BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kanda ya Ziwa, Elias Anania (20) kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu kupitia kundi sogozi la WhatsApp.
Inadaiwa mwanafunzi huyo amewataka wenzake kununua petroli na kuchoma askari polisi wenye sare popote watakakokutana nao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbroad Mutafungwa, alidai kuwa mbali na kuhamasisha askari kuchomwa moto, pia aliwataka wachome moto watumishi wa umma.
Alisema kijana huyo anadaiwa kusambaza ujumbe katika kundi hilo, akishawishi wenzake kununua petroli na vibiriti kushambulia askari wa jeshi hilo.
"Anashikiliwa kwa tuhuma za uchochezi, katika kuhamasisha hivyo, alidai kuwa vijana wamechoka, hivyo anawahimiza kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya maslahi yao na kudai haki zao za msingi," alisema.
Kamanda Mutafungwa alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
NIPASHE