TANZIA Mwanafunzi wa mwaka wa Pili wa Chuo cha Misitu auawa kikatili

TANZIA Mwanafunzi wa mwaka wa Pili wa Chuo cha Misitu auawa kikatili

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Mwili wake ulikutwa mtupu jirani na korongo ukiwa umechomwa na vitu vyenye ncha kali pamoja na kufanyiwa ukatili

Tukio hilo la kusikitisha limetokea siku ya xmas

======

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Misitu Tanzania (FITI), Felista Daudi (21) ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye korongo katika eneo la Laliga mjini Moshi.

Mwili huo uliokotwa ukiwa bila nguo huku ukiwa umetobolewa sehemu mbalimbali kwa kitu chenye ncha kali, na ukiwa na viashiria pia vya kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa mwanafunzi huyo uliokotwa kwenye korongo.

“Ni kweli tukio limetokea la mwanafunzi huyu kuuawa na mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye korongo.

“Lakini dalili za kwenye eneo la tukio hazionyeshi aliuawa pale, inaonekana aliuawa katika sehemu nyingine na kisha kutupwa kwenye hilo eneo,” alisema Kamanda Makona. Makona alisema Jeshi la Poli-si linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wote walio-husika na tukio hilo.

“Juhudi za uchunguzi zinaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji haya na tayari simu za marehemu tunazo, tuna-chokifanya sasa tunafuatilia kujua mtu wa mwisho aliyewasiliana naye ni nani, ili hatua nyingine zichukuliwe,” alisema Kamanda Makona.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa utumishi wa chuo hicho, Havyalimana Nyamaliza alise-ma Desemba 25, mwanafunzi huyo alitoka na wenzake kwa ajili ya kusheherekea Krismasi na hakurudi nyumbani aliko-panga.

“Desemba 26 asubuhi nilipigiwa simu kuwa kuna mwili wa mwanafunzi wetu umetupwa na uko pembeni ya maji kwenye korongo, tulifika eneo la tukio kuutambua mwili ndio tukabaini kuwa ni mwanafunzi wetu wa mwaka wa pili.

“Tulipofika kwenye eneo la tukio mwili wa mwanafunzi wetu ulikuwa mtupu, akiwa amechomwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, ambapo kwenye ziwa upande wa kushoto na kwenye mbavu alikuwa amechomwa na kitu chenye ncha kali.

“Ni tukio lenye kusikitisha na lenye kuumiza, pia mwili ulionekana kama umefanyiwa ukatili (kubakwa), tunaomba Jeshi la Polisi kuhakikisha waliohusika na tukio hili wanakamatwa ili haki itendeke,” alisema ofisa huyo. Katika kipindi kama hiki mwaka jana pia kulikuwa na matukio kadhaa ya mauaji, kujeruhiana na kujinyonga.

Mwaka huu 2020 ulianza kwa Polisi Kilimanjaro wanamsaka mama na mtoto wa miaka 12, ambaye alikuwa anadaiwa kumuua kwa jiwe mpenzi wa mama yake mzazi aliyetajwa kuwa ni Serafin Mrema (29).

Pia, walikuwa wanasakwa wamuua kwa kumchoma visu polisi anayejulikana kwa jina la Living, ambaye alikuwa ametoroka lindo na kwenda kunywa pombe na askari mwenzake.
 
Mwaka huu 2020 ulianza kwa Polisi Kilimanjaro wanamsaka mama na mtoto wa miaka 12, ambaye alikuwa anadaiwa kumuua kwa jiwe mpenzi wa mama yake mzazi aliyetajwa kuwa ni Serafin Mrema (29).

Pia, walikuwa wanasakwa wamuua kwa kumchoma visu polisi anayejulikana kwa jina la Living, ambaye alikuwa ametoroka lindo na kwenda kunywa pombe na askari mwenzake.

Hizi aya Mbona hazieleweki?
Anyway, R.I.P Mdada..
 
Wanafunzi someni ndo kilichowapeleka huko vyuoni na starehe mtazikuta kuweni wavumilivu. By the way uchunguzi uanzie kwa waliotoka nae ili waseme waliachana nae vipi au na wa mwisho kumchukua. Ina lillahi wa ina ilayhi rajiuna.
 
Duh! aisee nimepita eneo fulani huku Goba usiku wa leo mida ya saa nane nikiwa kwa miguu...nimekuta gari Premio nyeupe imechomekwa vichakani kama inataka kuelekea mabondeni huko...nilienda kuchungulia kama kuna mtu yamemsibu nikaikuta tupu na wala haijaharika..nahisi imefanya tukio nikirudi mtaani ntaulizia kilichojiri.

Tuweni makini hizi sikukuu...RIP
 
Watanzania tunasafari ndefu kwakweli, hata polisi hawaja kamilisha uchunguzi kujua watuhumiwa na chanzo cha tatizo tayari mwana JF ashatoa conclusion, hebu tuache mizaha na issues zinahusu uhai wa binadamu wenzetu, huwezi jua nani anasoma hizi kejeli zetu humu halafu marehemu ni mtu wake wa karibu. Sio lazima kila mada humu ihusishwe na mapenzi, unless proven.
 
Back
Top Bottom