Verrazanno
JF-Expert Member
- Sep 15, 2021
- 454
- 1,011
Mwanafunzi ni nani kisheriaok, sawa. Aliyekuwa anamuo hakujua kuwa ni mwanafunzi? Nchi hii wanafunzi hawaolewi hata kama tayari wana uwezo wa kuhimili maisha ya unyumba
Ana miaka 20 utambue, sio mtoto, na wakati Mudy anamsalandia alikua keshamaliza form4 matokeo amekuja baada ya kuona tundakwanini aolewe binti mdogo hajamaliza chuo??
Halafu hawa wapumbavu wanatumia mabilioni kuhimiza ushoga na ufirauni.Sasa kama kaamua kuolewa kwa hiari yake, serikali inaingilia vipi? Mpaka anaolewa ina maana anajitambua kimakuzi na kijinsia.
Huko ni kumvunjia haki zake za faragha na mahusiano yake. Mtoto ni yule ambaye hayo mambo hayajui na viungo vyake havina uwezo wa kuhimili vitendo vya unyumba
Kuyajua hayo mambo na viungo kuwa tayari si utashi wa mtu kuwa tayari kushiriki mambo hayo. Hukuona hapo akikataa kusoma, ndio maana wengine wote wako matatani.Sasa kama kaamua kuolewa kwa hiari yake, serikali inaingilia vipi? Mpaka anaolewa ina maana anajitambua kimakuzi na kijinsia.
Huko ni kumvunjia haki zake za faragha na mahusiano yake. Mtoto ni yule ambaye hayo mambo hayajui na viungo vyake havina uwezo wa kuhimili vitendo vya unyumba
Mijitu mijinga sana, huyo anayesema hivyo hawamezi ruhusu Binti yake afanyiwe hivyo, watu sijui wakoje.Watu wanaongea tu kwa sababu sio mtoto/ndugu yao.Nyie mnaona huyo binti kuozeshwa huo umri ni sawa?ilhali angesoma na kuja kuondoa umasikini huko kwao.Embu acheni akili za kijinga DC Mtatiro yupo sawa na apewe maua yake!Kwa sasa wazazi wataona kama wamekosewa lkn baadae binti akija kupiga hatua watafuraji
Ondo upuuzi wako hapa,SIASA TU...HAKUNA NIA NJEMA YA HILI...WAPO TAYARI MABINT WALIWE KWA ZINAA MITAANI LAKINI SIO KUOLEWA...AKILI ZA SHEITWANI HIZI.
Ukimaliza madarasa tajwa hapo juu wewe bado ni mwanafunzi mpaka matokeo(hitimisho la kile kilichokupekeka shule) yatoke ndio yataamua, ikatokea amefeli kesi ya uwanafunzi haipo, inakurudia ya Umri kama bado ni under 18.Mwanafunzi ni nani kisheria
Ukimaliza form IV, form IV au au la saba ukawa mtaani we bado mwanafunzi ?
sheria inasema ukiwa chini ya miaka 18 we ni mtotoMwanafunzi ni nani kisheria
Ukimaliza form IV, form IV au au la saba ukawa mtaani we bado mwanafunzi ?
Alivyoona mapolisi na mibunduki yao lazima alipanik sasa anahamisha goli Kwa wengine.bandiko linasema amelazimishwa
hatakama, hichi walichokifanya hapo ni kizuri
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amevunja ndoa ya kinyemela ya kimila iliyokuwa imefungwa baina ya "Muddy Muuza Urembo" wa Tunduru Mjini na Binti aliyechaguliwa kujiunga na elimu ya Kidato cha Tano katika Shule ya Wasichana ya Masasi.
DC Mtatiro ameongoza vyombo vya usalama kuwakamata wazazi waliomuoza binti huyo pamoja na washenga waliohusika na akafanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa Muddy Muuza Urembo majira ya saa 6 usiku akiwa anaishi na binti huyu wa shule kinyumba kwenye Kijiji cha Muungano, Tunduru Mjini.
Mzazi wa binti amekiri kumuoza binti huyo kwa mahari ya shilingi 30,000 kwa madai kuwa binti hakuwa tayari kuendelea na kidato cha tano.
Hata hivyo, DC Mtatiro alivyomuhoji binti huyo, binti alikiri kutaka na kupenda kuendelea na masomo yake ikiwa atapewa nafasi hiyo.
Mtatiro amemkabidhi binti huyo kwa taasisi inayolea na kufadhili wanafunzi wilayani Tunduru iitwayo KALAMU EDUCATION FOUNDATION (KEF) ili ihakikishe msichana huyo anaendelea na masomo.
Makamu Mwenyekiti wa KEF ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Masonya Wilaya ya Tunduru, Bwanali amekiri kupata taarifa kuhusu binti huyo na kuahidi kuwa taasisi yao itamsimamia.
Mtatiro amesisitiza binti huyo atasimamiwa aendelee na masomo yake na kuendeleza ndoto yake na amewaasa Wazazi wa Tunduru kuachana na mambo ya zamani ya kuoza mabinti ambao wana nafasi ya kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa Taifa.
Watuhumiwa watano kwa jumla wanashikiliwa na Polisi wilayani Tunduru wakiendelea kuhojiwa juu ya kula njama na kumuoza binti huyo.