Mwanafunzi wa Shule ya Msingi aua mwenzake kwa ngumi


Got you.
 
Hili liwe fundisho hata kwetu watuwazima. Mtu anaanzisha ugonvi bila kujua unaegombana nae yupo katika hali gani. Pengine ana siku kadhaa hajala. Ni bora kuwa mpole. Tumuombee huyo mtuhumiwa aweze kupata msaada wa kisaikolojia maana asije kujenga usugu akaona kuua ni kitu cha kawaida.
 
mwanzoni jina limehidhiwa, lakini mwishini mwandishi amelitaja. waandishi wa bongo akili zao zinahitaji king'amuz kupunguza chenga
 
Sangara naweza kusema ndio au hapana. kweli kuna uhaba wa walimu na inawezekana hilo likatoa mwanya kwa wanafunzi kukaa bila kitu cha kufanya Lakini kuishutumu CCM sio sahihi kwani walimu wengi wanapangwa mikoa hii hawaendi. Wapo Dar na miji mingine wanatafuta kazi lakini kwenda kwenye vituo vyao ni shida.
 
Sophia na Mwalimu wa somo husika nao wakamatwe.

Wao wanakamatwa kwa lipi? Kosa la mwazimisha kitabu na mwl. wa somo wanahusikaje hapo hadi wakamatwe? Mwl. asifundishe? Sophy asiazimishe daftari kwa wenzie? Wewe ni askari nini? Hata askari aliepitia mafunzo hawezi kufanyia kazi ushauri wako huo.
 
jamani hao ni watoto tu ambao kupigana ni kawaida.....sidhani kama ni mara ya kwanza hao watoto kupigana na wenzao wengine, walimu watawasimamia hao watoto kila sekunde?? inaonyesha wengi humu mlikuwa watoto perfect hampigani wala nini? huo ni utoto sema bahati mbaya amempiga mwenzie kaanguka vibaya.
 
Sophia na Mwalimu wa somo husika nao wakamatwe.

Labda kwa sababu ya matakwa ya sheria ila hii sio kesi ni bahati mbaya kwani hawakuwa wanapigana bali kunyanganyana daftari. Aliyeua anatakiwa tu ahamishwe apelekwe mkoa mwingine la sivyo atakuwa haunted maisha yake yote na hilo tukio . Hii ni bahati mbaya tu jamani. Ila nawapa pole waazi wa pande zote.
 
Pole kwa wazazi wa marehemu! Kwa mazingira hayo wamshukuru Mungu tu, marehemu hana sheria! Ukifuatilia huyo mtoto aliempiga mwenzake na kumsababishia umauti, utakuta kwao kila siku wazazi wake ni kupigana. Kwetu shinyanga, loh tupunguze ukatili!
 
MFANO WA UANDISHI WA UKAJANJA

mwenye umri umri wa miaka 12 (
jina lake linahifadhiwa kutokana na umri wake),

alafu
marehemu alikuwa ameng’anga’nia daftari alilokuwa ameazimwa na Sophia Mathew kwa ajili ya kuandika ‘notes’ kitendo ambacho kilimkera mwenzake na kuzua ugomv
 
Hapana shaka hakuna ajuae atakufa lini na atakufaje,wamsamehe tu huyo mtoto by the way
 

Ina maana huyo Sophia ndo jina lake limehifadhiwa? Ok. Swali la 1. Ilikuwa ni muda gani mbona mwalimu hakuwa darasani ? Kwa kawaida wakati wa mapumziko watoto wanakuwa nje. Swali 2. Ilikuwaje hawa wakawa darasani? Mwalimu mkuu na mwalimu wa kipindi watatakiwa waeleze jinsi hii ilivyokuwa hata kama kaangukia kisogo na kufa. Lazima kulikuwa na fujo darasani.
 
kumbe unaweza kumpiga mtu ngumi akafa mimi sitampiga tena mtu ngumi ni viboko tuuuu.
 
R.I.P marehemu...kumbe vijana wa kanda ya hiyo ujasiri huwa wanazaliwa nao.........
 

Mkuu kuhamishwa ni hatua ya tawi.. Mzizi ni mtoto kupata ushauri toka wanasaikolojia ili kumrudisha kwenye njia.. Maana hapo alipo huyo mtoto atakuwa amebeba burden kubwa ambayo imezungukwa uoga..
 
Mwanafunzi amuua mwenzake kwa ngumi Shinyanga

THURSDAY , 26TH FEB , 2015

Mwanafunzi wa shule ya msingi Ilola kata ya Ilola, Itwangi wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani hapa, Sophia Mathew (12), anashikiliwa na polisi kwa kumuua mwenzake wakati wakigombea daftari kwa kumpiga ngumi kichwani na kuangukia kisogo.



Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi Justus Kamugisha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Longinus Tibishubwamu, amesema tukio hilo limetokea juzi saa 7:30 mchana, wakati wanafunzi hao wakiwania daftari walioazima waliposababisha ugomvi mkubwa.

Tibishubwamu amemtaja mwanafunzi amefariki dunia ni Veronica Venance (12), anayesoma darasa moja na mwenzake aliyesababishia mauaji hayo.

Akizungumza na East Africa Radio jana, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Magere Jonas, amesema wakati wanafunzi hao wanagombea daftari hilo, alikuwa amepumzika chini ya mti akiwa na mwalimu mkuu msaidizi, na ghafla wakaletewa taarifa na wanafunzi wenzao wanagombana darasani.

Jonas amefafanua mara baada ya kuingia darasani wakamkuta mwanafunzi huyo akiwa amelala chini anagalagala, hivyo kuchukua jukumu la kumkimbiza kwenye kituo cha afya Bugisi jirani na shule hiyo lakini kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo alifariki dunia.

Hata hivyo, mtendaji wa kata ya Ilola, Mahona Joseph, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza marehemu alikuwa ameng’anga’nia daftari alilokuwa ameazimwa na Sophia Mathew kwa ajili ya kuandika (notes) kitendo ambacho kilimkera mwenzake huyo na kuzua ugomvi.

Aidha, Kaimu kamanda wa polisi mkoani humo, Tibishubwamu, amesema wanamshikilia mwanafunzi huyo kwa mahojiano zaidi pamoja na kufanya upelelezi juu ya tukio hilo na uchunguzi utakapokamilika watamfikisha mahakamani ili kupewa adhabu inayostahili.

KWELI WALIMU TUNAYO KAZI!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…