Marcossy A.M
Member
- Aug 21, 2008
- 61
- 24
Inabidi uanzishe uzi kujibu hoja zetu. Mimi nilisema kwamba mwanaharakati hatakiwi kukimbia kifo bali akabiriane nacho,unge itisha press conference na kutangaza hadharani kuwa kuwa wa2 wanakufuatilia kwa lengo la kukudhuru. Pepo hatoki bila kukemewa!
Naamini ujumbe huu utamfikia The Boss pia,
Kuwa kila kitisho cha usalama kina mazingira yake na namna yake ya kukikabili: Kukimbia ni moja ya mbinu ya kumkabiri adui popote! Na sasa nimerudi nikiendelea kutekeleza kile ninachoamini. Kwa taarifa tu, nilipata taarifa za kuwepo mpango wa uovu juu yangu na kushuhudia matendo yenye mashaka kwa usalama wangu. Kabla sijatafakari hatua za kuchukua wadau wangu wakanielekeza kuepusha shari wakati tunatafakari hatua za kuchukua. Niliporudi nikatioa taarifa vyombpo vya dola na kukutana na baadhi ya wadau. Hii ikiwa ni pamoja na kunipa nafasi ya kutafakari nini kinaendelea au kimetokea na kuwa ni namna gani naweza kukikabili vyema zaidi. Ni vyema mjue kuwa baadhi yetu huchukua hatua kulingana na uzoefu wetu wa matukio kama haya kwa wengine: waweza ukatoa taarifa kumbe bila kujua unaripotti kwa watesi wako!
Asanteni sana kwa kujali kwenu.