Mwanafunzi wa Cameroon atoa uzoefu wake wa kusoma nchini China

Mwanafunzi wa Cameroon atoa uzoefu wake wa kusoma nchini China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
微信图片_20230213104635.jpg


Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Pili cha Yaounde nchini Cameroon imefanya mkutano wa hadhara wa “Soma nchini China, changamsha maisha yako", na kumwalika Joseph Olivier Mendo’o, ambaye ni mhitimu wa Taasisi hiyo kutoa uzoefu wake wa kusoma nchini China. Takriban watu 200, wakiwemo walimu na wanafunzi wa Taasisi za Confucius, wanafunzi wa shule za sekondari wanaojifunza Kichina, na wajumbe wa sekta za elimu nchini Cameroon wameshiriki katika mkutano huo.

Mendo'o alisoma Kichina katika Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Pili cha Yaounde, na baadaye alipata fursa ya kwenda nchini China na kusoma katika Chuo Kikuu cha Beijing, ambacho ni moja ya vyuo vikuu maarufu zaidi nchini China. Kwa sasa, Mendo’o ni msaidizi wa Kituo cha Utafiti wa Mambo ya Afrika cha Chuo Kikuu hicho, na pia ni rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Afrika ya Chuo Kikuu hicho, na mwanzilishi wa Shirikisho la Vijana wa China na Afrika.

Mwezi Juni mwaka 2021, akiwa mmoja wa wawakilishi wa wanafunzi wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Beijing, Mendo’o aliandika barua kwa rais Xi Jinping wa China, na kupokea jibu kutoka kwake, jambo lililomfanya aamue kuchangia ushirikiano kati ya China na Afrika.

Wakati aliposoma katika Chuo Kikuu cha Beijing, Mendo’o alisafiri katika vijiji 30 nchini China, na kuwa afisa wa kijiji, ili kujifunza uzoefu wa China katika kupunguza umaskini.
 
Back
Top Bottom