Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wa mkoaWaliahidi wazazi, shule au Polisi?
Kwa Jimmy ifuatiliwe isiachwe ipiteWamesha mchafua Mwl jimmy kwa ujinga wa huyo mtoto
Mwalimu Jimmy pole sana mwalimu mwenzangu.Ukipata nafasi nitafute nikwambie kitu utanikumbuka the rest of your life brother.Inabidi watu wamuombe msamaha Mwalimu Jimmy, mtu anacheza dudu la yuyu huko anasumbua mpaka waziri.
ApeweHuyo Binti aliyemgundua apewe milion 5 zake.
Mtoto mpuuzi tu yule.tena ndo akagegedwe hukoKwa hiyo wanafunzi waibie mtihani wasichapwe fimbo 3 kwa sababu watakimbilia kwa wanaume? Hivi walimu wa Tanzania waliwakosea nini?
ewe jamaa acha kujifanya kichwa ngumu, huyo alikua lazim apatikane kwasbb saut ilipazw. Wakaona ohoo yasiwe makubwa ngoja t arudi, lkn kiufup huyo alikua tyr ashaolewa. Ayo mengin unajiongez t kakaHatimaye Ester Noah Mwanyiru mwanafunzi wa sekondari ya Pandahill aliyetoweka 18 May 2023 amepatikana.
Taarifa iliyotolewa na mama yake mzazi inaeleza amepatikana wilayani Mbalizi kwa mama fundi cherehani. Alibadili jina kuwa Erica na amekua akivaa Hijab inayofunika uso, na kuacha macho tu na hivyo kuwa ngumu kutambulika.
Chanzo cha kupatikana ni baada ya binti mmoja wa Mbalizi kusimuliwa kisa cha Ester na kudai amemuona kwa mama mmoja fundi cherehani. Leo asubuhi polisi wamevamia nyumba ya mama huyo na kumkuta Ester. Wote wawili wapo kituo cha Polisi Mbalizi kutoa maelezo.
-----
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema Mwanafunzi Esther Noah, aliyepotea tarehe 17 Mei 2023 (Siku 37) katika Sekondari ya Panda Hill, Mbeya amekutwa katika maeneo ya Ifisi, Mbeya alikuwa kwa mtu aliyefahamika kwa jina Moja la Baba Jose.
Mtu huyo baada ya kukaa na Mwanafunzi huyo kwa muda alikwenda kumuweka kwa mama mmoja na kuahidi kwenda kumchukua siku atayapata chumba Ili wakaendelee kuishi pamoja. Mama huyo alipobanwa na Jeshi la Polisi alisema kuwa Mwanafunzi huyo aliletwa na Baba Jose ambaye huwa anamletea magunia ya mkaa kuuzwa pale gengeni takriban wiki mbili, na alimwambia yule ni mke wake na ametoka naye Morogoro, hivyo anaomba amuache hapo mpaka atakapopata chumba cha kupanga ili aje amchukue mkewe. Mwanamke huyo alichukua jukumu la kumhoji mwanafunzi huyo, na aliambiwa kuwa anaitwa Erica na ametoka mkoani Morogoro.
BABA JOSE ANASAKWA NA JESHI LA POLISI
RC Mbeya, Juma Homera amesema jeshi la Polisi liko makini na litahakikisha linamkamata baba Jose anayedaiwa kumtorosha Mwanafunzi Esther Noah, Sekondari ya Panda Hill, Mbeya aliyepotea tarehe 17 Mei 2023 (Siku 37) na kumfikisha kwenye mikono ya sheria.
APIMWA MIMBA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema wamempima Esther Noah kipimo cha mimba Ili kujua hali yake na majibu yameonyesha hana mimba.
Na kwa siku zijazo ikionyesha ana mimba watampa nafasi ya kwenda kujifungia na kurudi shule.
#MyTake:
Simulizi ya kupotea kwa Ester na kupatikana kwake inaacha maswali mengi kuliko majibu.
