Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Gazeti la MwanaHALISI linakiri kupokea barua kutoka Idara ya Habari – MAELEZO, ikimtaarifu Mhariri Mtendaji kuhusu uamuzi wa kusitisha leseni ya gazeti hilo kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia tarehe 19 Agosti 2026.
Katika barua hiyo, Idara ya Habari – MAELEZO imeainisha hoja mbalimbali kuhusu baadhi ya habari zilizochapishwa na MwanaHALISI na kuhitimisha kuwa gazeti hilo limekiuka misingi ya uandishi wa habari.
MwanaHALISI halikubaliani na hitimisho hilo.
Tangu kuanzishwa kwake Aprili 2006, gazeti limejikita katika uandishi wa habari unaogusa masuala yenye maslahi kwa umma, hususan habari za uchunguzi, uwajibikaji wa taasisi za umma na matumizi ya rasilimali za nchi.
MwanaHALISI linatambua na kuheshimu sheria za nchi, pamoja na wajibu wa kila chombo cha habari kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na misingi ya taaluma.
Aidha, tunaamini katika uhuru wa habari, haki ya wananchi kupata taarifa na wajibu wa vyombo vya habari wa kuhoji, kuchunguza na kukosoa masuala yenye maslahi kwa umma.
Kwa msingi huo, tunasisitiza kuwa kutokubaliana na maudhui ya habari au ukosoaji unaotolewa na chombo cha habari hakupaswi, peke yake, kutafsiriwa kuwa ni ukiukwaji wa misingi ya uandishi wa habari.
Pale ambapo kuna madai ya ukiukwaji, ni muhimu madai hayo yazingatie sheria, ushahidi, mazingira ya uchapishaji pamoja na haki ya mhusika kusikilizwa.
Kuhusu toleo lililopaswa kuwa mtaani Alhamisi, tarehe 20 Agosti 2026, wakati barua ya kusitisha leseni ilipopokelewa, toleo hilo lilikuwa tayari limechapishwa na kusambazwa katika vituo mbalimbali vya mauzo nchini.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa MwanaHALISI uliwasiliana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, kumjulisha kuwa gazeti lilikuwa tayari limechapishwa na kusambazwa, na kuomba utekelezaji wa uamuzi huo uanze baada ya toleo hilo.
Mawasiliano hayo hayakupatiwa majibu kwa wakati, jambo lililosababisha hasara kubwa kwa kampuni baada ya MwanaHALISI kusitisha usambazaji wa gazeti lake, kwa kuzingatia sheria za nchi.
MwanaHALISI litaendelea kutekeleza wajibu wake wa kufanya uandishi wa habari kwa maslahi ya umma, kuhoji pale inapobidi, kuchunguza masuala yenye maslahi kwa wananchi na kutoa taarifa kwa umma kwa kuzingatia sheria na misingi ya taaluma.
Soma Pia: Leseni ya Gazeti la MwanaHALISI yasitishwa kwa Miezi Sita
Gazeti hili halikubaliani na uamuzi wa kusitishwa kwa leseni yake kwa kipindi cha miezi sita na linahifadhi haki zake zote za kisheria kuhusiana na uamuzi huo, ikiwemo haki ya kuomba mapitio na kuchukua hatua nyingine zinazopatikana kwa mujibu wa sheria.
Bodi ya Wakurugenzi ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), wachapishaji wa Gazeti la MwanaHALISI, inatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki ili kutathmini suala hili na kutoa mwelekeo kuhusu hatua zinazofuata.
Tunawashukuru wasomaji wetu na Watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kutuunga mkono.
MwanaHALISI linapenda kuuhakikishia umma kuwa litaendelea kusimamia ukweli, uwajibikaji, maslahi ya umma na uhuru wa habari, kwa mujibu wa sheria.

KUHUSU TOLEO LA ALHAMISI

MWAHALISI KUENDELEA NA WAJIBU WAKE