Mwanafunzi wa Kidato cha Tano aolewa kwa Tsh. 30,000 DC Mtatiro aingilia kati na kuvunja ndoa

Mwanafunzi wa Kidato cha Tano aolewa kwa Tsh. 30,000 DC Mtatiro aingilia kati na kuvunja ndoa

ok, sawa. Aliyekuwa anamuo hakujua kuwa ni mwanafunzi? Nchi hii wanafunzi hawaolewi hata kama tayari wana uwezo wa kuhimili maisha ya unyumba
Mwanafunzi ni nani kisheria

Ukimaliza form IV, form IV au au la saba ukawa mtaani we bado mwanafunzi ?
 
Sasa kama kaamua kuolewa kwa hiari yake, serikali inaingilia vipi? Mpaka anaolewa ina maana anajitambua kimakuzi na kijinsia.

Huko ni kumvunjia haki zake za faragha na mahusiano yake. Mtoto ni yule ambaye hayo mambo hayajui na viungo vyake havina uwezo wa kuhimili vitendo vya unyumba
Halafu hawa wapumbavu wanatumia mabilioni kuhimiza ushoga na ufirauni.
 
Watu wanaongea tu kwa sababu sio mtoto/ndugu yao.Nyie mnaona huyo binti kuozeshwa huo umri ni sawa?ilhali angesoma na kuja kuondoa umasikini huko kwao.Embu acheni akili za kijinga DC Mtatiro yupo sawa na apewe maua yake!Kwa sasa wazazi wataona kama wamekosewa lkn baadae binti akija kupiga hatua watafuraji
 
Sasa kama kaamua kuolewa kwa hiari yake, serikali inaingilia vipi? Mpaka anaolewa ina maana anajitambua kimakuzi na kijinsia.

Huko ni kumvunjia haki zake za faragha na mahusiano yake. Mtoto ni yule ambaye hayo mambo hayajui na viungo vyake havina uwezo wa kuhimili vitendo vya unyumba
Kuyajua hayo mambo na viungo kuwa tayari si utashi wa mtu kuwa tayari kushiriki mambo hayo. Hukuona hapo akikataa kusoma, ndio maana wengine wote wako matatani.
 
Watu wanaongea tu kwa sababu sio mtoto/ndugu yao.Nyie mnaona huyo binti kuozeshwa huo umri ni sawa?ilhali angesoma na kuja kuondoa umasikini huko kwao.Embu acheni akili za kijinga DC Mtatiro yupo sawa na apewe maua yake!Kwa sasa wazazi wataona kama wamekosewa lkn baadae binti akija kupiga hatua watafuraji
Mijitu mijinga sana, huyo anayesema hivyo hawamezi ruhusu Binti yake afanyiwe hivyo, watu sijui wakoje.
 
SIASA TU...HAKUNA NIA NJEMA YA HILI...WAPO TAYARI MABINT WALIWE KWA ZINAA MITAANI LAKINI SIO KUOLEWA...AKILI ZA SHEITWANI HIZI.
Ondo upuuzi wako hapa,
Vitoto vya sikuhizi kipo primary la nne kinaliwa, kwahio naye mlaji akitaka kuoa ndio aoe ili kuepusha zinaa?

Wewe mwanao upo tayari kukatisha masomo YA SEKONDARI kisa anaolewa?
Sishangai ndio maana mzee baba alioa katoto ka miaka 9 eti kisa ndoa.
Rubish kabisa.
 
Vibinti huko wanayajua mambo wakiwa wadogo

Ova
 
Mwanafunzi ni nani kisheria

Ukimaliza form IV, form IV au au la saba ukawa mtaani we bado mwanafunzi ?
Ukimaliza madarasa tajwa hapo juu wewe bado ni mwanafunzi mpaka matokeo(hitimisho la kile kilichokupekeka shule) yatoke ndio yataamua, ikatokea amefeli kesi ya uwanafunzi haipo, inakurudia ya Umri kama bado ni under 18.

Hata ukimaliza VI bado ni mwanafunzi ila katika kundi la mwanafuzi anayedhaniwa anajitambua anayeweza kufanya maamuzi yake mwenyewe.
 
Wanaoa au kula wanafunzi akili zao huwa haziko sawa, wengine hutupiwa kimbola na kupigwa zongo. Unakuta mwalimu mkuu kamkandamiza mwanafunzi wake mpaka kampa mimba inashangaza sana. Huo mchezo wafanyiane wanafunzi kwa wanafunzi watajuana wenyewe kama walikuwa wanawakwa tamaa za miili yao wakaamua kujaribu kujionjea mpiko. Mtu mzima ni aibu na fedheha
 
Baada ya miaka 8 atarudi humu kutafuta mchumba wakati Muuza urembo akila ugali wa serikali.
 
Dah! Mzigo unaenda kuwaangukia walimu. Imagine unafundisha wake za watu, halafu unatakiwa uwafaulishe kwa namna yoyote ile.
 
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amevunja ndoa ya kinyemela ya kimila iliyokuwa imefungwa baina ya "Muddy Muuza Urembo" wa Tunduru Mjini na Binti aliyechaguliwa kujiunga na elimu ya Kidato cha Tano katika Shule ya Wasichana ya Masasi.

DC Mtatiro ameongoza vyombo vya usalama kuwakamata wazazi waliomuoza binti huyo pamoja na washenga waliohusika na akafanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa Muddy Muuza Urembo majira ya saa 6 usiku akiwa anaishi na binti huyu wa shule kinyumba kwenye Kijiji cha Muungano, Tunduru Mjini.

Mzazi wa binti amekiri kumuoza binti huyo kwa mahari ya shilingi 30,000 kwa madai kuwa binti hakuwa tayari kuendelea na kidato cha tano.

Hata hivyo, DC Mtatiro alivyomuhoji binti huyo, binti alikiri kutaka na kupenda kuendelea na masomo yake ikiwa atapewa nafasi hiyo.

Mtatiro amemkabidhi binti huyo kwa taasisi inayolea na kufadhili wanafunzi wilayani Tunduru iitwayo KALAMU EDUCATION FOUNDATION (KEF) ili ihakikishe msichana huyo anaendelea na masomo.

Makamu Mwenyekiti wa KEF ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Masonya Wilaya ya Tunduru, Bwanali amekiri kupata taarifa kuhusu binti huyo na kuahidi kuwa taasisi yao itamsimamia.

Mtatiro amesisitiza binti huyo atasimamiwa aendelee na masomo yake na kuendeleza ndoto yake na amewaasa Wazazi wa Tunduru kuachana na mambo ya zamani ya kuoza mabinti ambao wana nafasi ya kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa Taifa.

Watuhumiwa watano kwa jumla wanashikiliwa na Polisi wilayani Tunduru wakiendelea kuhojiwa juu ya kula njama na kumuoza binti huyo.
 
Back
Top Bottom