Marahaba Mkuu 🙏
Kwa mujibu wa Sheria, kutoa ama kupokea Rushwa ni kosa kisheria. Rushwa ya ngono ni miongoni mwa aina mbalimbali za Rushwa tulizonazo kwenye jamii zetu.
Kwahiyo suala la mabinti kuombwa Rushwa ya ngono, ni kosa kisheria hivyo ni wito wangu Kwa mabinti wote wanaoombwa ngono huko maofisini ili kupewa huduma ni vyema wakaripoti tukio hilo ili hao waharifu waweze kukamatwa na kupelekwa Mahakamani.
Sisi Wazee tunawaheshimu hao mabinti as Kwa umri wanaweza kuwa sawa na umri wa mabinti zetu huko nyumbani.
Endeleeni kuwa na imani na Wazee 🤗