maana tunaonekana manyani meusi yasiyo na akili.
Mpe jembe akalime/afyeke/asafishe vyoo vya shule/apige magoti aite mvua mpaka wenzake wakitoka darasani/apewe suspension/alazimishwe asome vitabu kadhaa na aviandikie muhtasar la sivyo anafukuzwa shule n.k nk. mpe adhabu za kumjenga na sio kudhalilisha utu wake.
Wewe unawafahamu vizuri watoto wa shule. Mtoto anaishi mjini nyumbani hakuna shamba wala bustani unadhani ataweza kulima shuleni? Kama ataweza lawama za walimu kuwatesa watoto muda wa masomo ndio itakuwa habari ya mwanzo gazetini. Pia watoto wengi wanapenda kazi za nje ama wanasaidiana mwalimu akiondoka. Yaani unataka kumpa mwalimu ahakikishe amemaliza adhabu mwanafunzi bila kusaidiwa? Walimu wana mambo mengi ya kufanya. Adhabu inatakiwa kutolewa wakati tendo linafanyika na sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom