Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). "amegoma kutumika kama kete ya maridhiano, MwanaHALISI limedokezwa.
Taarifa zinasema, kumekuwapo na juhudi kubwa zinazolenga kutaka kumtumia Lissu na kesi yake, kama mtaji wa kisiasa wa kuelekea maridhiano kati ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na chama kikuu hicho cha upinzani nchini.
Vyanzo vya taarifa kutoka serikalini, chama chake na ndani ya familia zinasema, msimamo huo wa Lissu, ndio umechangiza kuwapo "mvutano mkali kati ya CHADEMA na Lissu kwa upande mmoja na serikali kwa upande mwingine.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mvutano umeongezeka baada ya familia ya Lissu, kufanya mazungumzo na kiongozi mmoja mwandamizi serikalini, ili kusaidia kumalizika kwa kesi yake.
Mkutano kati ya ndugu wa Lissu na kiongozi huyo, ulifanyika jijini Mwanza, Januari mwaka huu.
Kiongozi wa serikali alikuwa amewahakikishia wenzake kuwa anaweza kulipatia suluhu sakata la Lissu kwa kuishirikisha familia badala ya chama chake.
Mtoa taarifa anasema, kiongozi huyo alikutana na familia ya Lissu iliyokubali wazo hilo, lakini walitaka kwanza wakazungumze na John Mnyika, katibu mkuu wa CHADEMA na viongozi wengine, kabla ya kufikia makubaliano.
"...familia ikamwambia kwamba Lissu, hatapenda kuona kwamba kuna mgogoro au mivutano kati ya familia na chama chake, na au kati ya mawakili wake na familia au chama ma chake na mawakili wanaomtetea. anaeleza mmoja wa wanafamilia wa Lissu kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Anasema, "Hivyo basi, wajumbe wa familia wakamueleza kiongozi, kwamba mpango wowote wa kumtenganisha Lissu na CHADEMA, hautaweza kufua dafu. Wakaomba wakiarifu chama chake, ndipo wasonge mbele."
Anasema, kiongozi aliyepewa jukumu la kushughulikia suala la Lissu, ambaye gazeti hili linahifadhi jina lake, alikubaliana na hoja hizo na akawataka warejee siku nyingine ili waweze kumpa mrejesho.
Anasema, moja ya masharti valiyotolewa na kiongozi huyo, lilikuwa Lissu au familia kuandika barua ya kuomba radhi kwa wakubwa ili shauri lake liweze kufutwa na kuwa huru.
Kiongozi mmoja mwandamizi wa CHADEMA, amelithibitishia gazeti hili, kuwapo kwa mpango huo, ikiwamo kufanyika mkutano kati ya ndugu wa Lissu na kiongozi huyo wa serikali, jijini Mwanza.
Alisema, "Wakati tukiwa pale Arusha tukijiandaa na mazishi ya Mzee Mtei (Edwin Mtel, mwenyekiti wa kwanza wa Chadema), ndipo tulipoelezwa kuwa baadhi ya ndugu wa Lissu, walikwenda Mwanza kukutana na kiongozi wa serikali, aliyekuwa ameahidi kulishughlikia suala hili
Mtei alipumzishwa kwenye makazi yake ya milele, nyumbani kwake, Tengeru, mkoani Arusha, Jumamosi ya 24 Januari mwaka huu
Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya mazishi hayo, ndugu wa Lissu, waliwataarifu baadhi ya viongozi wa CHADEMA, kuhusu mazungumzo yao na kiongozi wa serikali na kufikia hitimisho la kumshirikisha Lissu, anayezuiliwa mgerezani.
"Tukapanga kwenda gerezani Ukonga. Walienda watu wanne (anataja majina). Mwanafamilia wetu mmoja na viongozi watatu wa CHADEMA. Wakafanikiwa kumuona Lissu na baada ya mazungumzo kina wakakubaliana kwamba iandikwe barua ya kwenda kwenye mamlaka za serikali." amefafanua mwanafamilie huyo
Anasema, lakini mmoja wa mawakili wa CHADEMA waliokwenda gerezani kumuona Lissu, alitaka mshitakiwa mwenyewe kuandika barua hiyo, kisha mmoja wa wanafamilia aifuate na kuipeleka kwa Mnyika, ili kuichapa, kisha kusaini na baadaye kunakohusika kuiwasilisha "Kimbembe killanza hapo. Lissu aliandika barua ambayo badala ya kuomba msamaha alitoa masharti makali ya kuwapo kwa maridhiano. Mpango mzima ultishia hapo, anaeleza.
Anasema, "Mwanafamilia alipoenda gerezani Ukonga kuchukua barua ua hiyo, hata Lissu hakuweza kumuona. Nadhani hata hiyo barua yule kiongozi aliyetuambla iandikwe, haljamfikia.”
Anasema, "Barua haikutufikia kama ndugu wa Lissu. Mwanafamilia aliyekwenda kumuona gerezani hakufanikiwa kumuona wala hakukabidhiwa barua ambayo kwa utaratibu wa magereza inapaswa kupitia kwa mkuu wa Gereza.”
Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wakati kuna madai kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA, wamekuwa wakimtuhumu makamu mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, kukwamisha mazungumzo ya maridhiano kwa masilahi yake binafsi.
Hata hivyo, Heche amekuwa akikana madai hayo.
Anasema, "Kama mimi ninanufaika, basi wamuachie huru Lissu, ili nisiweze kupata hayo manufaa Anaongeza, "Waliomfungulia kesi, ndio wanufaika ndio maana wanaendelea kumshikilia. Tunachotaka sisi ni Lissu kuachiwa huru bila masharti. Na tutakwenda kwenye mazungumzo ya maridhiano, tukiwa tunaongozwa na Lissu."
Heche anasema, huo siyo msimamo wake binafsi ni maamuzi halali ya chama chake, kwamba "CHADEMA itakwenda tu kwenye mazungumzo, ikiwa imeambatana na Lissu na kwamba na yeye ndiye atakayetuongoza.”
Heche anasema, "Sisi ni waumini wa mazungumzo ya maridhiano yasiyo na hila, wala ghiliba. Tulishafanya hivyo, wakati wa Freeman Mbowe akiwa mwenyekiti. Tumeshaweka wazi tuko tayari kwa mazungumzo lakini kwanza wamuachie huru Lissu kwa kuwa ndiye atakayetuongoza kwenye mazungumzo hayo.”
Anasema, walioko madarakani, wanapaswa kuonyesha kwa vitendo dhamira ya maridhiano kwa kumuachia huru Lissu badala ya kuuhadaa umma huku wakiendelea na kesi inayompotezea muda na kumnyima haki zake.
Anasema, "Hakuna kitu kibaya kama kumpotezea mtu muda, yaani Lissu yuko ndani kwa miezi 15 hata ukimuachia leo hutaweza kumfidia muda mliompotezea. Mmennyima haki kipindi chote anachokaa gerezani. Maridhiano ya hila na unafiki hatuyataki."
Heche anasema, amepata ujumbe wa Lissu aliyemueleza kuwa wako kwenye njia sahihi wasiyumbishwe na yeyote anayetaka kuwaondoa kwenye reli ya kushinikiza kupatikana kwa Katiba mpya na kuachiwa kwake.
Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi, kumekuja siku moja, baada ya Lissu kuiambia mahakama kuwa baadhi ya nyaraka anazoletewa na mawakili wake, hazifikishwi kwake na uongozi wa gereza analoshikiliwa wakati wmusikilizaji wahshouri la kikatiba, lililofunguliwa na mawakili wake, wakiongozwa na William Maduhu na Paul Kisabo.
Miongoni mwa masharti yaliyowekwa na Lissu, ni pamoja na kutaka kuachiwa huru kabla ya kuingia kwenye mazungumzo ya maridhiano, serikali kuomba radhi kwa kilichotokea 29 Oktoba na kulipa fidia waathirika, kuhakikishiwa uwapo wa Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Lissu yuko gerezani kwa takriban miezi 15 sasa. akituhumiwa kwa uhaini, kufuatia matamshi yake yaliyotokana na kaulimbiu ya chama chake ya kushinikiza kuwapo mageuzi kwenye mifumo ya uchaguzi.
Chanzo: Mwanahalisi, Julai 23, 2026.