1. Ester alitoroka shuleni baada ya kukutwa akifanya udanganyifu kwenye mtihani. Akachapwa viboko vitatu, kisha akapewa mtihani mwingine afanye. Lakini polisi walipoenda shuleni hakukua na mtihani wowote Ester aliofanya. Je mitihani yake ilienda wapi?
2. Shule ya Pandahill ina ukuta (fence) ya urefu wamita 3 na juu kuna nyaya za umeme. Inawezekanaje mtoto wa kike kuruka ukuta wa mita 3 wenye umeme?
3. Matron wa shule anasema Ester alitoroka na mwenzie mmoja na walikimbizwa hawakupatikana. Hata hivyo "rall call" ilipofanyika wanafunzi wote walikuwepo isipokua Ester tu. Je huyo aliyekimbia na Ester akiwa kwenye sare za shule ni nani?
4. Barua aliyoacha Ester alidai kuonewa na Mwalimu Jimmy, japo hakutaja uonevu huo. Kwanini hakwenda nyumbani kuwaeleza wazazi badala ya kukimbilia Mbalizi?
5. Kwanini Headmaster alienda kwa wazazi wa Ester kutoa pole?
6. Huyo mama wa Mbalizi aliwezaje kumpokea binti asiyemfahamu na kukaa nae comfortably?
7. Aliishi kwa huyo mama kama nani? Housegirl au?
8. Inaelezwa alienda kwa huyo mama na Hijab. Aliipata wapi? Sare za shule alizototoka nazo aliziacha wapi?
9. Alibadili jina kuwa Erica lakini akavaa Hijab. Huyo mama hakujiuliza iweje mtoto wa Kikristo kuvaa Hijab?
10. Binti aliyetoa taarifa kuwa amemuona Ester Mbalizi alimtambuaje ikiwa alivaa Hijab ya kufunika uso na kubakiza macho tu?
NB: Tunamshukuru Mungu Ester amepatikana akiwa mzima, lakini kwa kuwa suala hili limepaziwa sauti na umma, basi ni vema umma ukapewa majibu ya kuridhisha.!
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Angeendelea kuikalia hata week alafu bwana akee akamtupee mashambani hukoooKwamba ulitaka aonekane kwa mbinde? Au mimi sijakuelewa?
Baba Jose fundii sanaaa.. ila ataenda kula jeuri yake nyuma ya nondoo 😅😅Haya
Yanii achaa asilaumiweee Wanawake wanateswa na kupigwa kwenye ndoa zao hawaondokiii... itakuwa shuleee tena PCB ilivyokuwa ngumu[emoji28]Ila lakini Ester asilaumiwe maana dushe ni tamu et
Ndo huyo baba Jose 🤣🤣Duh mbona niki click inaleta Mzabzab aisee,
Sosho midia maza fakaSocial media saivi ndio inaongoza viongozi...
MPENI NAFASI ARUDI SHULE MENGINE NI MBWEMBWE TU.ATAFUTIWE SHULE PENGINE#UPDATES Mwanafunzi Ester Noah Mwanyilu, amepatikana katika chumba cha kupanga cha Mama Abdul kilichopo maeneo ya Ifisi Mbalizi, na kwamba alipelekwa hapo na muuza mkaa aitwaye Baba Jose na kusema ni mke wake hivyo anaomba hifadhi baada ya siku mbili angemchukua ili wakaishi wote.
Aidha vipimo vyote vya kiafya vimefanyika na Ester hana ujauzito na hivyo ataendelea kukaa na maafisa ustawi wa jamii ili kumsaidia kumpa ushauri wa kisaikolojia arudi shule, na mwanaume huyo atasakwa mpaka akamatwe.
RC Homera ametoa rai kwa walimu wa Pandahill kupunguza kasi ya kuchapa viboko.
#MwanafunziApatikana
#EastAfricaTV
Duh mbona niki click inaleta Mzabzab aisee,