TANZIA Mwanafunzi SAUT afariki akiwa ameenda kuogelea ziwani

TANZIA Mwanafunzi SAUT afariki akiwa ameenda kuogelea ziwani

Unauliza maswali ya hovyo sana
Kwanza, mimi sijauliza maswali wewe poyoyo. Nimeuliza swali moja tu.

Pili, hilo swali si la hovyo. Bali wewe ndiye mpuuzi ukashindwa kuelewa mantiki ya swali langu.

Ajali humpata mtu popote. Na hakwenda pale kwa nia ya kufa. Alienda kufurahia, isivyo bahati akapoteza maisha.

Hakuna mtu afuataye ajali ama kifo. Bali humkuta tu pasipo kutaraji.
 
Ni bora msumeno ufyatuke na kunikata shingo kuliko mimi kupeleka shingo yangu kwenye msumeno ili unikate.
 
Naogopa sana maji.

Pole nyingi kwa wafiwa, inauma kupoteza kijana mdogo.
 
Alishindwa kutulia hostel au ghetto kwake? Hao wenzake walishindwa vipi kumuokoa akiwa anapigania uhai wake?

Mambo mengine mbona yanaepukika kabisa!! Polee kwa wafiwa.

Rip dear!! [emoji24][emoji24][emoji24]
Ajali kazini tu bibie 😀
Alafu ziwa liko kama beseni maji yapo ugokoni hatua mbili mbele ni 500m kwenda chini kwahiyo unatakiwa ujue kuogelea kweli
 
Mwanafunzi Wa Chuo kikuu Cha SAUT Campus ya Mwanza Amefariki Dunia Alipokuwa Ameenda kuogolea Kando Kando Kando ya Ziwa Victoria Maeneo ya Sweya Beach.

Taarifa hiyo ilitolewa Na Wenzake Ambao walikuwa wameenda Nao kuogolea katika Maeneo hayo ya Kando kando ya Ziwa Na Na Kifo hicho kimetokea Jana Siku ya Mei Mosi Ambako Wanafunzi walikuwa Hawana vipindi Madarasani.

Mwanafunzi Aliyefariki Anasoma Shahada ya Kwanza katika Fani ya Ualimu Kwa Mwaka wa Kwanza (BAED 01)

Katika Hatua Nyingine Mwili wake Ulitolewa Ziwani Leo Na Jeshi La Uokoaji Kanda Ya Mwanza Mara Baada ya Jana Kuzama na Kushindwa kupatikana kutoka Na sababu Zilikuwa kuwa Nje ya Uwezo.

Baadhi ya Wakazi katika Maeneo ya Sweya Wanasema Kuwa Imekuwa Ni Desturi kwa Wanafunzi wanao Soma SAUT kuja Kuogelea Katoka Hayo Maeneo kipindi wawapo masomoni Wakirejelea Kipindi Cha Mapumziko Ama Siku za Mwisho wa juma (Week end) huwa kuna Idadi kubwa ya Wanafunzi.

Vile vile Wanasema Wanafunzi wengi hupendelea kuja Kupiga Picha Na Kukaa Nyakati za Jioni

Chanzo:Taarifa Na ME
Jinsia gani huyo marehemu habari nusu nusu!
 
Katika Hatua Nyingine Mwili wake Ulitolewa Ziwani Leo Na Jeshi La Uokoaji Kanda Ya Mwanza Mara Baada ya Jana Kuzama na Kushindwa kupatikana kutoka Na sababu Zilikuwa kuwa Nje ya Uwezo.
Usishangae wakikwambia walikwenda kutafuta pump ya kupunguza maji
 
Dah asee pole sana kwa wafiwa,, jamaa ameondoka ameacha chuo cha hovyo kupitiliza Tz yan nashangaa sana kusikia SAUT bado kuna first Year chuo hakifai hata kidogo.
 
Hakika uchunguzi ufanyike, hao wenzake wabanwe waeleze ukweli.
Siwezi fahamu ilikuwaje lkn kwa uzoefu wangu kuhusu kuogelea ni vyema ukawa unafahama historia ya eneo husika,mazingira yake hasa uwepo wa tope na mapango.

Huenda ukazama chini na ukanasa pangoni au topeni na hasa maji yakiwa hayajatulia (machafu) kiasi cha kutokukuwezesha kuona mbali pindi uzamiapo.

Lkn kuna ile ghafla huko eneo lenye kina kirefu bila kutarajia sasa ile kupima urefu wa kina cha maji kama siyo mzoefu wa kuogelea hupelekea kukosa msawazo (balance) na hivyo maji kukupeleka yatakako.
 
Ajali kazini tu bibie [emoji3]
Alafu ziwa liko kama beseni maji yapo ugokoni hatua mbili mbele ni 500m kwenda chini kwahiyo unatakiwa ujue kuogelea kweli
Inaumiza sana, kijana mdogo anakatisha ndoto zake.
Sipati picha wazazi wana hali gani huko waliko, [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Siwezi fahamu ilikuwaje lkn kwa uzoefu wangu kuhusu kuogelea ni vyema ukawa unafahama historia ya eneo husika,mazingira yake hasa uwepo wa tope na mapango.

Huenda ukazama chini na ukanasa pangoni au topeni na hasa maji yakiwa hayajatulia (machafu) kiasi cha kutokukuwezesha kuona mbali pindi uzamiapo.

Lkn kuna ile ghafla huko eneo lenye kina kirefu bila kutarajia sasa ile kupima urefu wa kina cha maji kama siyo mzoefu wa kuogelea hupelekea kukosa msawazo (balance) na hivyo maji kukupeleka yatakako.
Duuuh hii hatarii sasa.
 
Back
Top Bottom