Mwanafunzi kidato cha nne auwawa kwa kipigo shuleni mkoani Iringa

Mwanafunzi kidato cha nne auwawa kwa kipigo shuleni mkoani Iringa

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
1,821
Reaction score
3,980
Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bukimau iliyopo Kata ya Bumilayinga, Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi, Kojak Emily Ungele (19), amefariki dunia katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia Jumatatu, Juni 1, 2026, baada ya kile kinachodaiwa kuwa kushambuliwa akiwa katika mazingira ya shule na chini ya uangalizi wa walimu na walezi wa shule hiyo.

Credit: BBC SWAHILI FACEBOOK PAGE

1000073813.jpg
=======

Mama Mzazi wa mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bukimau iliyopo Kata ya Bumilayinga,Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,Kojak Emily Ungele (19) amefariki dunia mnamo Juni 1, 2026 baada ya kushambuliwa akiwa katika mazingira ya shule na chini ya uangalizi wa walimu na walezi wa shule hiyo.Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na tuhuma za wizi wa mashine ya kunyolea nywele pamoja na redio.

Baada ya tukio hilo, mwanafunzi huyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Nyororo kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa kutoka kituoni hapo, kijana huyo alikuwa tayari ameshafariki dunia kabla ya kufikishwa katika kituo hicho cha afya.Aidha Jeshi La Polisi linawashikiria watuhumiwa wa Mauaji hayo akiwemo Mwalimu Mlezi (Patron) na Watuhumiwa Wengine ambao inadaiwa ni Wanafunzi waliohusika Na Mauaji Hayo.


Baba Mzazi wa Marehemu

PATRONI HAKUPOKEA SIMU ZETU,bMWILI ULIKUTWA UMEVUJA DAMU NYINGI - Anaitwa Emily Ungele ambaye ni Baba Mzazi wa mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bukimau iliyopo Kata ya Bumilayinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Kojak Emily Ungele (19) amefariki dunia mnamo Juni 1, 2026 baada ya kushambuliwa akiwa katika mazingira ya shule na chini ya uangalizi wa walimu na walezi wa shule hiyo.Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na tuhuma za wizi wa mashine ya kunyolea nywele pamoja na redio.

Baada ya tukio hilo, mwanafunzi huyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Nyororo kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa kutoka kituoni hapo, kijana huyo alikuwa tayari ameshafariki dunia kabla ya kufikishwa katika kituo hicho cha afya.Aidha Jeshi La Polisi linawashikiria watuhumiwa wa Mauaji hayo akiwemo Mwalimu Mlezi (Patron) na Watuhumiwa Wengine ambao inadaiwa ni Wanafunzi waliohusika na Mauaji hayo.

 
Hawa waalimu inabidi wawe wanaangaliwa kama wana ubinadamu kabla ya kuajiriwa.Majitu mengine in nature yana roho mbaya.Watu wanaodili na watoto wasiangaliwe vyeti tu.
 
Back
Top Bottom